TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, August 13, 2014

MAMA, BABA WADAIWA KUMSULUBU VIBAYA MTOTO!

Mtoto anayetambulika kwa jina la Fadhili amekuwa akifanyiwa unyama na baba na mama yake wa kambo.
vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa watoto yamekuwa yakiendelea kufanyika kila siku licha ya kukemewa mara kwa mara, safari hii, baba na mama wakidaiwa kumsulubu mtoto wao.Katika hali ya kuonesha kwamba vitendo hivyo  bado vinaendelea kwa kasi, familia moja iliyopo Kunduchi jijini Dar imeshikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za ukatili dhidi ya mtoto baada ya kudaiwa kumsulubu kwa vipigo mfululizo mtoto wake aliyejitambulisha kwa jina la Fadhili (10).Chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa mbali na vipigo hivyo, mtoto huyo amekuwa akinyimwa chakula na kudaiwa kung’atwa meno na mdogo wake sambamba na kutakiwa kunywa mkojo wake ikiwa ni adhabu ya makosa anayoyafanya.
Majeraha ya mkononi aliyoyapata mtoto Fadhili kutokana na unyama wa baba na mama yake wa kambo.
“Yaani anayofanyiwa mtoto huyo ni ukatili mkubwa, tena nje ya umri wake, inafikia hatua hatazamiki kutokana na majeraha yaliyopo mwilini mwake. Mbaya zaidi hasomi shule na amekuwa mlezi wa baba yake ambaye amepooza,” 
kilisema chanzo hicho kilichoiomba OFM iingilie kati kwa kuwa suala hilo lilishawahi kuripotiwa kwenye ngazi ya serikali ya mtaa bila kufanyiwa kazi.
Majeraha mengine sehemu juu ya mkono.
Timu ya Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ilifika eneo la tukio kuhakikisha taarifa hizo ambapo ilibahatika kuzungumza na mtoto huyo ambaye alikiri kufanyiwa ukatili huo na wazazi wake.OFM ilishuhudia makovu mengi mwilini mwake jambo liliwafanya kufika kwenye Ofisi ya Mtendaji Kata ya Kunduchi ambao waliambatana hadi nyumbani kwa mtoto huyo.
Majeraha ya meno mkononi.
Baba mzazi wa mtoto huyo alikataa katakata madai ya mkewe kumtesa mwanaye.
“Mke wangu hahusiki na huyu mtoto, mimi ndiye nitakwenda kuyajibu hayo mashtaka kwa kuwa ni wangu na huyu si mama yake,  kama shule nimemsimamisha ili anihudumie hapa nyumbani kwa kuwa nimepooza,” 
alisema baba huyo.
Baba mzazi wa mtoto Fadhili akiwa na mke wake .
Hata hivyo jitihada za kuwafikisha ofisi ya mtendaji zilishindikana baada ya familia hiyo kuona ikiandamwa na OFM, lakini baadaye walijisalimisha wenyewe na kufikishwa kituo cha Polisi cha Kawe ambapo walifunguliwa mashtaka kwa jaladaKW/RB/6720/14 UNYANYASAJI.

No comments:

Post a Comment