TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, August 14, 2014

UKAWA:TUTAING'OA CCM UCHAGUZI 2015

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au  namba +255767869133

VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), vimetangaza kuunganisha nguvu kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia kuing'oa CCM madarakani.

Mkakati huo umetangazwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo wanachama wa chama hicho kuhusiana na namna ya kukabiliana na changamoto wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Mbatia alisema vyama vinavyounda UKAWA vya NCCR-Mageuzi, CHADEMA na CUF vitaungana kwa pamoja ili kuunganisha nguvu ya umma itakayosaidia kuing'oa CCM madarakani katika uchaguzi wa 2015.

"Wananchi wamekuwa wakilia kwa muda mrefu kutaka vyama kuungana na sisi tumelisikia hilo ndilo la maana kwa sasa; tumeanzisha mazungumzo ya vyama vinavyounda UKAWA kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuleta pamoja nguvu ya umma kwa ajili ya mwaka 2015," alisema Mbatia.

Alisema ili mtu aje kuwa Rais lazima ajipange na kuonesha kile alichonacho kwa jamii na baada ya hapo anaweza kutangaza nia yake, lakini si kukurupuka na ndio maana wao wanajipanga ili kuona nguvu ya wananchi inaletwa pamoja kupitia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

"Uchaguzi si mtu kuamka usingizini na kuamua kutangaza nia, bali unatakiwa ujipange ili kuona namna gani utaweza kuleta sera zako kwa jamii,mtu umeshindwa katika ngazi ya familia na Chama; itakuwaje uweze kuongoza Taifa kubwa kama Tanzania?" alihoji Mbatia.

Akizungumzia mchakato wa Katiba, Mbatia alisema wao kama UKAWA hawasimamii mawazo ya Chama kimoja; bali ni maoni ya wananchi kwa ujumla.

Alisema kitendo cha wao kukataa kushiriki vikao vya Bunge Maalum la Katiba ni kuonesha jinsi gani hata wakiamua kuungana lazima madaraka wayapate kwani wanasimamia kile wanachotaka wananchi.

Alisema mapendekezo yaliyopo kwenye rasimu ya Katiba ni ya muundo wa Serikali tatu. "Sasa iweje leo watu wapindishe ukweli,Katiba si ya mtu mmoja bali ni mawazo ya watu na sisi tutaendelea kusimamia msimamao wetu kwani hayo ndiyo maoni ya wanachi waliyotaka wao," alisema Mbatia.

"Leo inashangaza watu kudai kuna Muungano wakati Januari 12, mwaka huu wakati wa sherehe za Mapinduzi, Rais Jakaya Kikwete alipoenda Zanzibar aliingia Uwanja wa Amani kama si Rais, huku Rais wa Zanzibar akiingia kwa misafara na kwa kushangiliwa na umati wa watu," alisema Mbatia na kuongeza;

"Jambo hili linaonesha kuwa Zanzibar ni nchi na kilichopo shirikisho la nchi na ndo maana watu wana hoji uhalali wa Serikali mbili."

Alisema Watanzania wasahau kupata Katiba Mpya kwa sasa kwani licha ya Bunge hilo kuendelea lakini kuna mambo mengi ya kuifanya katiba hiyo isipatikane likiwemo kutokuwepo kwa Daftari la Kudumu la Wapiga kura.

"Kuendelea kwa Bunge hilo ni sawa na kufuja fedha za umma, kwani Daftari la Kudumu la Wapigakura ndilo linatakiwa litumike kwenye kura ya maoni ya kupitisha katiba hiyo lakini mpaka sasa tume ya Taifa ya uchaguzi bado haijatoa majibu ya kuaminika juu ya upatikanaji wa daftari hilo," alisema Mbatia na kuongeza.

"Tuliitwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi tukaambiwa mpaka sasa tume hiyo haina Daftari la Kudumu la Wapigakura na huu mfumo wa BRV wanaotaka kuutumia unahitaji umeme wakati huko vijijini umeme wenyewe hakuna... nchi nyingi zimejaribu mfumo huo zimeshindwa zikiwemo Kenya na Afrika Kusini, sasa sisi tutauwezaje wakati hao wenzetu walioushindwa wametuzidi kiuchumi na mpaka sasa bado hatujaona dalili za maandalizi juu ya Daftari hilo?" alisema.

Alisema inashangaza kuona hata wajumbe waliokuwa Dodoma wameongezewa siku na Rais kutoka 60 hadi 84 na kumfanya kila mjumbe kupata milioni 24.

Aliendelea kusema kuwa kinachotakiwa kwa sasa ni Bunge hilo kusitishwa hadi mwakani baada ya Uchaguzi Mkuu na wala si kuvunjwa.

Alisema Bunge la Jamhuri likae na kufanya baadhi ya mabadiliko kwenye Katiba iliyopo ili kuweza kuwa na uchaguzi ulio huru na haki.

"Bunge la Jamhuri likae na libadilishe baadhi ya vipengele kwenye katiba ya sasa," alisema na kuongeza kwamba, miongoni mwa vipengele hivyo; ni ili rais aweze kutangazwa mshindi na ni lazima afikishe asilimia 50 ya kura zote.

No comments:

Post a Comment