President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete
signs a condolence book at Zambia’s High Commissioner residence in Dar
es Salaam today following the death of Zambia’s President Michael Sata
early this week at a London hospital where he was receiving treatment.On
the left seated is the First Lady Mama Salma Kikwete and standing
second left is Zambia’s High Commissioner to Tanzania H.E. Judith
Kapijimpanga(photo by Freddy Maro)
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Friday, October 31, 2014
MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA HUDUMA KWA JAMII AMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE DAR LEO
MAKOCHA 35 KUSHIRIKI KOZI YA LESENI C YA CAF
Makocha 35 wameteuliwa kushiriki
kozi ya ukocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
itakayofanyika mjini Morogoro kuanzia Novemba 5 hadi 19 mwaka huu.
Kozi hiyo itaendeshwa na Mkufunzi
wa CAF, Sunday Kayuni na itafanyikia Mchikichini College ambapo
washiriki wote wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya ukocha vya ngazi ya
Kati (Intermediate) pamoja na vyeti vya kitaaluma vya elimu ya
sekondari (academic).
Washiriki wa kozi hiyo ni
Abdulmaliki Nemes (Airport FC), Ahmed Haule (Kilimanjaro Talented Youth
Sports Centre), Ally Jangalu (Moro Kids), Amri Saidi (Mwadui FC),
Athuman Kambi (Morogoro), Charles Mwakambaya (Burkina Faso FC), Damian
Mussa (Alliance One) na Daudi Sichinga (Kasulu United).
Denis Maneva (Shule ya Msingi
Logo), Edgar Juvenary (JUT- Mlale), Hamisi Mangolosho (Shule ya Msingi
Mtimbwilimbwili), Henry Ngondo (Chalinze Academy), Issa Hamisi (Polisi
Kilimanjaro), Jumanne Chale (Dar es Salaam), Kizito Mbano (Masasi
Alliance), Martin Saanya (Magereza Morogoro) na Masoud Gumbwa (Sokoine
University Academy).
Mbwana Makata (Oljoro JKT), Mrage
Kabange (Kagera Sugar), Muhibu Muhibu (Stand United FC), Nsubuga Solomon
(Kishoto FC), Nyamtimba Muga (Kizuka Secondary), Oscar Mirambo
(Makongo), Rashid Abdallah (Tech Fort Academy), Renatus Shija (Rhino
Rangers), Safari Nyerere (Elimu Sports Academy) na Said Lyakuka (Kizuka
Stars).
Simeon Mwesa (Mtibwa Sugar U20),
Simon Shija (Tabora), Suleiman Mtungwe (Ruvu Shooting), Swalehe Allawi
Abdul (Alliance Academy), Yasin Bashiri (Kick Off Sports Academy) na
Zuberi Katwila (Mtibwa Sugar).
Wakati huo huo, kutakuwa na kozi
ya wiki mbili ya ukocha ya ngazi ya Kati (Intermediate) itakayofanyika
jijini Dar es Salaam kuanzia Desemba 29 mwaka huu.
Makocha wote wanaotaka kushiriki kozi hiyo wanatakiwa kutuma maombi katika Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA).
BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LACHOCHEA UBORA WA UTENGENEZAJI SAMANI NCHINI
KAMPUNI ya Furniture Centre
(FCDL), na Shirikisho la Watengenezaji Samani Nchini (TAWOFE), wamesaini
makubaliano (MoU) kuongeza ubora wa bidhaa za samani zinazotengenezwa
nchini na kuzifanya zipate soko ndani na nje ya nchi.
Makubaliano haya yamekamilika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa
Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ikiwa ni mwendelezo wa
Tathimini iliyofanywa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
kwa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani, katika kuiwezesha sekta
ya Samani nchini kupitia vikundi na makampuni ya ndani.
Tathimini hiyo ya Baraza ya mwaka 2008, ilijikita katika kubaini
mahitaji na changamoto zinazoikabili sekta ya samani hapa nchini.
Baraza liliweza kuandaa warsha iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali na
ambapo matokeo ya tathmini hiyo yaliwasilishwa. Wadau kutoka sekta ya
umma na binafsi walishiriki katika mrejesho wa tathmini hiyo na wao pia
kuchangia maoni zaidi kwa ajili ya kuiboresha.
Washirika hao walisaini makubaliano hayo katika hafla
iliyoshuhudiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji wa
Uchumi na Uwekezaji), Dk Mary Nagu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dk Anacleti Kashuliza, alisema
pamoja na kuwepo kwa fursa kubwa ya soko la samani hapa nchini bado
ushiriki wa vikundi na makampuni ya ndani katika soko hilo ni mdogo sana
kulinganisha na samani zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.
Alisema tunatoa wito kwa taasisi za Umma na Binafsi ziunge mkono
jitihada hizi kwa kununua samani toka kwa watengenezaji samani wa ndani
na ili kuwapa ushirikiano zaidi utakaowezesha kuimarisha sekta ya
samani zitengenezwazo ndani ya nchi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAWOFE, Bw Fredrick Waibi,
alielezea makubaliano kati ya FCDL na TAWOFE ni mkakati mzuri
utaomjengea uwezo fundi seremala kuweza kutengeneza bidhaa zitakazoweza
kukubalika kimataifa, kuongeza tija kazini na kupunguza umaskini kati ya
mafundi seremala.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa FCDL, Bw Shafik Bhatia, alisema kama
wadau muhimu wa samani nchini wameona umuhimu na wanajivunia
kushirikiana na Tawofe katika kuboresha huduma za samani nchini .
Ajali mbaya yatokea jijini Arusha leo,watu tisa wapoteza maisha
Ajali
mbaya imetokea jioni ya leo katika eneo la Tengeru,Jijini Arusha
ikihusisha gari dogo aina ya Toyota Hiace (pichani juu) linalofanya
safari zake kati ya Usa River na Katikati ya mji wa Arusha na Lori la
Mafuta. Chanzo cha Ajali hiyo inaelezwa kwamba ni hiyo daladala lilikuwa
likijaribu kulipita gari jingine ndipo likakutana na loli hilo la
mafuta na kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya abiria wote
waliokuwa kwenye daladaa hilo ambao idadi yake haijafahamika
rasmi.taarifa kamili itawajia baadae kidogo.Picha na Dixon Busagaga wa
Globu ya JAMII Kanda ya Kaskazini.
BAADA YA KULALA GEREZANI SIKU MOJA =CHID BENZ APATA DHAMANA
Na : Mwene Said
Hatimaye
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemwachia kwa
dhamana Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo fleva), Rashidi
Makwaro (29), maarufa kama Chid Benz, baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya mahakaman hiyo.
Chid
Benz, alifikishwa mahakamani hapo jana akikabiliwa na mashitaka matatu
ikiwemo kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh.
38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na
kigae.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Warialwande Lema alisema mshtakiwa alitakiwa kuwa na
wadhamini wa wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazotambulika na wasio
walimu pamoja na kusaini hati ya dhamana ya Sh. milioni moja.
Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Inspekta Jackson Chidunda.
Wakili
Kombakono alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa Ndege wa
Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa
dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85.
Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.
Wakili
huyo wa serikali alidai kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza na la
pili, mshtakiwa alikutwa akiwa na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa za
kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni kosa.
Mshtakiwa alikana mashitaka yote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Hakimu Lema alisema kesi hiyo itatajwa Novemba 11, mwaka huu.
MIRADI YA UZALISHAJI CHACHU YA VIJANA KUACHANA NA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA INATOKANA NA UJASIRIAMALI
Kaimu
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC,Rukia Mtingwa wa kwanza kushoto
akimkabidhi hundi yenye thamani ya
shilling milioni 116,952,000 Mkurugenzi wa Kituo cha MAA MEDI bwana Furaha
Levilal wa kwanza kulia katika uzinduzi wa program maalum ya Vijana.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bwana James kajugusi akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano
wa Benki ya NBC,RuAkia Mtingwa alipokuwa akizindua Programu Maalumu kwa Vijana
itakayotolewa Kituo cha MAA MEDI.
Meneja
wa Miradi kutoka kituo cha MAA MEDI bwana Albany James akiongea na waandishi wa
habari katika uzinduzi wa programu maalum kwa Vijana iliyozinduliwa jana jijini
Dar es Salaam.
Baadhi
ya washiriki walioudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Maendeleo ya Vijana wakati wa uzinduzi wa Program maalum kwa Vijana
iliyoandaliwa na kituo cha MAA MEDI.
SERIKALI YA Burkina Faso YAMEGUKA.
Amiri jeshi mkuu wa jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore ametangaza kuvunjwa kwa serikali na bunge la taifa.
Jenerali Traore hata hivyo hakutangaza ni nani atakayechukua uongozi wa taifa hilo.
Jenerali Traore aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutaundwa serikali ya mpito baada ya kufanyika mazungumzo baina ya wanasiasa wa upinzani na kiongozi Bwana Campaore.
Jenerali Traore hata hivyo hakutangaza ni nani atakayechukua uongozi wa taifa hilo.
Jenerali Traore aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutaundwa serikali ya mpito baada ya kufanyika mazungumzo baina ya wanasiasa wa upinzani na kiongozi Bwana Campaore.
Jenerali Traore alikuwa akiwahutubia waandishi wa habari baada ya kushuhudia fuzo la maandamano katika mji mkuu wa Ouagadougou.
Mmoja wa wabunge nchini Burkina Faso akitorokea kuokoa maisha yake.
Waandamanaji walivamia majengo ya bunge na majumba ya wafuasi wa rais Blaise Compaore wakipinga azimio lake la kutaka kubadilisha katiba ya taifa ilikumruhusu kuwania kipindi kingine cha uongozi baada ya kutawala kwa zaidi ya miaka 27.
Awali Waandamanaji waliteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, na kuwafurusha wabunge .Runinga ya taifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika la utangazaji.
Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi.Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto.Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa.
Rais Blaise Compaore ameomba utulivu ,katika ujume aliotumwa kwa Twitter.Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore kuwania tena Urais mwaka ujao.
Uharibifu katika majengo ya serikali Ougadougou
Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa Blaise Compaore.
Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.
Compaore alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987.
Amekua akishinda uchaguzi lakini kura hio hukumbwa na utata.
Ufaransa na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania tena..
Mmoja wa wabunge nchini Burkina Faso akitorokea kuokoa maisha yake.
Waandamanaji walivamia majengo ya bunge na majumba ya wafuasi wa rais Blaise Compaore wakipinga azimio lake la kutaka kubadilisha katiba ya taifa ilikumruhusu kuwania kipindi kingine cha uongozi baada ya kutawala kwa zaidi ya miaka 27.
Awali Waandamanaji waliteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, na kuwafurusha wabunge .Runinga ya taifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika la utangazaji.
Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi.Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto.Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa.
Rais Blaise Compaore ameomba utulivu ,katika ujume aliotumwa kwa Twitter.Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore kuwania tena Urais mwaka ujao.
Uharibifu katika majengo ya serikali Ougadougou
Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa Blaise Compaore.
Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.
Compaore alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987.
Amekua akishinda uchaguzi lakini kura hio hukumbwa na utata.
Ufaransa na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania tena..
- 34 people like this.
- Godfrey Mgaza Jr. Hii inatakiwa tutoke siku moja kudai mapesa yetu yanayotafunwa na washenzi then tuwapupe kule Watawala ambao wapo kirushwa zaidi
- Godfrey Mgaza Jr. Maskini nchi hii yaani kuna mijitu sijui niite ''Mizimu au Mikundu''maake ipo ipo tu sasa kama haya masenge hapo juu Elly Madinda na hili lingine Khaleed Hafeed sasa mijitu kama hii ambayo ipo ipo haijitambui ila tu kwa kujipendekeza kwa Miccm ni shidaa sana kutoka.Kwanza issue iko kivingine kabisa yenyewe inakuja na issue zingine lol kaazi kweli kweli.
MISS TANZANIA 2014 SITTI MTEMVU KUVULIWA TAJI RASMI
WAKATI serikali kupita Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),
ikisema itakifuta cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti
Abbas Mtemvu, taarifa zinasema kwamba hawezi tena kuendelea na taji
hilo
imethibitisha kwamba uamuzi umekwisha kufanyika wa kumvua Sitti taji
hilo alilovikwa katika mazingira tata, uamuzi unaotarajiwa kutangazwa
wakati wowote kuanzia sasa.
Hata hivyo, haijafahamika kama hatua hiyo itachukuliwa na Baraza la
Sanaa Tanzania (BASATA) ama Sitti mwenyewe baada ya kubainika kwamba
taji hilo linazidi kuiweka pabaya familia ya Mbunge wa Temeke, Abbas
Mtemvu, ambaye ni baba yake.
Uchunguzi wetu umebaini kwamba hata hatua ya awali ya kuwania taji hilo ilichukuliwa na Sitti na baadhi ya wanafamilia bila kushirikishwa kwa Mbunge Mtemvu, jambo ambalo lilimsononesha awali katika ushiriki wa Miss Temeke, na kwamba Mbunge Mtemvu amekerwa na hali inayoendelea ikiwa ni pamoja na kuwapo utata wa cheti cha kuzaliwa cha mwanae Sitti, pamoja na kuwa anawajibika kisheria kwa anayoyafanya kutokana na kufikia umri wa zaidi ya miaka 18. Kwa upande wake, RITA imesema inaweza kukifuta cheti kilichotolewa Temeke na kuchukua hatua stahiki ikibainika kwamba alitoa taarifa za uongo wakati wa kuwasilisha maombi ya kukupata cheti hicho. Mtendaji Mkuu wa RITA, Philip Saliboko, leo Alhamisi Oktoba 31, 2014 amesema kwamba kwa sasa wanakamilisha uchunguzi wa kina kuhusiana na cheti hicho, baada ya kuibuka utata wa taarifa za kuwapo vyeti viwili vinavyotofautiana mwaka wa kuzaliwa. Baada ya kuibuka kwa utata huo, RITA ilianza upekuzi maalumu wa nyaraka alizowasilisha Sitti katika ofisi za RITA Temeke ili kubaini kwanza uhalali wa cheti, kabla ya kutafuta ukweli wa taarifa zilizowasilishwa chini ya kiapo. Kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Sura ya 108 Toleo la 2002), ni kosa la jinai kutoa taarifa za uongo kwa Msajili na pia ni kosa la jinai kughushi. Imeelezwa kwamba sababu kubwa ya kuchelewa kwa uchunguzi huo ni kutokana na uchunguzi huo kuhusisha nyaraka zote za watoto waliozaliwa Temeke katika miaka ya 1980 hadi 1992 kipindi ambacho Sitti anadai alizaliwa.
Katika mashindano ya Miss Temeke yaliyofanyika Jumamosi Agosti 23, 2014, Sitti aliyeibuka mshindi alidai amezaliwa mwaka 1991 kabla ya kupata cheti kilichodaiwa kutolewa na RITA Septemba 9, 2014 kikionyesha kazaliwa nyumbani (si hospitali), Temeke Mei 31, 1991.
Hati ya kusafiria ya Sitti inaonyesha alizaliwa Mei 31, 1989 na si 1991 kama alivyodai. Hati hiyo namba AB202696 ilitolewa Dar es Salaam, Februari 15, 2007. Hati hiyo ni ya pili baada ya hati ya mwanzo kwisha muda wake.
TAARIFA ZISIZO ZA KWELI KUHUSU UTEUZI WA KONSELI WA HESHIMA JIMBO LA GUANDONG, CHINA UFAFANUZI UMETOLEWA RASMI
Hivi karibuni kumezuka taarifa za upotoshwaji zilizotolewa kwenye
mitandao ya kijamii kwamba Serikali ya Tanzania imemteua Bw. Salaah,
Mkurugenzi wa Home Shopping Centre, (pichani ) kuwa Konseli wa Heshima
(Honorary Consul) kwenye mji wa Guangzhou kwenye Jimbo la Guandong.
Watoa
taarifa hizo, hawakutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai yao zaidi ya
kutoa picha mbalimbali za Bw.Salaah kutoka kwenye mitandao mingine ya
kijamii.
Taarifa hizo sio za kweli.
Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za mahusiano ya kidiplomasia ya China, nafasi ya Konseli wa Heshima
haitambuliki 'mainland' China. Kwa maneno mengine hakuna nchi yoyote
duniani inayoweza kuteua mtu kuwa Konseli wa Heshima katika eneo lolote
la China isipokuwa Hong Kong ambako kuna mamlaka huru za utawala
zinazofuata sheria zake.
Kwa
faida ya umma, ni vema kufafanua kwamba Nchi ya China inakubali nchi za
Nje kufungua Ubalozi kamili (Embassy) ambao makao yake yanatakiwa
kuwepo katika mji Mkuu wa China- Beijing na Konseli Kuu ama kwa lugha
iliyozoeleka Ubalozi Mdogo (General Consulate) ambao unaweza kufunguliwa
kwenye makao Makuu ya mji wowote ule katika Majimbo ya China.
Watu
wengi wamekuwa wakichanganya Ubalozi Mdogo au Konseli Kuu (General
Consulate) na Konseli (Ubalozi) wa Heshima (Honorary Consulate).
Konseli Kuu (General Consulate) ni sehemu ya Ubalozi (ndio maana wengi
huuita Ubalozi Mdogo) ambapo kiongozi wake na maafisa wake wote ni
watumishi wa Serikali kutokea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa. Masharti
ya kuwa Mkuu wa Konseli 'General Consulate' lazima uwe Afisa Mwandamizi
wa Mambo ya Nje mwenye uzoefu usiopungua miaka 10 ya Utumishi katika
Wizara ya Mambo ya Nje.
Kwa
muktadha huo, taarifa kwamba Bw.Salaah ameteuliwa kuwa Balozi wa
Heshima wa Tanzania huko Guangzhou sio kweli kwasababu Sheria za China
haziruhusu uwepo wa nafasi hiyo. Aidha, Bw Salaah hawezi kuwa Balozi
Mdogo (Consul General) kwa kuwa yeye sio mwajiriwa wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Hivyo habari zinazosambazwa kwenye
mitandao ya kijamii sio za kweli na zinalenga kuupotosha umma.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA MAMBO YA
NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
OCTOBER 30, 2014
KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YAMALIZA ZIARAYAKE KATIKA MGODI WA BUZWAGI
Kamati
ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira jana imekamilisha ziara yake
kwa kukagua mgodi wa Buzwagi na kuridhishwa na utekelezaji wa maagizo
yaliyotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na usimimamizi wa Mazingira
(NEMC) kwa mgodi huo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu akifafanua jambo mbele
ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira. Wa kwanza kulia ni
Mh. James Lembeli Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (katikati) akiambatana
wajumbe wa Kamati katika ziara ya kukagua bwawa la kuhifadhia maji
katika mgodi wa Buzwagi.
BREAKING NEWS:BASI LA SIMBA MTOTO USO KWA SUO NA LORI DARAJA LA WAMI,


Ajali mbaya daraja la Wami basi la Simba Mtoto na Lori baada break za Lori kufeli,
Dereva wa Lori amepoteza maisha hapohapo...
Mungu tunusuru na Ajali..Dereva wa Lori amepoteza maisha hapohapo...
Benki ya Exim katika Maonyesho ya Wiki ya Viwango yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
SKYLIGHT BAND INAKUKARIBISHA USIKU WA LEO THAI VILLAGE KWA BURUDANI YA KIPEKEE KABISA!
Kifaa kipya cha Skylight Band Bela Kombo akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo ndani ya ukumbi wa Thai Village Ijumaa iliyopita.
Binti
mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni Digna Mbepera kwenye hisia kali za
muziki wa Live kwa mashabiki wa Skylight Band ndani ya ukumbi wa Thai
Village Masaki jijini Dar.
Subscribe to:
Posts (Atom)










