TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, August 14, 2014

WANAFUNZI VYUO VIKUU KUMVAA PINDA KESHO

UMOJA wa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (TAHLISO) umetangaza kufanya maandamano ya amani kesho hadi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuishinikiza Serikali kulipa fedha zao kwa ajili ya Mafunzo kwa Vitendo.

Wanafunzi hao wametangaza uamuzi huo ikiwa ni wiki ya nane sasa tangu walipotakiwa kuripoti katika maeneo ya mafunzo ya vitendo, lakini kutokana na kukosa fedha wameshindwa kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Rais wa TAHLISO, Musa Mdede, alisema awali waliipa siku saba Serikali ili iwe imewalipa fedha wanafunzi lakini hadi sasa ni wiki ya nane hakuna fedha zilizopelekwa vyuoni.

Alisema mafunzo kwa vitendo ni muhimu kwani hiyo ni sehemu ya masomo yao na ikiwa hilo halitafanyika basi ni lazima mwanafunzi atarudia mwaka kutokana na kukosekana kwa alama ambazo lazima ziwepo ili kukamilisha masomo yake.

"Tumefuatilia sana hadi sasa, lakini hakuna kitu chochote kilichofanyika wanafunzi kutoka vyuo saba havijapewa fedha hizo, kitu ambacho kinaweza kufanya wanafunzi wengi kurudia mwaka," alisema na kuongeza;

"Baada ya kufuatilia kwa muda mrefu na kutoa siku saba ili Serikali ilipe fedha hizo ambazo ni sh. bilioni 1 hakuna kilichofanyika."

Mdede alisema kutokana na hali hiyo wanafunzi kwa sasa wameanza kuwa na wasiwasi kama watapewa fedha zao za kujikimu za mwezi Oktoba.

Alibainisha kuwa vyuo ambavyo hadi sasa havijapata fedha hizo ni Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),Theophilo Kisanji cha jijini Mbeya,Chuo cha Mt. Augustino cha Mwanza,Tumaini Makumira cha Arusha,Chuo cha Mt. Augustine Tawi la Tabora,Chuo cha Kumbukumbu ya Stephano cha mkoani Kilimanjaro,Chuo cha Jordan cha mkoani Morogoro na Chuo cha Bugando cha mkoani Mwanza.

Akizungumzia hali hiyo, Waziri wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Waziri Juma, alisema wamefuatilia kwa kipindi kirefu lakini uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HEALSB) ulisema hauna fedha.

"Tulikwenda Bodi ya Mikopo kupeleka kilio chetu na bahati nzuri tulikutana na Mkurugenzi wa Bodi hiyo na tulimwambia suala hilo, lakini alisema kama yeye angekuwa na fedha basi angewapa... lakini hakuna fedha; na Hazina haijapeleka fedha kwenye Bodi; hivyo fanyeni mnachoweza kufanya," alisema akimnukuu Mkurugenzi wa HEALSB

Chanzo:Majira


No comments:

Post a Comment