TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, August 14, 2014

MAGEREZA KUELIMISHA WAKULIMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au  namba +255767869133.
JESHI la Magereza mkoni Dodoma, limewataka wakulima na wafugaji wa mkoa huo kufika katika maeneo yao ya bustani ya ufugaji ili kupata elimu ya kisasa ya ukulima na ufungaji bora.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Magereza mkoa wa Dodoma, Kibwana Kamtande, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya kilimo na ufugaji bora kwa wakulima na wafugaji mkoani hapa.
Kamtande alisema licha ya jeshi hilo kutoa huduma kwa wafungwa pekee lakini pia limejikita kutoa huduma ya elimu ya kilimo na ufugaji kwa wananchi wa mkoa huu.
Kwa mujibu mkuu huyo, magereza zote za wilaya za mkoa wa Dodoma zimekuwa kikijishughulisha na kilimo na ufugaji sambamba na shughuli za kiujasiriamali kama utengeneza wa viatu, kufuma vitambaa na mashuka, utengenezaji wa  majiko na sabuni na ufyatuaji wa matofali.
“Wananchi wasiwe na fikra potufu juu ya jeshi hili bali waungane na sisi katika suala zima la kujikwamua na umasikini,”alisema.
Chanzo:Tanzania Daima 

No comments:

Post a Comment