TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 9, 2013

RAIS MSTAAFU MZEE MWINYI AFUNGUA SKULI MPYA YA MAPINDUZI,CHAANI ZANZIBAR

 
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akifungua Skuli mpya ya ,Sekondari ya Mapinduzi Chaani ikiwa ni shamra shamra za kuadhimi miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR.
…………………………………………………….
NA RAMADHANI ALI /MAELEZO
 Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi amesema Zanzibar ni miongoni mwa nchi chache Duniani zinazoendelea kutoa Elimu bila malipo tokea kuasisiwa Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964.
 Akizungumza katika ufunguzi wa Skuli mpya ya Sekondari ya Mapinduzi, Chaani katika maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mzee Mwinyi amesema mafanikio hayo yanatokana na viongozi shupavu wa Mapinduzi na wale waliofuatia kuongoza Zanzibar.
 Amewapongeza viongozi na wananchi  wa Zanzibar kwa jumla kwa kuendeleza malengo  ya Mapinduzi ya 1964 ya kuimarisha maendeleo katika nyanja mbali mbali.
 Rais mstaafu amewahimiza wananchi kuendeleza Umoja kwani bila umoja na mshikamano hakuna maendeleo yatakayopatikana.
 Amewashukuru wahisani wanaosaidia   maendeleo ya Zanzibar hasa katika nyanja ya elimu na afya na amesema misaada yao itaendelea kuthaminiwa .
 Amewataka wazee wa Chaani kuendelea kuwasimamia watoto wao na kuhakikisha wanaitumia skuli hiyo katika kubadilisha uwezo wao wa kusoma kuwa bora zaidi.
 Akizungumza katika sherehe hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna amesema baada ya kupata msaada wa  skuli mpya 19 za sekondari na Benki ya Dunia na skuli mbili msaada wa BADEA, Wizara yake inatilia mkazo katika kuondosha tatizo la walimu wa sayansi linalokabili Skuli nyingi za Zanzibar.
 Amesema  Nigeria imewapatia msaada wa walimu 13 wa sayansi na tayari wamefanya mazungumzo na nchi ya Marekani, Uingereza, Ghana, India, Palestina, Misri na Oman na wote wameonyesha azma ya kusaidia kupunguza tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment