TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, August 14, 2014

NEC YAFAFANUA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au  namba +255767869133.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Mstaafu Damian Lubuva, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akitoa ufafanuzi wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.(Mpiga Pucha Wetu)
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotarajiwa kuanza hivi karibuni linamhusu kila raia mwenye sifa ya kupiga kura.
Ufafanuzi huu umekuja wakati pakiwa na mawazo tofauti ya nani hasa anatakiwa kushiriki katika zoezi hilo, huku baadhi ya watu wakidhani kuwa jambo hilo linawahusu watu ambao hawakujiandikisha kupiga kura au waliopoteza kadi au waliofikia umri wa kupiga kura.

Mwenyekiti wa Nec, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, amesema jana jijini Dar es Salaam kuwa, katika kufanya maboresho hayo na kupata daftari linaloaminika zaidi, tume inatarajia kutumia mfumo mpya wa ‘Biometric Voters Registration System’, ambao utatumia utambuzi wa watu kwa alama za binadamu.

Alisema kwa kutumia mfumo huo, muhusika atachukuliwa alama za vidole vyote 10 vya mikono, picha na sahihi yake.

“Hii ni tofauti na mfumo uliokuwa unatumika wa ‘Optical Mark Recognition (OMR)’ ambapo muhusika alikuwa anajaza fomu na kuchukuliwa alama ya kidole kimoja tu ambao ulikuwa na uwezekano wa watu kujiandikisha hata mara mbili bila kutambulika” alisema na kuongeza. Watu wote wenye sifa watatakiwa kujiandikisha upya katika mfumo huu mpya na kupatiwa kadi mpya,” alisema.

Jaji Lubuva alisema uboreshaji wa daftari hilo unatokana na matakwa ya kisheria na malalamiko ya wadau mbalimbali.

Alisema tangu kufanyika kwa uchuguzi mkuu mwaka 2010 pamekuwa na malalamiko toka kwa wadau mbalimbali kama vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserikali na wapiga kura wenyewe kuhusu haja ya kuboresha daftari hilo na kuondoa watu ambao hawastahili kuwamo kama vile waliofariki na kuongeza wengine wenye sifa.

“Malalamiko haya yanafanya imani ya watu juu ya Daftari la Wapiga Kura iwe ndogo,” alisema.

Alifafanua kuwa, sheria inaitaka Nec kuboresha daftari la wapiga kura mara mbili kati ya uchaguzi uliopita na uchaguzi unaokuja.
“Ni kutokana na matakwa ya kikatiba na sheria na malalamiko haya, Nec imelazimika kufanya zoezi hili kabla ya kura ya maoni na uchaguzi mkuu ujao 2015,” alisema.

Akizungumzia matayarisho ya zoezi hilo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Mallaba, alisema yanaridhisha na kuendelea vizuri.

Alisema maboresho ya daftari hilo kwa awamu hii ni mahsusi kwa ajili ya kura ya maoni Katiba mpya itakayofanyika mapema mwaka 2015, uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na chaguzi ndogo zitakazofuata baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Mallaba alisema tayari Nec imeanzisha na kuhakiki vituo vipya na kuviweka katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa na kwamba  vimeongezeka kutoka vituo vya awali 24,919 na kufikia vituo 40,015 nchi nzima na tayari ununuzi wa vifaa vya uandikishaji ikiwamo ‘Biometric Voter Registration Kits’ umeshafanyika.
 
SOURCE: NIPASHE

No comments:

Post a Comment