TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, January 7, 2013

WAZIRI MKUU AENDESHA HARAMBEE YA PAPO KWA PAPO KUCHANGIA UKARABATI WA VISIMA TISA

 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameendesha harambee ya papo hapo na kufanikiwa kuchangisha sh. milioni nane kwa ajili ya ukarabati wa pampu za visima tisa vya maji kwa wakazi wa kijiji cha Magamba, kata ya Magamba wilaya ya Mlele mkoani Katavi. 
Waziri Mkuu alilazimika kuendesha harambee hiyo jana mchana (Jumapili, Januari 6, 2013) wakati akijibu hoja za wakazi wa kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Magamba wilayani Mlele.
Kaimu Mhandisi wa Maji wa Wilaya hiyo, Bw. Enock Msengi alisema wanakijiji hao kupitia kamati ya maji walikuwa na sh. 150, 000/- kwenye akaunti yao. “Kama wangekuwa na fedha walau sh. milioni tatu, tungemudu baadhi ya gharama, lakini kwa hizi fedha alizochangisha Waziri Mkuu, tunaweza kukarabati visima vyote na vikafanya kazi… vinavyohitajika zaidi ni vipuri vya pampu,” alisema mara baada ya mkutano huo.
Akizungumza na wakazi hao, Waziri Mkuu aliwasisitiza watumie kilimo cha sesa ili kiwe mkombozi wao. Alipowaita mbele ya hadhara mabalozi wa mashina 18 na kuhoji kila mmoja wao analima ekari ngapi na anatumia kilimo gani, alibaini kuwa ni balozi mmoja tu ambaye anatumia kilimo cha sesa na amepanda kwa mistari na kutumia mbolea.
“Hawa wana ekari moja hadi ekari tano lakini wengi wao mmesikia ni matuta, matuta, matuta hata kwenye karanga wametumia matuta. Nawasihi sana mwakani kila mmoja atumie kilimo cha sesa kwa sababu kina tija zaidi kuliko hayo matuta… yanapoteza sehemu kubwa ya ardhi ya kilimo,” alisisitiza.
Waziri Mkuu ambaye alikuwa anamalizia ziara yake ya jimbo kwenye kata mbili kati ya 14 zilizobakia wakati wa ziara yake Desemba mwaka jana, aliwasihi mabalozi hao watumie umoja wa kikundi chao cha kilimo kuelimishana na akaahidi kuwatafutia majembe ya kukokotwa na ng’ombe ikiwa ni pamoja na kuwanunulia maksai ili waboreshe kilimo na wawe viongozi wa mfano.

WALIOFAULU DARASA LA SABA 2012 KWENDA KAWE UKWAMANI WARIPOTI SHULENI LEO

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kawe Ukwamani, jijini Dar es Salaa, Peter John (wa nne kushoto mwenye suruali) akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi walioripoti shuleni hapo leo asubuhi kwa ajili ya kuanza muhula wa masomo ya Sekondari baada ya kufalu mtihani wa darasa la saba wa 2012 na kuchaguliwa kujiunga na shule hiyo. Wanafunzi wote waliochanguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari Kidacho cha kwanza, na wale wa sekondari waliokuwa mapumzikoni, wametakiwa kuripoti shuleni hii leo kote nchini. Picha na www.sufianimafoto.blogspot.com

RAIS MSTAAFU KARUME AFUNGUA SKULI YA DONGE ZANZIBAR

 
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja  Pembe Juma Khamis mara alipowasili katika Ufunguzi wa Skuli ya Secondary huko Donge Muanda Kaskazini Unguja.
 
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akikata Utepe kuashiria Ufunguzi wa Skuli ya Secondary huko Donge Muanda Kaskazini Unguja.
 
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akikunjuwa Kitambaa kuashiria Ufunguzi wa Skuli ya Secondary huko Donge Muanda Kaskazini Unguja.
 
Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume akitia saini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuhudhuria Ufunguzi wa Skuli ya Secondary huko Donge Muanda Kaskazini Unguja.
 
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akipanda Mti katika Uwanja wa Skuli mara baada ya kufungua skuli hio ya Secondary huko Donge Muanda Kaskazini Unguja.
 
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akikagua baadhi ya madarasa ya skuli ya Secondary ya Donge Muanda ilioko huko Kaskazini Unguja.
 
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akitoa hotuba yake ya kufungua skuli ya Donge Muanda ilioko huko Kaskazini Unguja ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi.
 
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume katika picha ya pamoja na Maofisa mbali mbali katika hafla ya ufunguzi wa skuli ya Donge Muanda ilioko huko Kaskazini Unguja ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi.
 PICHA NA YUSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

YUSUF OMAR CHUNDA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUWA NA VITAMBULISHO (PRESSCARD)

 
 Na Radhia Abdalla      PEMBA                                                
 Mkurugenzi Idara ya Habari,Maelezo Zanzibar Yusuf  Omar Chunda amewataka waandishi wa Habari Nchini kuhakikisha kwamba wanafanya kazi zao wakiwa na leseni za uwandishi wa habari (PRESSCARD) ilikuhakikisha kwamba wanafanya kazi zao hizo    kwa mujibu wa sheriaNo5 ya mwaka 1988 ya magazeti .
 Hayo ameyaeleza leo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali huko katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Chake chake Pemba.juu ya utendaji wa kazi za Idara hiyo kwa mwaka 2012na kuomba mawazo yao kwa utendaji wa kazi kwa mwaka 2013.
 Amesema kuwa na kitambulisho   kitamrahishia mwandishi huyo kufanya kazi kwa mujibu wa sheri  na kupata habari anazozihitaji kwa wahusika bila ya matatizo ambazo  zitachapishwa na kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari.
 Mkurugenzi huyo amewataka waandishi hao kutopuuza agizo hilo la kuwa na kitambulisho kwani ni kwa faida yao wenyewe kutokana na kazi zao wanazo zifanya kila siku.
 Chunda amesema kuwa viongozi wasionekane wagumu pale wanapotaka kutoa habari kwanza kwa kuuliza waandishi vitambulisho vyao kwani wao wanahitaji kupata uhakika wa mwandishi huyo kama amepata kibali cha kuandika habari nchini kama sheria inavyotaka .
 Amesema kuwa ni vyema kwa waandishi kuelewa kazi zote zinakwenda kwa mujibu wa sheria kwa hivyo waandishi kama kioo cha jamii na wao wanastahiki kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na wawe mfano.
 Mkurugenzi huyo amewashukuru waandishi wa habari wote kisiwani Pemba kwa mashirikiano mazuri walioipa idara yake katika utendaji wa kazi kwa mwaka 2012 na amewataka mashirikiano hayo yawe endelevu ili kufanikisha shughuli za idara hiyo na Taifa kwa Ujumla .
 Aidha amewashukuru pia waandishi wa habari, viongozi wa dini pamoja na NGOs za habari kwa mashirikiano walioyatoa wakati wakutoa mawazo yao juu ya mabadiliko ya sheria No5 ya mwaka 1988 ya magazeti na Majarida Zanzibar

Wasanii watakiwa kushiriki Tamasha la Sanaa la Afrika Mashariki

 
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imewataka wasanii nchini kujitokeza kushiriki tamasha la sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambalo litafanyika nchini Rwanda mwezi ujao. 
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, kwa Niaba ya Katibu Mkuu, afisa Utamaduni Mwandamizi wa Wizara hiyo Makao makuu, Habibu Mohamed amesema tamasha hilo lijulikanalo kama JAMAFEST litafanyika kwa siku nane kuanzia Februari 9 hadi 16 mwaka huu.
“ Kwanza napenda kuwajulisha kuwa tumepata mwaliko wa kushiriki Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki, ‘JAMAFEST – 2013’  ambalo ni tamasha muhimu sana kwa wasanii wetu kushiriki katika hatua ya kutangaza na kuuza kazi zao katika soko la sanaa la Afrika Mashairiki,” amesema Habibu.
 Amesema kutokana na mwaliko huo wa Jumuiya, Wizara inatoa mwaliko kwa wasanii, asasi, vikundi, wabunifu wa mavazi na kampuni kwa hapa nchini, ambao zitaweza kufanya maonesho na kuuza bidhaa na huduma za Sanaa na Utamaduni, katika mabanda ya Tanzania kutuma maombi yao wizarani ambapo mwisho wa kutuma maombi ni Januari 25.
Amesema washiriki watajigharamia nauli ya kwenda na kurudi, chakula na malazi katika kushiriki tamasha hilo.

SHUKRANI ZA DHATI KUTOKA WATANZANIA WAISHIO NJE YA NCHI KWA RAIS DK.JAKAYA KIKWETE NA SERIKALI YAKE YA AWAMU YA NNE.

 
Naomba kuchukua fursa hii kutoa shukrani za dhati na wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete na Serikali yake ya awamu ya nne, kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba yaTawi la  CCM UK na nina imani kwa niaba ya wana jamii ya Wa-Tanzania Walioko Nje ya Nchi (Dispora)  kwa Ujumla, katika juhudi anazofanya kujumuisha Dispora Tanzania kwenye kuchangia maendeleao ya Nchi yetu.
Wana-Dispora tulio wengi tumeshuhudia kwa vitendo
tangu Rais Jakaya Kikwete na Serikali yake imeingia Madarakani , jitihada  na mikakati tofauti na iliyo wazi  ya Serikali Kuu  kutafuta mbinu za kudumu ili kushirikiana na kuwahusisha wana Diaspora, katika kuchangiamaendeleo ya Kiuchumi na Kijamii ya Nyumbani, Tanzania.
Nakumbuka Mheshimiwa Rais Kikwete katika kikao chake cha kwanza na Watanzania waishio Uingereza Mnamo mwaka wa fedha 2006/2007  pale Churchill Hotel, UK , katika Hotuba yake ambayo mbali na kutuelezea mafanikio na mikakati mbalimbali iliyopangwa na serikali yake kwenye utekelezaji wa Sera zake za ya awamu ya nne, kwa nia ya  kutimiza maazimio ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2005 na baadae 2010, vile vile alituahidi wana-Dispora kuwa atahakikisha yeye Binafsi atafanya jitihada zake zote kwa kadri ya uwezo wake aliyopewa na Mwenyezi Mungu  na Serikali yake haitusahau na katuacha nyuma Wana Dispora . Kilichoendelea baada ya Mkutano ule wana Dispora UK tulishudia thamani yetu kwa Serikali na Taifa letu ,kwani tumekuwa tukipewa kipaumbele kwa kila Kiongozi Mkuu wakiwemo Mawaziri na Wabunge wetu tofauti,  anapotembelea  Uingereza (na nina imani Nchi mbalimbali ) mbali na kuwa na ratiba zao ndefu za  kikazi, wanapata  muda wa kubadilishana mawazo nasi na tunaona matunda ya mchango wetu huu yameanza kuonekana ,licha ya kuwepo changamoto za kawaida zinazokabilika.  Hili  tunamshukuru sana Rais wetu kwa kulipa uzito unaostahili na kuonyesha mfano wa Uongozi wake bora na uliotukuka.
Kwa mara ya kwanza Tanzania Dispora  tumepata sauti na kuthaminiwa kwa wazi kwa Mchango wetu wa hali na  mali tunaorudisha nyumbani ili kuchangia Maendeleo . Wana-Dispora sasa  tunajivunia kupewa  na Rais wetu  jina la Mkoa . Baada ya kuanza na dawati la Dispora pale Wizara ya Mambo ya Nje, ili kuweka mfumo wa kudumu na kutimiza ahadi yake Mheshimiwa Rais mwaka ulipita 2012 aliteua Mkurugenzi wa Idara ya Dispora. Sasa tuna Idara/Kitengo kizima na si dawati tena. Kitengo/Idara yenye jukumu la kushughulikia mambo muhimu na tofauti ya Dispora. Hii ni hatua kubwa sana na ya muhimu na hatutaacha kumshukuru Rais wetu kwa kuliona na kulitambua hili na kutuletea matunda yake.

MIRAJI MRISHO KIKWETE ATEULIWA KUWA “MAKAMU WA RAIS” WA IBF/AFRIKA MAENDELEO YA VIJANA

 
Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Africa (IBF/Africa) limemteua bwana Miraji Mrisho Kikwete kuwa Makamu wa Rais anayeshughulikia maendeleo ya vijana katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati. Uteuzi wa Miraji unaanza January mwaka mpya 2013.
 Katika kumteua Miraji, Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati bwana Onesmo Ngowi alisema kuwa Miraji ana uwezo wa kuwahamasisha na kuwaunganisha vijana katika shughuli za maendeleo.
 Aliendelea kusema kuwa Miraji atakuwa anawahamashisha vijana, kuwaunganisha, kuwajengea uwezo wa kimaendeleo yatakayoratibiwa na IBF.
 Aidha, Rais huyo alisema kuwa Miraji atakuwa anabuni njia mbalimbali za kuwaunganisha vijana wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ili waweze kufaidika na miradi ya IBF ambayo inalenga kwenye elimu, kujenga vipaji pamoja na kuwaunganisha kwenye biashara ya utalii wa michezo.
 Katika mkutano wake wa mwaka uliofanyika katika jiji la Honolulu, jimbo la Hawaii, nchini Marekani hivi karibuni IBF iliupokea mradi wa “Utalii wa Michezo” uliobuniwa na kuwakilisshwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtazania Onesmo Ngowi.
 Lengo kuu la mradi huu ni kulifanya bara la Afrika hususan Tanzania kuwa kitovu kikuu cha “Utalii Michezo” hivyo kujenga uchumi imara. Nchi za Tanzania na Ghana ziliteuliwa kuwa nchi za mfano kwenye mradi huu.
 Katika mradi huu, IBF itatumia mtandao walionao katika nchi zaidi ya 203 duniani kuhamasisha wanachama wake na famlia zao, wapenzi pamoja na marafiki zao kuja Afrika/Tanzania kutalii pamoja na kuwekeza katika miradi mbalimbali.
 Uteuzi wa Miraji utasaidia kuwaunganisha vijana ili waweze kuchangia na kufaidika na biashara ya utalii kwenye mradi huu umefanywa wakati muafaka.
 Miraji ambaye ni Mjasiliamali amejipambanua katika maendeleo ya jamii na ana mchango mkubwa sana katima kuendeleza vijana nchini Tanzania.
 Rais Ngowi alimwelezea Miraji kama tegemeo ambalo vijana wanalihitaji kwani wanahitaji uhamasishaji wa hali ya juu na Miraji ana uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa kwani alishawahi kuifanya kwa kipindi kitefu.
 Miraji Mrisho Kikwete ni msomi wa chuo kikuu cha nchini Oman ambako amesomea elimu ya utawala wa biashara ambayo ndiyo lengo kuu la uteuzi wake. Ana haiba ya kupendwa na vijana pamoja na uwezo wa kujichanganya nao.

RAIS JAKAYA KIKWETE AANZA ZIARA YA SIKU NNE KATIKA MKOA WA TABORA

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipkea ripoti ya mkoa wa Tabora toka kwa Mkuu wa Mkoa Mhe Fatma Mwassa huo aliyosomewa mara baada ya kuwasili mkoani humo jana kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.
(PICHA NA IKULU)
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Tabora  Mhe Fatma Mwassa wakati alipokuwa akisoma ripoti hiyo mbele ya Rais mara baada ya kuwasili kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.

RAIS AHUDHURIA SHEREHE ZA KUSIMIKWA WAKFU ASKOFU DKT ALEX SEIF MKUMBO WA KKKT DAYOSISI YA KATI

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo (mwenye fimbo) pamoja na viongozi wa kanisa hilo wakiongozwa na Askofu Mkuu Dkt Alex Gehaz Malasusa (kulia kwa Rais), Msaidizi mpya wa Dayosisi hiyo Mchungaji Syprian Yohana Hilinti (wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Kone na viongozi wengine katika sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana Januari 6, 2013.
PICHA NA IKULU
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na kiongozi wa kanisa la KKKT nchini  Dkt Alex Gehaz Malasusa na  Askofu  mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana Januari 6, 2013

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na  kiongozi wa kanisa la KKKT nchini  Dkt Alex Gehaz Malasusa baada ya kupokea kamba kama ishara ya kupokea zawadi ya ngombe toka kwa Dayosisi  hiyo huku  Askofu  mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo akishuhudia  katika sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana Januari 6, 2013
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na  Wasaidizi wa Maaskofu wa Kanisa la KKKT baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo Januari 6, 2013
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Kanisa la KKKT baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana Januari 6, 2013

BARAZA LA MADIWANI ARUSHA LARIDHIA KUACHIA ENEO LA LAKILAKI

 
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu(TAMISEMI) Hawa Ghasia
 
Mahmoud Ahmad Arumeru
……………………………………..
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha, hatimaye  jana  januari 5.2013 limeidhinisha kuliachia eneo la Lakilaki  lililopangwa kujengwa mji wa mfano wa Arusha(Arusha Safari Town)  na kukabidhi hati miliki ya ardhi hiyo, kwa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Taasisi za  Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
 Maamuzi hayo, yalifikiwa jana katika kikao cha dharura ambacho, kilihudhuriwa na waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu(TAMISEMI) Hawa Ghasia,  baada ya serikali kukubali kulipa  mkopo  uliokopwa na halmashauri hiyo kutoka  Benki ya biashara ya Afrika(CBA) kiasi cha sh 8.6 bilioni pamoja na riba sambamba na kurejesha gharama za mradi huo kiasi cha sh 788.2 bilioni na faida ambayo halmashauri hiyo, ingepata kiasi cha sh5.6 bilioni.
 Akizungumza mara baada ya madiwani hao, kwa kauli moja kukubali kulitoa eneo hilo, Waziri Ghasia alisema Serikali imekubali kulipa gharama hizo, ili kuhakikisha inapatikana ardhi hiyo kwa manufaa ya Taifa zima.
 Waziri huyo, pia  alisema Rais Jakaya Kikwete alikuwa akifuatilia kupatikana kwa ardhi hiyo na ameiondoa hofu halmashauri hiyo, kupoteza fedha ambazo tayari wametumia na ambazo wangepata kama wangetekeleza mradi huo.
Hata hivyo, kabla ya madiwani hao, kukubali kutoa ardhi hiyo, walitaka uthibitsho wa maandishi wa Serikali kukubali kulipa deni la benki na gharama zote, hoja ambayo ilikubaliwa na waziri huyo, ambaye alisema tayari aliandika barua kwa halmashauri hiyo kueleza jinsi watakavyorejeshewa fedha zao.
 Awali mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha,  Halfani Hida alisema mradi wa awali kama ungetekelezwa tayari walikuwa wamepima jumla ya viwanja  348 ambavyo vingegawanywa kwa wananchi na kuipatia  halmashauri hiyo mapato ya sh 13.3 bilioni, pia viwanja vya biashara  vingeingiza mapato ya sh 1.7 bilioni huku maeneo ya huduma yalitarajiwa kuingiza sh 332.6 milioni.
 Eneo hilo la laki laki lina ukubwa wa ekari,  430 lilinunuliwa na halmashauri hiyo toka kwa Valahala Estate limited kwa sh 8.6 bilioni lakini wakati mradi ulipotaka kuanza ndipo mgogoro uliibuka baina ya halmashauri na watendaji wa serikali nje ya halmashauri na ndipo baadaye eneo hilo lilitwaliwa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya makazi  ambapo lilichukuliwa na wizara ya mambo ya nje

Rais Dk. Shein azindua Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi
wa Jengo la Bohari Kuu ya Dawa,Maruhubi Nje ya Mji wa Zanzibar jana
ikiwa ni shamra shamra za kilele  cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu
ya zanzibar,(kulia)  Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso
Lenhardt.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kama ishara ya uzinduzi
wa Jengo la Bohari Kuu ya Dawa,huko Maruhubi Nje ya Mji wa Zanzibar
jana ikiwa ni shamra shamra za kilele  cha miaka 49 ya Mapinduzi
Matukufu ya zanzibar,(kulia) ni Naibu waziri wa Afya Sira Ubwa Mamboya
na  Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso Lenhardt.[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa
Bohari Kuu,Said Mohamed,(kulia) alipotembela sehemu ya kuhifadhia
Dawa,baada ua uzinduzi wa Jengo la Bohari Kuu ya Dawa huko Maruhubi
Nje ya Mji wa Zanzibar,ikiwa ni shamra shamra za kilele  cha miaka 49
ya Mapinduzi Matukufu ya zanzibar,(wa tatu kushoto)  Balozi wa
Marekani Nchini Tanzania Alfonso Lenhardt.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu Kulia)pamoja na Viongozi
wengine akiwemo Balozi wa Marekani Nchini  Alfonso
Lenhardt.wakiangalia namna ya uchukuwaji dawa kwa kutumia mashine
maalum na kutoa nje ya Bohari kuu ya Dawa,baada ya ufunguzi rasmi jana
huko Maruhubi Nje ya mji wa Zanzibar,ikiwa ni shamra shamra za kilele
cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzíbar  
………………………………………………
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema uzinduzi wa Bohari kuu ya Dawa utaiwezesha Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar kupanga bajeti yake vyema ya dawa na kusaidia utoaji wa huduma za afya kwa ubora wa hali ya juu.
 Rais Shein ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Bohari Kuu ya Dawa iliyopo Maruhubi mjini Zanzibar ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar.
 Amesema Bohari hiyo ya kisasa ni matunda ya kujivunia ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo kwa hakika italeta tija katika upatikanaji wa dawa na uimarisha wa afya za wananchi.
 Dkt. Shein ameelezea matumaini yake kwa sekta ya afya kupitia Bohari hiyo na kwamba anaamini baada ya miaka mitatu Zanzibar itakuwa haipeleki tena Wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.
 Aidha Dkt. Shein amewataka watumishi wa Serikali kubadilika kiutendaji kulingana na kasi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa Bohari hiyo kuitunza vyema ili iendelee kutoa huduma kama inavyotakiwa.
 Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Sira Ubwa amesema Bohari hiyo itaboresha utoaji wa huduma kwa uhakika kutokana na ubora wa vifaa na mitambo ya kisasa ambapo wataalamu wataweza kubaini mahitaji ya Dawa zinazohitajika katika kila Hospitali za Unguja na Pemba.
 Kwa upende wao Mabalozi wa Marekani na Denmark wameelezea kufurahishwa kwao na juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha afya ya Wananchi hasa katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria na Ukimwi.
 Aidha wameahidi kuendelea kutoa mashirikiano kwa Serikali hasa katika huduma za Afya kwa Mama na Watoto, Elimu,Mapambano dhidi ya magonjwa ya maambukizi pamoja na uzazi wa mpango.
 Bohari hiyo iliyojengwa na Serikali ya Mapinduzi kwa msaada wa Shirika la USAID na NIDA inaelezewa kuwa ya tatu duniani katika viwango vya ubora ambapo jumla ya Dolla za Kimarekani Milion 1.2 zimetumika kukamilisha ujenzi wake.

TPBC KUFANYA UCHAGUZI FEBRUARY 2013

 
Onesmo Ngowi Rais wa TPBC
………………………………………..
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini TPBC) imetangaza kuanza kufanya uchaguzi katika ngazi ya mikoa kuanzia tarehe 20 February 2013.
 Katika chaguzi hizo, mikoa itafanya chaguzi zake kuwachagua viongozi wake katika nafasi za Kamishna wa mkoa, Katibu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mweka Hazina Msaidizi pamoja na wajumbe 10 wa Kamati ya Utendaji ya Mkoa.
 Mikoa ambayo itafanya chaguzi ni pamoja na Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Dar-Es-Salaam, Morogoro, Tanga, Pwani, Mwanza, Mara na Bukoba.
 Baada ya chaguzi za mikoa TPBC itafanya uchaguzi mkuu katika ngazi ya Taifa mwishoni mwa mwezi wa tatu (Machi) 2013. Wadau wa ngumi wanahimizwa kujitokeza kwa wingi ili waweze kushiriki katika chaguzi hizi.
Rais wa TPBC Onesmo Ngowi ameshatangaza kuwa hatagombea tena uongozi katika Kamisheni na kuwataka Watanzania wanaopenda mchezo wa ngumi kujitokeza ili waweze kuiongoza Kamisheni.


 MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imewaagiza wamiliki vyombo vya usafiri (mabasi ya abiria), kuacha mara moja kuweka matangazo ambayo yanapoteza uhalisia wa rangi iliyokubalika katika mkataba.
Akizungumza na FULLSHANGWEBLOG mwishoni wiki jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa Barabarani, Leo Ngowi, alisema utaratibu huo iliyozuka hivi karibuni hakubaliki kwa kuwa haiko katika makubaliano kisheria.
Alisema agizo hilo linawataka wale wote waliofanya hivyo kuhakikisha kuwa wanayaondoa matangazo yote ili kuondoa usumbufu kwa abiria.
Ngowi alisema wanaupinga utaratibu huo kutokana na ukweli kwamba hauko kwenye sheria, kwa wale watakaokaidi agizo hilo gari zao zitakamatwa kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria. 
“Kuna gari nyingi zimefanya hivyo, hususan  daladala ambazo zimepoteza kabisa uhalisia wa muonekano unaotakiwa hali inayoleta usumbufu kwa abiria wa maeneo husika.
“Tulikwisha wambia waache lakini naona bado wanaendelea kufanya hivyo, hivi karibuni niliwahi kuyakamata magari matatu kwa makosa kama hayo” alisema Ngowi
Akifafanua, Ngowi alisema kinacho kubalika ni matangazo madogo ya aina ya stika, na siyo yale yanayoharibu rangi za gari hizo kwa mfano kuna daladala zimeweka matangazo ya simtanki ambayo yamefunika bodi lote na kufanya gari hilo lisijulikane rangi yake halisi.
Ngowi alisema hivi sasa hakuna makubaliano hayo, hata hivyo, wako kwenye mchakato kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kupitisha hilo, lakini kwa sasa wasifanye hivyo.

WANANCHI KIJIJI CHA KICHEBA WALALAMIKIA UONGOZI WAO KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA MRADI WA MAJI (TALDO)

 
(MKUU wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Subira Mgalu)
…………………………………………………………….
BAADHI ya wakazi wa Kijiji cha Kicheba wilayani Muheza, Tanga wameutupia lawama uongozi wa kijiji hicho kwa kushindwa kusimamia kwa haki upatikanaji wa maji ya mradi wa ‘Taldo’ 
Akizungumza na FULLSHANGWEBLOG kwa njia ya simu kwa niaba ya wanakiji wenzake, mkazi huyo, Yusuf Issa, alisema hali ya upatikanaji wa huduma hiyo umevurugwa kabisa na viongozi hao kwa tamaa ya kujipatia fedha.
Alisema uongozi huo umevuruga utaratibu kwa kuruhusu baadhi ya watu kujiunganishia maji hayo kinyemela, huku wakisababisha vituo maalum vya umma  kukosa huduma hiyo, hivyo kulazimika kwenda kununua maji kwa watu hao tena kwa bei kubwa.
“Lengo  la kusaidia wanakijiji hao la kujipatia huduma hiyo kwa kuchangia  kiasi kidogo kwa ajili ya matengenezo inapotokea kuharibika kwa koki, limetoweka baadala yake limegeuzwa kitega uchumi cha baadhi ya viongozi kwa kuanzisha vituo vyao vya kuuza maji kinyemela majumbani mwao, kwa kila ndoo sh 500 ”alisema Issa.
Issa alisema watu hao wamevuruga njia zote za bomba kubwa linalopeleka maji katika vituo vya wananchi, ambapo kwa sasa upatikanaji wamaji umekuwa shida na wa kubahatisha kutokana na kuzibwa kwa mabomba hayo.
Alipoulizwa Mbunge wa wilaya hiyo, Hebert Mtangi kuhusu mgogoro huo, alisema  ndiyo kwanza anausikia, hata hivyo, alisema kama wamefanya hivyo hayo ni makosa kuwa hiyo asili ya mradi huo wa kuweka kuingiza maboma majumbani.
“Hayo ni makosa lakini kitu kikubwa kwanza nitakutana na diwani wangu anithibitishie hilo, kama lipo na baadaye waje wawaeleze wananchi kwenye mkutano wa hadhara kuwa kibali cha kuwaruhusu watu hao kuweka mabomba majumbani mwao kimetolewa na nani”alihoji Mtangi.
Mtangi alisema katika kijiji hicho kuna wenyeviti wa vitongoji, mwenyekiti wa kijii hata mwenyekiti wa maendeleo wa kata ambaye iweje yatokee hayo, acha nitakutana nao kwa ajili ya kupata taarifa kuhusu hilo.

WABUNGE WA MKOA WA ARUSHA WATAKIWA KUHUDHURIAVIKAO VYA ALAT ILI KUCHANGIA MAENDELEO YA MKOA

 
NA GLADNESS MUSHI -LONGIDO
WABUNGE wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha kuwa wanahudhuria kwenye vikao vya jumuiya za Serikali za mitaa(ALAT)na kuachana na tabia ya kukwepa vikao hivyo  kwa muda mrefu sana kwani michango ya wabunge inaweza kuimarisha jumuiya hiyo pamoja  na mkoa wa Arusha ambao unahitaji majibu badala ya maswali kutoka kwa Viongozi.
 Hayo yameelezwa jana wilayani Longido na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa kwa Tawi la Arusha(ALAT)Goodson Majola katika kikao cha wadau wa Jumuiya  hiyo na Viongozi wake
 Majola alisema kuwa wabunge wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanahudhuria vikao kwa kuwa wanajua na kutambua shida na changamoto mbalimbali ambazo zimo kwenye jamii lakini kama watakuwa hawahudhurii vikao bado jamii itaendelea kuwa na changamoto mbalimbali
 Aliongeza kuwa wabunge wanapokwepa vikao mbalimbali hasa vya jumuiya za Serikali za Mitaa kunasababisha  maendeleo kuwa hafifu sana kwenye jamii huku wannachi nao wakiwa  na hisia tofautitofauti juu ya utendaji kazi wa wabunge hao pamoja na Halmashauri zao.
 “Sasa hivi wabunge wanatakiwa kujua na kutambua kuwa jamii ambayo inaongoza haitaji maswali bali inahitaji majibu na hii pia ni hata ndani ya halmashauri zetu kwa hiyo mpaka sasa wabunge wanatakiwa kutumia Jumuiya hii na kushirikiana na kisha kutatua kero za jamii,lakini kama watakuwa wanakimbia vikao ni wazi kuwa Jumuiya hii haitaweza kufikia malengo yake”aliongeza Majola.
 Katika hatua Nyingine Katibu wa Jumuiya hiyo,Khalifa Idda alisema kuwa endapo kama wadau mbalimbali pamoja na watalamu wa Halmashauri zaa Mkoa wa Arusha wataweza kutumia Jumuiya hiyo vema basi wataweza kusaidia hata Halmashauri kuepukana na Hati chafu ambazo zimekuwa zikisumbua sana baadhi ya halmashauri.
 Idda alisema kuwa kupitia Jumuiya hiyo wataweza kujadili mambo mbalimbali ambayo yanasababisha na kuwa kikwazo cha hati chafu hivyo suala la hati chafu kutoka kwa mkaguzi mkuu wa Serikali (CAG)litakuwa ni ndoto hivyo kuongeza hata ufanisi zaidi wa kimapato.
 “Suala la hati chafu limekuwa kikwazo kikubwa sana kwenye Halmashauri zetu lakini kama watu watakuwa na umoja na watashiriki kwa undani sana kwenye ALAT basi wataepukana na hilo kwa kuwa hapa tutaweza kujadili kwa wale waliofanikiwa kuvuka na hata wale walioshindwa na wenyewe tutaelezana kisa kikubwa ni kipi hivyo ni vema kila halmashauri na wataalamu wake wakatumia vema jumuiya hiyo”aliongeza Idda

Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Mkoa wa Singida

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitumia laptop yake kuwaonyesha viongozi mbali mbali wa Mkoa wa Singida wakati alipokuwa akiwaelezea masuala muhimu ya maendeleo nchini.Rais Kikwete amewasili Mjini Singida Januari 5 kwa Ziara ya kikazi ya Siku Mbili.Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment