TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, December 30, 2013

WANARUNGWE KUANZISHA REDIO YA KUTANGAZA VIVUTIO MKOANI MBEYA

photo0027_2 
Na Kiza Sungura-MAELEZO
Wakazi wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wanakusudia kuanzisha Kituo cha Redio ya kijamii kwa ajili ya kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii na shughuli nyingine za maendeleo katika eneo hilo ili kuongeza kipato kwa wananchi wake na taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Mandalizi ya Harambee ya uanzishaji wa  Redio Rungwe FM Bw. Christopher Andendekisye  wakati akizungumza  waandishi wa habari .
Alisema kuwa Mkoa wa Mbeya na husasani Wilaya ya Rungwe inavyo vivutio vingi ambavyo kwa sababu ya kukosa chombo cha mawasiliano kama vile Redio vimekuwa havifahamiki kwa wananchi wengi wan je ya Wilaya hiyo na hivyo kuikosesha Serikali mapato ambayo yangetokana na sekta ya utalii.
Bw. Andendekisye alisema kuwa  kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili Wilaya Rungwe, Uongozi wa Christian na Gospel Ministry umeamua kuanzisha mchakato wa usajili Redio inayoitwa Rungwe FM, ikiwa ni Redio ya kijamii kwa ajili  ya kuhamasisha shughuli mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa ndani ya Wilaya ya Rungwe.
Alisema Redio hii tayari ipo katika orodha ya redio zilizoomba usajili wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA], imesajiliwa mwezi septemba mwaka 2013.
Kufuatia hali hiyo Bw. Andendekisye aliwaomba wananchi na wakazi wa Wilaya ya Rungwe kusaidia upatikanaji wa shilingi milioni 170 zinahitaji kukamilisha ununuzi wa vifaa vitakavyosaidia uanzishwaji wa redio hiyo mapema.
Aliongeza kuwa hadi hivi sasa wameshapata ahadi ya shilingi milioni 92 na kuongeza kuwa ili kumalisha kiwango chote wanatarajia kufanya harambee mwezi Machi 2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Bw. Andendekisye alisema kuwa kwa mwananchi atakayehitaji kuwachangia anaweza  kutuma fedha zake kupitia akaunti 038201043087 Tukuyu Christian Fellowship –NBC Bank

MABIBO BEER YADHAMINI MAADHIMISHO YA MIAKA MITANO YA UPIGAJI DISCO NCHINI!!

001 
 Ma Dj wakitoa burudani wakati wa kusherekea miaka mitano ya Grooveback Djs ambayo inaundwa na Ma Dj maarufu nchini,  Dj Peter Moe, PQ, Crucial, KT, Tony na JB, iliyofanyika katika bar maharufu ya East 24  iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Ma Dj waalikwa wa kimataifa waliokuwepo ni Dj Pinye na Dj Nijo kutoka Kenya. Grooveback wanapiga Disco la nguvu kila jumamosi East 24 Bar, Arcade House, chini ya udhamini wa Windhoek Lager – 100% PURE BEER.002Mashabiki mbalimbali wakipata burudani wakati wa Kusherekea miaka mitano ya Grooveback Dj003  
Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Mabibo, Jerome Rugemarila (katikati), akiwa na warembo wa kampuni hiyo.004 
Wana habari Dotto Mwaibale (kushoto), Faustine Kapama (katikati), wakiwa na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Mabibo, Boniface.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo,  Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo, Kelvin Coster alisema muitikio wa wapenzi wa muziki ulikuwa ni mkubwa.
 
“Mashabiki ni wengi mno waliofika kushiriki sherehe hii ya kutimiza miaka mitano ya upigaji muziki wa disco” alisema Coster.
Alisema kampuni hiyo iliamua kudhamini sherehe hiyo kupitia kinywaji cha Windhoek kinachopendwa na watu wengi kutokana na ubora wa kimataifa na bei yake kuwa nafuu.
 
” Napenda kusisitita kuwa Windhoek ni bia ambayo ukinywa haileti matatizo yoyote kama ya kuumwa kichwa,  mnywaji akiamka asubuhi atajisikia vizuri pasipo mzingio wa ziada” alisema Coster.
Alisema wanywaji wanapaswa kuzingatia kunywa bia yenye namba MB66 ambayo inauzwa kwa chupa sh.3,000 na katoni kwa sh.58,000 ambapo faida yake ni sh.14,000 na si vinginevyo.

MATOKEO YA UCHAGUZI WA KIKAPU YATANGAZWA DODOMA

MAPINDUZI CUP: SIMBA YAIKAMIA AFC LEOPARD MECHI YA UFUNGUZI, MATOLA KUONGOZA BENCHI LA UFUNDI, LOGARUSIC KUTUA JANUARI 2 !!

IMG_4773 

NYASI za uwanja wa Kinesi , jijini Dar es salaam zinaendelea kuhimili daluga za wekundu wa msimbazi, Simba SC, ambao wanajiandaa na mechi ya ufunguzi ya michuano ya kombe la Mapinduzi januari mosi, majira ya saa 2:00 kamili usiku dhidi ya AFC Leopard kutoka Kenya, nuwanja wa Amaan, kisiwani Unguja.
Simba iliyopangwa kundi moja na timu za  KMKM, AFC Leopard ya Kenya pamoja na KCC kutoka Uganda inaendelea kujifua chini ya kocha msaidizi, Seleman Matola `Veron`, huku kocha mkuu Mcroatia, Zdravko Logarusic `Loga` akitarajia kuwasili Zanzibar januari 2 mwakani.
Kaimu Afisa habari wa klabu hiyo, Stanley Philipo `Stan` ameuambia mtandao huu kuwa wanatarajia kuendelea na mazoezi leo jioni, huku wakitarajia kung`oa nanga jijini Dar es salaam kueleka Zanzibar jumanne (Desemba 31).
“Maandalizi ni mazuri sana. Ongezeko la wachezaji wapya na kocha mpya kumeleta mabadiliko katika kikosi, wachezaji wanajituma zaidi kutafuta namba kwani mwalimu hawajuii”. Alisema Stanley.
Stanley aliongeza kuwa kukosekana kwa kocha mkuu hakujaathiri chochote kwani Matola ni kocha mzuri na ataongoza timu  katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya miamba ya soka kutoka nchini Kenya, AFC Leopard.
“Mechi ya ufunguzi itatupa dira halisi ya michuano ya msimu huu. Tunaheshimu ubora wa Leopard, lakini tunajipanga vizuri kuhakikisha tunapata ushindi wa kwanza na kuongeza imani kwa mashabiki wetu”. Alisema Stanley.
Kaimu Afisa habari huyo alisema,  kombe la Mapinduzi ni nafasi nzuri ya kuandaa kikosi chao kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara, hivyo mashabiki watarajie soka zuri na la uhakika.
“Tumekuwa  wakati wa mpito kutengeneza timu, lakini sasa dawa imeanza kupatikana kutokana na mabadiliko ya kikosi na benchi la ufundi yaliyofanywa. Umefika wakati wa mashabiki wetu kupata burudani ya soka”. Alijisifu Stanley.
Wakati huo huo, kocha msaidizi wa Simba SC, Seleman Matola amejigamba kuwa mtihani aliopewa na bosi wake ataumudu vizuri katika mchezo wa kwanza huko Zanzibar.
Matola alisema klabu hiyo itashusha kikosi kamili , wala haina mzaha na mashindano hayo kutokana na umuhimu wake  katika kujenga kikosi chao.
“Simba itashuka na kikosi kizima. Malengo ni kutwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi”. Alisema Matola.
Logarusic na Matola walirithi mikoba ya makocha waliofukuzwa kazi, Abdallah Kibadeni na Jamhuri Kiwhelo `Julio` baada ya kumalizika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara, huku Simba ikiwa nafasi ya nne na pointi 24.
Mbali na mabadiliko ya benchi la ufundi, Simba imefanya usajili katika dirisha dogo na kuwaongeza kikosini makipa Ivo Philip Mapunda na Yaw Berko.
Wanandinga wengine ni Juma Awadh Issa, Ali Badru, Donald Mosoti, na Uhuru Seleman Mwambungu, ingawa TFF imewataka kufanya marekebisho katika usajili wao.
Zilibaki nafasi tano, lakini wamewaombea usajili wachezaji sita (6), hivyo wanatakiwa kupunguza,  kama watashindwa kufanya hivyo, kamati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanya yenyewe.
Kocha Logarusic anatarajia kuwatumia wachezaji wote ikiwa ni mikakati yake kuandaa kikosi cha kwanza cha ligi kuu soka Tanzania bara, ngwe ya lala salama inayotarajia kuanza kushika kasi januari 25 mwakani.
Mbali na Simba SC, timu nyingine za Tanzania bara zitakazoshiriki michuano hiyo ni mabingwa watetezi, Azam fc, Dar Young Africans na Mbeya City.

Ataka mawaziri wapewe meno

makamba 
“Waziri hana mamlaka ya kumwondoa mkurugenzi wa halmashauri, taasisi, shirika na katibu wa wizara yake kutokana na kubanwa na mfumo.” Makamba. 
…………………………………………………………………………….
Mwanza. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema ipo haja ya kubadili mfumo wa watendaji serikalini ili wanapoboronga nao wajibishwe na mawaziri.
Akizungumza katika mahojiano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini hapa, Makamba alisema mfumo uliopo sasa, hauwapi nguvu mawaziri  ili kuwawajibisha watendaji pale wanapokosea na badala yake unawabana wenyewe hivyo kuendelea kuwa kitanzi kwao.
“Mimi ni waziri, akikosea katibu nawajibishwa huyu anabaki, mimi siwezi kumwajibisha hivyo wanafanya lolote na sisi tunalazimishwa kuwajibishwa kisiasa kwa makosa ya watendaji,” alisema.
“Baada ya Kamati ya Maliasili Ardhi na Mazingira iliyo chini ya Mwenyekiti wake, James Lembeli kuomba kwa Spika kutumia ushahidi kwa kuweka kanda za video ili kuonyesha kilichotokea kwenye Operesheni Tokomeza Ujangili, hali ilichafuka ndani ya kikao cha Bunge na kila mmoja akawa na hisia na wengine kuanza kububujikwa na machozi na wabunge kuchangia hoja za kutaka mawaziri kuachia ngazi, hawakuangalia kiini cha tatizo, waliwabana mawaziri tu,” alisema.
Alisema Serikali kupitia mamlaka za juu, inapaswa kuangalia mfumo uliopo kwa lengo la kuubadilisha na kuingiza mapendekezo na mfumo mpya kwenye Katiba Mpya kuhusu uwajibikaji wa mawaziri na watendaji wakuu kwenye wizara, taasisi, idara, halmashauri na mashirika ya umma ambao ni wataalamu mbalimbali kuwajibishwa na mawaziri husika endapo kutaonekana utendaji wao haukidhi ama kwenda kinyume na maadili na sheria zilizopo.
CHANZO: MWANANCHI

Katiba: Mwelekeo mpya kujulikana

katibaWajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakitia saini Rasimu ya Pili ya Katiba juzi. Rasimu hiyo itakabidhiwa leo kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais Ali Mohamed Shein, Karimjee, Dar es Salaam. Picha ya mtandao. 
………………………………………………………………………………………………
Dar es Salaam. Swali la nini kilichomo katika Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya litajibiwa leo wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba itakapokabidhi rasimu hiyo kwa Rais Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.
Rasimu inayosubiriwa kwa hamu na wananchi wa kada zote itatolewa ikiwa imepita miezi saba tangu tume hiyo ilipotoa Rasimu ya Kwanza ya Katiba ambayo ilijadiliwa na kuboreshwa katika Mabaraza ya Katiba yaliyoketi kuanzia Julai 12 mpaka Septemba 2, mwaka huu.
Tume hiyo iliyoanza kazi Mei 3, 2012 kwa kukusanya maoni ya wananchi, iliandaa rasimu ya kwanza iliyotangazwa Juni 4, mwaka huu.
Hafla ya kukabidhi rasimu hiyo itafanyika leo saa 6.00 mchana katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na asasi mbalimbali.
Baada ya kukabidhi rasimu hiyo ya Katiba, Tume ya Mabadiliko ya Katiba itavunjwa kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Warioba ndiye atakayesoma rasimu hiyo kwenye Bunge Maalumu la Katiba linalotazamiwa kuanza vikao vyake Februari, mwakani.
Alipoulizwa nini kilichoongezwa au kupunguzwa katika rasimu hiyo, Jaji Warioba alisema: “Siwezi kueleza kama kuna kilichoondolewa au kurekebishwa… kesho (leo), Watanzania watapata fursa ya kujua mapendekezo ya tume, wasubiri.”
Baadhi ya mambo yanayosubiriwa kwa hamu kujua kama yamefanyiwa marekebisho au la kwenye Rasimu Mpya ni pamoja na mfumo na muundo wa Muungano, umri wa kugombea urais, wabunge kutokana na mikoa, umri wa kugombea urais na mengine.
Serikali Tatu
Tume ya Mabadiliko ya Katiba kupitia Rasimu ya Kwanza ilipendekeza kuundwa kwa Serikali Tatu na alipokuwa akizungumzia hilo wakati akitangaza Rasimu ya Kwanza, Jaji Warioba alisema uamuzi huo ulifikiwa kwa kuwa yalikuwa ni maoni ya wananchi walio wengi.
Hata hivyo, pendekezo hilo lilizua mjadala mkubwa kwani chama tawala, CCM, kilipinga na kuweka bayana kwamba kinataka muundo wa Muungano uendelee kuwa wa Serikali mbili.
Vyama vya upinzani kwa upande wake, viliunga mkono pendekezo hilo la muundo wa Serikali Tatu huku CUF kikienda mbali zaidi kwa kutaka Zanzibar ipewe mamlaka ya kuwa na dola kamili.
Katika Rasimu ya Kwanza ilipendekezwa mambo saba tu ndiyo yabakie kwenye mamlaka ya Muungano.
Mambo hayo ni pamoja na Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ulinzi na Usalama, Uraia na Uhamiaji, Sarafu na Benki Kuu, Mambo ya Nje, Usajili wa Vyama vya Siasa na Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na mambo ya Muungano.
Mambo hayo, ilipendekezwa na Tume hiyo kuwa chini ya wizara ambazo zitaongozwa na mawaziri wakazi ambao hawatatokana na wabunge kwani watatakiwa kuchaguliwa nje ya taasisi hiyo.
Kurejeshwa kwa jina la Tanganyika
Baada ya kutolewa kwa Rasimu ya Kwanza, mjadala mwingine ulioibuka hasa baada ya kupendekezwa kwa muundo wa Muungano kuwa wa Serikali Tatu ni hatua ya Tume kuendelea kutumia jina la Tanzania Bara.
Baadhi ya wadau walikosoa pendekezo hilo wakitaka jina la Tanganyika litajwe katika Katiba badala ya Tanzania Bara.
Katika Rasimu ya Kwanza, Tanzania Bara na Zanzibar zilihesabiwa kuwa washirika wa Muungano.
Ikiwa Serikali tatu zitarudishwa swali linakuja kama Tanzania Bara itatumia jina la Tanganyika ambalo ililitumia kuanzia mwaka 1961  hadi 1964 ilipoungana na Zanzibar.
Kufutwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu
Rasimu ya kwanza ilipendekezwa kufutwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu kwenye Serikali ya Muungano na badala yake kupendekeza kuwapo kwa Rais na Makamu wake.
Baadhi ya wadau walihoji juu ya usimamizi wa kazi za kila siku za Serikali jukumu ambalo kwa sasa lipo kwa Waziri Mkuu.
Umri wa kugombea urais
Suala hilo nalo lilizusha mjadala mkali wakati wa mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba Mpya.
Mapendekezo ya Rasimu ya Kwanza yalitaka moja ya sifa za mgombea urais kuwa miaka 40 lakini baadhi ya wanasiasa, hasa vijana, wametaka umri huo ushushwe hadi miaka 35.
Wagombea binafsi
Jambo jingine lililopendekezwa katika Rasimu ya Kwanza ni kuwapo kwa mgombea binafsi kuanzia ubunge hadi urais.
Hilo halikuwa na mjadala mkubwa miongoni mwa wadau mbalimbali kutokana na ukweli kwamba ni jambo ambalo limekuwa likipigiwa kelele kwa muda mrefu na wananchi.
Muundo wa Bunge la Muungano
Rasimu ya Kwanza ilipendekeza kuwa wabunge watakuwa 75.
Kwa maana ya 50 kutoka Tanzania Bara, 20 kutoka Zanzibar na watano kutoka kundi maalumu ambao watateuliwa na Rais kwa ajili ya kuwatetea watu wenye ulemavu.
Kwa mujibu wa mapendekezo ya Rasimu ya Kwanza, wabunge wa kuchaguliwa watagombea kupitia mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Rasimu ya kwanza ilipendekeza kuwa kila mkoa utachagua mbunge mmoja wa kike na wa kiume ili kuleta uwiano na kupendekeza kufutwa kwa viti maalumu suala ambalo lilizua mjadala.
Haki za Binadamu
Moja ya mambo ambayo yaliibuka mjadala ni haki za binadamu. Katika Rasimu ya Kwanza, ilipendekezwa kuundwa kwa Tume ya Haki za Binadamu itakayokuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wasiozidi saba.
Lakini wadau wengi waliotoa maoni yao walitaka sheria kandamizi 40 za Tume ya Nyalali zisiwepo katika Katiba Mpya.
Mambo mengine
Kuhusu madaraka ya Rais, Tume hiyo ilipendekeza katika Rasimu yake ya Kwanza kwamba yabaki kama yalivyo hasa kwa uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu, pia ashirikiane na taasisi na vyombo vingine katika uteuzi.
Katika Rasimu hiyo ya Kwanza, pia ilipendekezwa kusiwepo na uchaguzi mdogo, isipokuwa kama nafasi hiyo itaachwa na mgombea binafsi lakini kama ni wa kutoka katika chama cha siasa, ijazwe na mtu kutoka chama chake.
Kuhusu Tume ya Uchaguzi, Tume hiyo ilipendekeza katika Rasimu ya Kwanza kwamba jina la Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC), libadilishwe na iitwe Tume Huru ya Uchaguzi.
Rasimu hiyo, ilipendekeza kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu (Supreme Court), majaji wa Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani watateuliwa na Rais, baada ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.
CHANZO: MWANANCHI

WAZIRI MKUU MHE. PINDA AHUDHURIA JUBILEI YA KANISA KATOLIKI ARUSHA

IMG_0180  
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Maaskofu wa Kaisa Katoliki baada ya Ibada ya Jubilei ya miaka 50 ya  Kanisa Kuu  la jimbo la Arusha  iliyofanyika mjini Arusha  Desemba 30,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)IMG_0134

MTEMVU AIPIGA JEKI TIMU YA NETIBOLI YA TEMEKE QUEENS MASHINDANO KOMBE LA TAIFA 2013!!


 Mbunge wa Temeke, ambaye pia ni Mlezi wa timu ya netiboli ya Temeke Queens, Abbas Mtemvu, akimrejeshea Kombo la ubingwa Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Kibira lililokuwa linashikiliwa na mabingwa watetezi wa michuano ya Taifa Cup, Temeke Queens. Hafla hiyo ilifanyika wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo kwenye Uwanjawa Taifa Dar es Salaam.
 Mtemvu akimkabidhi kocha wa Temeke Queens, Amina Mussa fedha kwa ajili ya posho za wachezaji na viongozi wa timu hiyo inayoshiriki michuano hiyo.
Mtemvu akiwa na wachezaji wa timu ya Temeke Queens mabingwa watetezi wa mashindano hayo.
 
 Mwanaidi Ngubege wa Temeke Queens (kushoto) akijiandaa kufunga goli dhidi ya timu ya Mkoa wa Katavi.
 
Lillian Sylidion wa Temeke akidaka mpira
 
Mchezaji Sekela Dominick (kushoto) wa timu ya Temeke Queens akigombea mpira wa juu ya Rose Israel wa timu ya Mkoa wa Katavi katika mashindano ya kuwania Kombe la Taifa (Taifa Cup) siku ya ufunguzi wa michuano ya mchezo wa netiboli, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Temeke Queens ilishinda 58-27. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Benchi la wachezaji wa timu ya Mkoa wa Katavi
 
Kocha Amina Mussa wa Temeke akitoa mawaidha kwa wachezaji wakati wa mapumziko

TAMASHA LA KRISMAS JIJINI ARUSHA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI WAFANYA KWELI

Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba na kucheza jukwaani wakati wa tamasha la Krismas lililofanyika leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wa jiji hilo, ambapo waimbaji mbalimbali wamepanda jukwaani na kukonga nyoyo za mashabiki wao wakiwemo Bony Mwaitege, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Edson Mwasabwite, Tumaini Njole, The Voices, Victoria Singerls, mwimbaji wa kimataifa wa muziki wa injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti na wengine wengi. 3 
Watoto mbalimbali wakicheza na mwimbaji Rose Muhando jukwaani. 4 
Rose Muhando akiimbisha mashabiki wake. 5 
Mwimbaji Tumaini Njole akifanya vitu vyake jukwaani. 6 
Mwimbaji Wema kutoka Arusha akiimba jukwaani 7 
Upendo Kilahiro kushoto na Upendo Nkone wakiimba jukwaani kwa pamoja. 8 
Mwimbaji Bony Mwaitege akiruka jukwaani wakati alipokuwa akiimba. 10 
Baadhi ya mashabiki wa muziki wa injili waliojitokeza katika tamasha hilo. 13 
Askofu mkuu wa makanisa ya Calvary Asemblies of God , Dunstan Maboya akitoa neno katika tamasha la Krismas  kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo huku akiwa ameambatana na mchungaji mwenzake, kushoto ni Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion 15 
wimbaji wa kimataifa wa muziki wa injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti akifanya vitu vyake jukwaani katika tamasha la Krismas jijini Arusha leo. 
 18 
Kundi la The Voices likifanya vitu vyake jukwaani.

KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA YA GNSM CONTRACORS CO. LTD INAYOENDESHA NA GEOFREY MUNGAI YATOA MSAADA WA CHAKULA CHA MWAKA MPYA KWA YATIMA TOSAMAGANGA



Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai akiwa na  watoto  yatima  wa  kituo  cha Tosamaganga  wilaya ya Iringa jimbo la kalenga ambako alifika kukabidhi msaada wa chakula chenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 1.5 kwa ajili ya mwaka mpya kwa  watoto hao 

Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai  akiwa karibu na gari  lililobeba msaada  wa  chakula 
Baadhi ya watoto  yatima  wa  kituo cha Tosamaganga  Iringa  wakiwa  wamepumzika 
Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai  kulia akiwa amemshika mmoja kati ya  watoto yatima kituo cha Tosamaganga kushoto ni diwani wa  viti maalum tarafa ya Kalenga Shakra  Kiwanga  ambae  alikuwa ni  mwenyeji wa Mungai katika  kukabidhi msaada  wa chakula  kwa  yatima hao
Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai  akiwa na mmoja kati ya  watoto yatima  wa  kituo cha  Tosamaganga  Iringa leo 
Mlezi  wa  watoto  hayo Sisita Herena  Kihwele  kushoto  akiwa na  ugeni  uliofika  kituoni Tosamaganga kwa ajili ya  kushuhudia  tukio la Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai  kulia kukabidhi msaada wa chakula  xcha mwaka mpya kwa  watoto kituoni hapo 
Watoto  hao yatima   wakiimmba  mbele ya ugeni 
Mtoto  aliyefahamika kwa  jina la Nyota  akimsalimia Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai  ambae  alifika  kituoni hapo leo  kuwapa watoto hao chakula cha sikukuu ya mwaka  mpya ,mtoto  huyo alitelekezwa porini na mzazi  wake baada ya  kujifungua kabla ya  kituo  hicho kumuokota na kumtunza kituoni hapo 
Baadhi ya  yatima  kituo cha Tosamaganga 

Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai  kulia  akiwa na mlezi wa  kituo hicho sisita Herena  Kihwele 
Diwani  wa  viti maalum tarafa ya  Kalenga  Shakra  Kiwanga  kulia akimpongeza Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai  kulia kwa kusaidia  yatima
Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai kulia akikabidhi msaada  wa chakula na  vitu mbali mbali vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 1.5 kwa mlezi wa  kituo cha watoto  yatima cha  Tosamaganga Sisita  Herena Kihwele 
Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai  kulia  akiwa na wadau mbali mbali  walioongozana  kukabidhi misaada kwa yatima kituo cha Tosamaganga  leo 
Watoto  yatima  wa  kituo cha Tosamaganga  wakimpongeza Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai  kulia kwa kuwajali kwa  mwaka  mpya 

Diwani  wa  viti maalum tarafa ya  Kalenga  Shakra  Kiwanga  kushoto  akimpongeza Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai  kulia kwa kusaidia  yatima
 Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa ya  GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai   amekabidhi  msaada  wa chakula  cha mwaka  mpya chenye thamani  ya  zaidi ya Tsh milioni 1.5 kwa  kituo cha kulelea  watoto yatima  cha  Tosamaganga katika   jimbo la kalenga wilaya ya  Iringa vijijini .
Akikabidhi  msaada  huo  leo  Mungai  alisema  kuwa  amelazimika  kufika katika  kituo  hicho  ambacho  kinasimamiwa na masisita  wa kanisa la RC  kama  sehemu ya  mwendelezo wa kampuni  yake kuendelea  kuzungukia  vituo mbali mbali vya kulea yatima  na  kuwapa faraja  hasa katika msimu huu wa sikikuu.
Alisema  kuwa miongoni mwa vituo ambavyo amepata  kuvikumbuka katika msimu  huu wa sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya ni pamoja na  kituo cha Daily Bread Life (DBL) kilichopo jimbo la Iringa mjini na kituo hicho cha Tosamaganga  kilichopo jimbo la Kalenga huku lengo likiwa ni  kuwakumbuka  yatima  hao  na  kuihamasisha  jamii  kuelekeza nguvu  zao kwa  yatima kama  hao.
Bw  Mungai alisema  kuwa   takwimu  za maambukizi ya VVU katika  mkoa  wa Iringa zimeendelea  kuongezeka na iwapo  jamii haitajenga  utamaduni  wa kujali  yatima  vifo vya watoto  yatima ambao watakosa chakula baada ya kupoteza wazazi  wao kwa VVU pia  vitazidi  kuongezeka   hivyo lazima  misingi  ya  kuwajali  yatima ikaanzwa kuwekwa mapema  zaidi. 
” Hawa  watoto  iwapo  jitihada za vituo vya  kusaidia yatima visinge kuwa na moyo huo  leo yawezekana  baadhi yao  wasingekuwepo hapo  tungekuwa  tumewazika  ila kazi nzuri  ya  kujitolea  inayofanywa na vituo  vya yatima  ndio  imewafikisha hapa leo ….hivyo lazima  sisi kama  jamii  kuunganisha  nguvu zetu na vituo vya yatima”
Pia  alisema  kuwa  hata  viongozi  wa vyama vya siasa na serikali ni vema wakaweka utaratibu  wa  kufanya ziara  za mara kwa mara katika  vituo  vya yatima na  kujifunza mazingira ambayo  watoto hao  wanaishi ikiwa ni  pamoja na  kusaidia  kutatua changamoto  zinazovikabili vituo vya yatima mkoani Iringa .
Kwani  alisema kwa upande wake kama  mkandarasi ambae amekuwa akifanya kazi ya ujenzi wa barabara  mkoani Iringa na nje ya mkoa ameona  ni vema  katika fedha  kiasi ambazo anazipata  kuweka utaratibu wa kusaidia watoto yatima kama njia ya  kuwahamasisha pia wenzake  kujitoa kwa yatima  katika maeneo yao ama  kusaidia kuchangia maendeleo ya maeneo yao. 
Katika  hatua  nyingine Mungai aliwapongeza  walezi  wa  vituo vya  yatima katika mkoa  wa Iringa kuwa kutokana na mchango wao  wa kulea yatima hata  idadi ya yatima  na  watoto wa mitaani katika mji wa Iringa imeonekana  kupungua zaidi  
Kwa  upande  wake  diwani  wa viti  maalum tarafa  ya Kalenga Shakra  Kiwanga  akimpongeza  Mungai  alisema  kuwa ameonyesha upendo mkubwa kwa  yatima  hao na kuwataka makandarasi  wengine  kuiga mfano  huo. 
Kiwanga  ambae pia ni mmoja kati ya makandarasi wadogo mkoani Iringa alisema  kuwa alichofanya Mungai ni somo kwao pia katika kutoa sehemu ya makusanyo wanayoyapata  kupitia kazi mbali mbali. 
Awali mlezi  wa  kituo  hicho Herena Kihwele  alisema kuwa kituo hicho kina  watoto zaidi ya 100 na  kuwa kwa  sasa kituo kinakabiliwa na changamoto kubwa ya kushindwa  kuwalipia ada  sekondari   watoto zaidi ya 10  waliofaulu darasa la  saba ila kituo hakina uwezo wa  kuwasomesha . 
Iwapo umeguswa kuchangia  kituo hicho ada ama msaada  wowote  ule waweza  kuwasiliana na mlezi wa kituo hicho Sisita Herena Kihwele kwa simu  0768831477 pia  waweza  kutumia namba hiyo kwa kutuma M-PESA.