TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 9, 2013

TABOA YAMPONGEZA WAZIRI DK. EMMANUEL NCHIMBI KWA UAMUZI WA KUPUNGUZA VITUO VYA UKAGUZI

 
CHAMA cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(TABOA) kimepongeza hatua zilizochukuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Dk Emmanuel Nchimbi kupunguza kero katika usafiri wa mabasi iliyokuwa ikichangiwa na wingi wa vituo vya ukaguzi vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha kimemtaka Waziri huyo kudhibiti tabia inayofanywa na  baadhi ya mabasi yasiyo na leseni za usafirishaji, kusafirisha abiria kinyume na utaratibu uliopo,jambo alilosema litasaidia  kupatiakana kwa haki za abiria pindi tatizo lolote litakapotokea.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,Katibu wa Taboa Enea Mrutu alisema  hivi karibuni walimuomba Waziri huyo kuyafanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyoyopo barabarani, ikiwemo ya kupunguza vituo vya ukaguzi, jambo alilosema kuwa amelitekeleza kikamilifu na hivyo kuwaondolea usumbufu uliokuwepo.
Alisema mbali na kero hiyo pia Nchimbi amefanikiwa kudhibiti tabia ya baadhi ya askari waliokuwa na tabia ya kujificha vichakani na kujitokeza ghafla barabarani pindi wanapoona basi  limekalibia na kuliandikia faini  kwa madai kuwa lilikuwa katika mwendo mkali.
“Tunashukuru siku chache baada ya kulilalamikia suala hili na kumuomba Waziri kulifanyia kazi, tayari majibu yake tumeyaona na tunawaomba viongozi wengine wawe mfano wa viongozi hawa ambao mara nyingi hufanyia kazi kero zinazofikishwa mbele yao” alisema Mrutu.
Aidha alisema kumekuwepo na mabasi katika mikoa mbalimbali yanayofanya kazi ya kusafirisha abiria bila kuwa na leseni za usafirishaji, jambo alilosema ni hatari pindi ajali inapotokea na hivyo kumtaka waziri kulisimamia suala hilo kupitia kitendo cha usalama barabarani.

No comments:

Post a Comment