TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, November 7, 2014

Shule ya Msingi Kawanzige iliyoko Halmashauri ya Mji wa Mpanda yaendelea kufanya vizuri

unnamed1
Mwanafunzi wa shule ya msingi Kawanzige wakicheza baada ya kutoka madarasani wakijiburudisha kwa michezo wakati wa mapumziko hapo shuleni.
……………………………………………………………………………
Na Kibada Kibada -Katavi.
Pamoja na Changamoto lukuki zinazoikabili Shule ya Msingi Kawanzige iliyoko Halmashauri ya Mji wa Mpanda  Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi nje kidogo ya Mji umbali wa takribani kilometa 30 kutoka  mjini bado shule hiyo imeonekana kufanya vizuri katika matokeo ya elimu ya Msingi kwa mwaka  yalitangazwa na Baraza la mitihani la taifana  kushika nafasi ya kwanza kwenye shule zilizoko kwenye  Halamshauri hiyo.
Shule hiyo ambayo imeshika nafasi ya kwanza kwa Halmashauri ya mji na kuzigalaghaza shule zilizoko mjini ambazo zinapata kila aina ya  mahitaji yote muhimu.
Shule ya Kawanzige yenye idadi ya walimu kumi  kati yao saba wa kiume na watatu wa kike ina Idadi ya wanafunzi Wanafunzi 484 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, ambapo wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba walikuwa wanafunzi 23 kati yao wanafunzi wa kiume walikuwa  na wakike
Shule hiyo ilishika nafasi ya kwanza katika halamshauri hiyo yenye shule 24 na nafasi ya pili kimkoa kati ya shule 159 nafasi ya 430 kitaifa kati ya shule 15867 za msingi nchi hivyo kuwa na wastani wa 174,0000.
Matokeo hayo yanaifanya shule kuwa moja ya shule bora pamoja na kuwa katika mazingira magumu kwa kutokuwa na vyumba vya madarasa wanafunzi madarasa tofauti kusomea kwenye chuma kimoja kwa wakati mmoja darasa la tatu na la tano, na wale wa darasa la kwanza na pili nao kuwa katika darsa moja huku wakiwa hawana madawati wakika chini changamoto ambayo inahitaji kupatiwa ufumbuzi.
Mbali ya changamoto hiyo kwa wanafunzi vitabu vya kiada na ziada ni shida maji hakuna matundu ya vyo ni shida,na walimu nao wanakabiliwa na changamoto lukuki kama ukosefu wa makazi bora, nyumba za kuishi hakuna,motisha kidogo kutoka kwa wakuu wao wa kazi hali iliyopelekea kutoa malalamiko yao kwa mkuu wa wilaya aliyetembelea shule hiyo kujionea changamoto zinazowakabili na kuwatia moyo waskate tama wawe na moyo wa kulipenda Taifa lao wakati Serikali inaendelea kushughulikia madai yao.
Pamoja na changamoto hizo bado walimu hao hawajakataa tama waliendelea kuchapa kazi kwa ushirikiano mkubwa na moyo wa kuipenda nchi yao pamoja na kuelewa changamoto zilizoko mbele yao hali iliyochangia kfanikisha ufaulu huo na kufanya vizuri huku wakiziacha mbali shule nyingine ambazo zinapata mahitaji muhimu na zina pata mahitaji muhimu ya huduma za kielimu na pia watoto wanasoma masomo ya ziada kwa kuwa hata umeme upuo.
Kutokana na hilo mkuu wa wilaya ya M,panda Paza Mwamlima amemwagiza mkurugenzi kupitia Idara ya Elimu Halmashauri ya mji kuona namna ya kuweza kuzipatia changamoto ufumbuzi na kuhakikisha madai na stahili za walimu wanatimiziwa ili waendelee kuchapa kazi na kulijenga taifa kwa kuelemisha watoto ambao watakuja kuwa viongozi wa baadaye wa Taifa hili.

TUZO ZA WANAMICHEZO BORA 2013/2014

index
MIFUKO ya hifadhi ya Jamii ya NSSF na PSPF imejitokeza kudhamini tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania ambazo zitafanyika Desemba 12 mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubilee (VIP), Dar es Salaam, zikiandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Udhamini wa PSPF katika tuzo hizo ni Sh. Milioni tano, wakati NSSF imetoa Sh. Milioni mbili, hivyo kufanya fedha taslimu ambazo hadi sasa TASWA imepata kufikia Sh. Milioni 37.
Wadhamini wengine ni Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) Group Limited iliyotoa Sh. Milioni 10 na Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL iliyotoa Sh milioni 20.
Uongozi wa TASWA unaendelea na mazungumzo na kampuni mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo, ambapo licha ya walioahidi kutoa fedha taslimu, lakini wapo wengine tunaendelea kuzungumza nao kwa ajili ya kudhamini kwa njia ya huduma zinazoambatana na tuzo hizo.
Ni imani ya TASWA kwamba hadi kufikia Novemba 20 mwaka huu kampuni na wadau mbalimbali walioahidi kutusaidia watakuwa wametekeleza ahadi zao kulingana na mazungumzo tuliyofanya nao, hivyo kuwatangaza rasmi.
Wanamichezo zaidi ya 100 wanatarajiwa kuwania tuzo kwa michezo mbalimbali, ambapo Kamati ya Tuzo za Wanamichezo Bora wa TASWA, inatarajiwa kukutana wiki ijayo kujiridhisha kwa mara ya mwisho orodha ya mapendekezo ya wanamichezo kutoka vyama mbalimbali vya michezo kwa ajili ya kuwania tuzo hizo.
B; MEDIA DAY BONAZA
TASWA kila mwaka inaandaa bonanza la vyombo vya habari linalojulikana kama Media Day Bonanza, ambalo hushirikisha wadau mbalimbali kutoka vyombo vya habari.
Lengo la bonanza hilo ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari, ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja.
Lakini  mwaka huu bonanza hilo limechelewa kutokana na na suala la wadhamini ambao awali TASWA ilikubaliana nao, lakini baadaye walisema wamepata matatizo ya kifedha.
Hata hivyo kutokana na umuhimu wa bonanza hilo, uongozi wa TASWA umezungumza na wadau wengine na mazungumzo hayo yanaendelea ili Media Day Bonanza ifanyike mwezi ujao likiwa ni maalum kwa ajili ya kufunga mwaka 2014.
Tunajua maswali kuhusu Media Day yamekuwa mengi pengine kuliko majibu, pia wasiwasi kwa baadhi yenu ni mkubwa kuliko uhakika, lakini tunawahakikishia mambo yanaenda vizuri na ni imani yetu yanakaribia kuiva.
Kwa hili la Media Day, tuliona ni bora tukawie kuliko kuvurunda. Tusikimbie kwa kasi bila kutazama tuendako. Tutambae, lakini macho njiani na mbele tunakoelekea na hiyo ndiyo dhamira yetu.

TANZANIA KUENDELEA KUHIFADHI MISITU KUISAIDIA DUNIA

GU9A7905Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) akibadilishana mawazo na kushoto ni Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD Kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Eduardo Rojas ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya misitu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na kulia ni Charles McNeill, UN-REDD Programme (UNDP) kabla ya kuanza kwa kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha.
Na Mwandishi wetu, Arusha
TANZANIA imesema ipo tayari kuendeleza juhudi za kimataifa za kupunguza kuendelea kuliwa kwa tabaka la ozone kwa kuhakikisha kwamba inatunza misitu na kuwaelimisha wananchi juu ya menejimenti ya misitu hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge wakati wa kufungua kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha.
Alisema ingawa Tanzania kwa sasa ina hekta milioni 48.1 za misitu na mapori ambayo sawa ni asilimia 55 ya eneo lake, Tanzania kupitia misitu hiyo inanyonya zaidi ya tani milioni 76 za hewa ya ukaa ingawa yenyewe inatoa chini ya tani hizo.
Hata hivyo alisema kwamba pamoja na juhudi za serikali kuna changamoto kubwa katika kutunza misitu hiyo ambapo kiwango cha ukataji wa misitu kwa sasa ni kiasi hekta 372,000 kwa mwaka sawa na asilimia 1.1 ya eneo la ardhi la nchi.
Katika hali ya kawaida na endelevu eneo linaloruhusiwa kuvuna kwa mwaka linaweza kutoa mita za ujazo milioni 42.8 kwa mwaka wakati mahitaji halisi ni mita za ujazo Milioni 62.3 kwa mwaka.
“Asilimia 92 za mahitaji ni kwa ajili ya nishati kama kuni na mkaa.” Alisema akionesha changamoto zinazokabili serikali ya Tanzania pamoja na ukweli kuwa mabadiliko ya tabia nchi tayari yameonesha ukali wake nchini.
GU9A7946Afisa Mawasiliano wa Sektretariet ya Program ya Umoja Mataifa ya-REDD, Jennifer Ferguson-Mitchell (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wanaohudhuria kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha.
Mabadiliko ya tabia nchi yanayotokana na kuzidi kwa joto katika tabaka la ozone kumesababisha kupanda kwa bahari wka sentimeta 19 na kusababisha baadhi ya visiwa katika pwani ya Tanzania kuzama kama cha Maziwe kilichopo wilaya ya Pangani.
Aidha alisema keundelea kuyeyuka kwa barafu ni dalili nyingine ya Tanzania kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi kwa hiyo taifa la Tanzania linajikita pamoja na mataifa mengine kuhakikisha kwamba programu ya Umoja wa mataifa ya kuhifadhi misitu inafanikiwa.
Aidha alisema kwa mazingira ya sasa ambapo tani milioni 1 ya mkaa huzalishwa nchini kwa mwaka huu nusu yake ikitumika jiji la Dar es salaam na majiji ya Arusha na Mwanza yakitumia kiasi kinachobaki kunahitaji juhudi za ziada kuongeza kasi ya upandaji miti kiasi cha hekta 185,00 kwa mwaka katika kipindi cha miaka 16 ijayo.
Waziri Binilith alisema pamoja na Tanzania na mataifa mengine ni laizma kushirikiana katika kupunguza kasi ya ukataji miti katika misitu huku wananchi wake wakisaidiwa njia nyingine ya kuendesha maisha yao.
GU9A7961Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge akisamiana na Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD Kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Eduardo Rojas ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya misitu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano kufungua kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha. Wa pili kulia ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD kutoka nchi wadau Dk Chea Sam Ang kutoka Cambodia Naibu Mkurugenzi Mkuu kitengo cha Misitu wizara ya kilimo, Misitu na Uvuvi.
Alisema mikakati ya kutunza misitu ili kupunguza kiwango cha joto duniani pia itasaidia kunyanyua uchumi wa wananchi, kuondoa umaskini na kutengeneza mtengamano wa mazingira na ekolojia hasa kwa jamii ambayo inategemea misitu kuwezesha maisha.
Waziri huyo aliwataka wadau waliopo katika mkutano huo wa siku mbili kujadili na kubadilishana uzoefu na kuhakikisha kwamba mkakati wa Umoja wa mataifa wa kukabiliana na mseleleko wa joto kwa kuwekeza katika kuhifadhi misitu unafanikiwa.
Umoja wa Mataifa una mpango wa kuhifadhi misitu unaojulikana kama Reduce Emissions from Deforestation and Forest Degradation (REDD+) unatarajia kuanza 2016-2020.
Wakati huo huo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza awali alishukuru mchango wa Norway katika kuwezesha utekelezaji wa programu ya UN REDD+ nchini Tanzania na maeneo mbalimbali duniani.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa mkutanoni hapo Norway imechangia dola za Marekani milioni 11 kuwezesha kutekelezwa kwa majukumu ya Umoja wa Mataifa katika kufanikisha programu hiyo katika nchi mbalimbali.
GU9A7967 
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiani na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge alipowasili kwenye ukumbi wa mikutano. Katikati ni Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD Kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Eduardo Rojas ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya misitu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO).
Utoaji wa hela hizo umeelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa kitengo cha kimataifa cha mabadiliko ya hali ya hewa katika Wizara ya hali ya hewa na mazingira ya Norway.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha Waziri Dk Binilith Mahenge, wawakilishi mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa mataifa (– UNDP, UNEP, na FAO),Sekretarieti ya UN REDD, wajumbe wa bodi ya sera ya UN REDD, Mashirika yasiyo ya kiserikali, Mwakilishi huyo wa UN alisema mafanikio yanayopatikana kwa sasa na duniani ni matokeo ya uwezeshaji wa Norway na wadau wengine katika mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuhifadhi misitu.
Alisema kazi ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa ni kuhakikisha wanatoa msaada wa kitaalamu na misaada mingine kuiwezesha serikali kutimiza wajibu wake.
Alisema Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na nchi nyingine 56 duniani wanaounda UN-REDD wamefanya vyema kuziwezesha nchi hizo kuwa tayari katika kutekeleza programu husika kwa manufaa ya nchi zao na dunia kwa ujumla.
GU9A8214Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge akisoma hotuba yake wakati akifungua kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha.
Alisema Tanzania kama nchi nyingine duniani zinazoendelea inakumbana na changamoto kubwa ya kuhifadhi misitu hasa kutokana na wananchi wake wengi kutegemea sana misitu kwa mambo mbalimbali yanayohusu maisha yao.
Aidha alisema kama taifa lina uwezo mdogo wa kusimamia sera na sheria zinazohusu hifadhi ya misitu.
REDD+ ambayo imeanza kutekelezwa nchini Tanzania mwaka 2008, mikakati ya utekelezaji wa mkakati huo imefanywa na kupitishwa na Bunge la Tanzania mwaka 2013.
Kukiwa na kikosi kazi cha kuwezesha kutekeleza UN REDD+ Tanzania pia imepongezwa kwa kuanzisha miradi tisa yenye lengo la kuwezesha utekelezaji wa malengo ya REDD+
Aidha katika utekelezaji wake serikali imejikita katika vipato vingine kwa jamii inayoishi karibu au ndani ya misitu kwa kuwa na kilimo kinacholinda mazingira na ufugaji nyuki.
GU9A8249Meza kuu kutoka kushoto ni Head, UN-REDD Programme-Secretariat, Bw. Mario Boccucci, Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD kutoka nchi wadau Dk Chea Sam Ang kutoka Cambodia Naibu MkurugenzI Mkuu kitengo cha Misitu wizara ya kilimo, Misitu na Uvuvi, Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD Kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Eduardo Rojas ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya misitu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na Thais Linhares-Juvenal kutoka sekretarieti ya programu ya Umoja wa Mataifa ya kuhifadhi misitu (UN-REDD) wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.
Alvaro alisema kutokana na mafanikio yaliyopatikana kwa sasa UN na serikali ya Tanzania wanakamilisha awamu ya pili ya UN REDD+ kwa kuangalia uzoefu uliopatikana katika awamu ya kwanza.
Utekelezaji wa awamu ya pili utafanyika mara tu fedha zitakapopatikana.
Naye Abbas Kitogo ambaye ni Meneja wa miradi ya nishati na mabadiliko ya tabia nchi (UNDP) alisema kwamba mkutano huo wa 13 utawezesha kubadilishana uzoefu wa sekta mbalimbali katika kutunza misitu huku wananchi wakiendelea kuneemeka.
Alisema nchini Tanzania kumekuwepo na miradi ya kujenga uelewa, kutengeneza mpango wa kutekeleza yanayotakiwa kufanywa na kujenga uwezo kwa wadau ili kujua REDD na kufuatilia athari za utekelezaji wa mradi huo.
GU9A8136Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma risala wakati wa ufunguzi wa kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge.
GU9A8261Pichani juu na chini ni wadau wanaohudhuria kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachoendelea kwenye hoteli ya Ngurdoto Jijini Arusha.
GU9A8296
GU9A8315
GU9A8055
GU9A8387Mkurugenzi Mkuu wa kitengo cha kimataifa cha mabadiliko ya hali ya hewa katika Wizara ya hali ya hewa na mazingira ya Norway, Bw. Morten Nordskag akitangaza mchango wa serikali ya kuchangia dola za Marekani milioni 11 kuwezesha kutekelezwa kwa majukumu ya Umoja wa Mataifa katika kufanikisha programu hiyo katika nchi mbalimbali katika kikao hicho.
GU9A7982Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwenye tete-a-tete na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.
GU9A8347Mmoja wa washiriki akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
GU9A8469Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ( wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD Kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Eduardo Rojas ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya misitu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) huku Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (katikati) akifafanua jambo kwa mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) wakati wa zoezi la kupiga picha ya pamoja.
GU9A8445
GU9A8466Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge kwenye picha ya pamoja na wadau wanaohudhuria kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika hoteli ya Ngurdoto Jijini Arusha.

SKYLIGHT BAND YAZIDI KUWABAMBA MASHABIKI WAKE WA MUZIKI WA LIVE, TUKUTANE BAADAE THAI VILLAGE

DSC_0225Majembe ya Skylight Band yakitoa burudani ya kukata na shoka kwa mashabiki wao Ijumaa iliyopita ndani ya ukumbi wa Thai Village Masaki jijini Dar..Kutoka kushoto ni Aneth Kushaba AK47, Mkongwe wa muziki wa dansi Joniko Flower, Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa bongo, Digna Mbepera na Sam Mapenzi.
DSC_0179Sehemu ya umati wa mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na sebene la Nasaka Dough ndani ya kiota cha Thai Village Masaki Ijumaa iliyopita.
DSC_0242Kikosi kazi cha Skylight Band kikiongozwa na rapa Joniko Flower kutoa burudani kwa mashabiki wake (hawapo pichani) Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha maraha cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0244Kutoka kushoto ni Aneth Kushaba AK47, Sony Masamba, Bela Kombo, Sam Mapenzi na Digna Mbepera wakijibu mapigo ya mashabiki wa Skylight Band kwa staili ya aina yake.
DSC_0254Mashabiki wa Skylight Band wakijibu mapigo kwa staili ya “Yachuma chuma”…Muguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma, Yachuma chuma nataka mukanda Yachuma chuma….raha iliyoje unakosaje sasa, fanya uje tukutane pale kati.
DSC_0255Na huku nako hawavumi lakini wamo kama inavyoonekana pichani.
DSC_0261Wadau nao wakaendelea kujiachia……Asanteni kwa kuja na kuitakia wito wa Ukodak kwa sana bila woga…!
DSC_0013Divas wa Skylight Band wakiongozwa na Meneja wa bendi Aneth Kushaba AK47 kutoa burudani kwa mashabiki wao. Kulia ni Bela Kombo na kushoto ni Digna Mbepera kwenye show iliyowabamba wakazi wa jiji la Dar Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0174Wadada warembo kama hawa wanapatikana Skylight Band pekeee…ni Kila Ijumaa ndani ya Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0017Digna Mbepera akifanya yake huku akipewa back up na Aneth Kushaba AK47.

NSSF YAWAKABIDHI NYUMBA WASANII WA ORIJINO KOMEDI

Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly (kulia) akimkabidhi msanii wa Orijino Komedi, Mjuni SilveryMpoki funguo ya moja ya nyumba za gharama nafuu walizokopeshwa wasanii  wa kikundi hicho na NSSF wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wasanii hao zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam hivi karibuni, mkopo huo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15. (Na Mpiga Picha Wetu)

ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kukopeshwa wasanii wa kikundi cha Orijino Komedi Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF) zilizopo katika mradi wa ujenzi wa Mtoni Kijichi jijini
Dar es Salaam.

Mac Reagan ‘Kipara’ na Mjuni SilveryMpoki wakiangalia moja kati ya nyumba walizokabidhiwa na NSSF baada ya kukopeshwa na Shirika hilo na mkopo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15.
Kushoto, Mac Reagan, Joti na Mpoki wakiangalia nyumba zao walizokabidhiwa na NSSF.
Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly akimkabidhi funguo ya nyumba msanii wa Orijino Komedi.  
Msanii Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’ akipokea funguo ya nyumba yake.

Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David ‘Seki’ akipokea funguo ya nyumba yake kutoka kwa Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly (kulia)
Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba kwa wasanii kikundi cha Orijino Komedi.
Msanii Mac Reagan akizungumza baada ya makabidhiano ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NSSF Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.

Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David ‘Seki’ akifafanua jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa nyumba.

SHINDANO LA MODEL OF TOURISM KUFANYKA NOVEMBA 22 MWAKA HUU JIJINI ARUSHA

Kiongozi wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiongea na washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha ambapo waliweza kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo
SAM_1055
Meneja Mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete akizungumza na washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha
SAM_1029
Kiongozi wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiteta jambo na mratibu wa shindano hilo Samdia Charles
SAM_1076
Mkurugenzi mkuu hifadhi za Taifa ,Tanzania Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha
SAM_1065
Mkurugenzi wa utalii na masoko Ibrahim Mussa akiwa anawasikiliza washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha (hawapo pichani)ambapo aliwataka washiriki hao kutumia nafasi hiyo kutangaza utalii wa ndani
SAM_1073
Mkurugenzi mkuu hifadhi za Taifa ,Tanzania Allan Kijazi akipata utambulisho kutoka kwa washiriki wa shindano hilo
SAM_1071
Washiriki wakipata picha ya pamoja nje ya jengo la makao makuu ya TANAPA jijini Arusha
SAM_1068
SAM_1042
Kiongozi wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiwa anatoa maelekezo kwa washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania
Na Pamela Mollel wa jamiiblog
Washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania wametakiwa kutumia fursa hiyo katika kutangaza utalii wa ndani hali itakayopelekea idadi kubwa ya watanzania kutembelea hifadhi za Taifa
Rai hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa utalii na masoko Ibrahim Mussa ,jana wakati washiriki wa shindano hilo walipopata fursa ya kutembelea makao makuu ya TANAPA jijini Arusha
Bw. Mussa aliwataka washiriki hao kutumia fursa hiyo katika kutangaza utalii wa ndani hali itakayo pelekea idadi ya watanzania kujitokeza kwa wingi kutembelea hifadhi za Taifa
Alisema kuwa ipo haja kwa watanzania kuona utalii ni sehemu ya starehe ambayo unaweza kujifunza hata ukiwa na familia yako tofauti na starehe zingineNaye Maratibu wa shindano hilo Samdia Charles alisema lengo la kuanzishwa kwa shindano hilo ni kuhamasisha utalii wa ndani na kutangaza vivutio vya nchi yetu kimataifa kupitia maonyesho ya mavazai kama vile new York fashion week,Paris fashion week na Victoria’s secret fashion show
Aidha alisema kuwa katika shindano hilo washiriki wametoka katika mikoa mbalimbali ya Dar es saam, Arusha,Iringa,Mbeya,Manyara,Singida,Kilimanjaro,Tanga,Tabora,Dodoma na Mwanza Shindano hilo lilianzishwa mwaka 2013 ambapo mwaka huu kuna jumla ya washiriki 19 kati yao 16 ni mabalozi wa hifadhi za taifa na shindano hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 22 novemba 2014katika ukumbi wa triple A jijini Arusha

KAMPUNI YA BIA YA MABIBO KUPITIA BIA ZAKE ZA WINDHOEK LAGER NA WINDHOEK DRAUGHT YAJITOSA MKOA KAGERA

 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr.James Rugemalira akizungumza na wadau mbalimbali wa mjini Bukoba wakati wa Promosheni ya bia za Windhoek Lager na Windhoek Draught katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo zilizofanyika Hoteli ya New Coffee Tree Inn mjini Bukoba leo usiku. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com simu namba 0712-727062)
 Fr.James Rugemalira (katikati), akisisitiza jambo  kwenye promosheni hiyo. Kutoka kushoto ni Mganga
 Mkuu wa Halmsahauri ya Wilaya ya Bukoba, Hamza
 Mugura, Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya
 inayofanya shughuli zake mjini Bukoba ya KADETFU,
Yusto Muchuruza, Mshauri wa Fr.James, Enic Kashasha
 na Andrew Kailembo.
Wadau wakiwa kwenye promosheni hiyo.
Mrembo huyu mnywaji wa Windhoek naye
 alikuwepo kwenye promosheni hiyo.
Mshereheshaji wa Promosheni hiyo, Andrew Kagya,  akiwajibika.
Meneja Mauzo wa Kanda ya Ziwa, Godfrey Mwangungulu, akielezea ubora wa Bia za Windhoek.
 Mdau wa Windhoek akifuatilia matukio yote kwa karibu.
 Hakika imependeza.
 Fr.James Rugemalira (katikati), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali.  Kutoka kushoto ni Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali mkoani Bukoba, Sakina Husein Sinda,Mganga Mkuu wa Halmsahauri ya Wilaya ya Bukoba, Hamza Mugura, Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya inayofanya shughuli zake mjini Bukoba ya KADETFU, Yusto Muchuruza, Mshauri wa Fr.James, Enic Kashasha na Andrew Kailembo, Mmiliki wa Walkgard Hoteli, Adventina Matungwa na Dk.Julius Zelothe.
 Wanahabari wakiwa kwenye promosheni hiyo.
 Wadau wakiwa kwenye promosheni hiyo
Promosheni imenogaaaa.
  Wadau wakiwa kwenye promosheni hiyo.
Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya inayofanya shughuli zake mjini Bukoba ya KADETFU, Yusto
Muchuruza,akichangia mada katika promosheni hiyo.
Hapa Windhoe imependezaaa ni tamuuuuuuu
 Wadau wakipata kinywaji cha Windhoek katika promosheni hiyo.
Meza kuu    hiyoooo,wanachangamkia Windhoek.