Muonekano wa basi la Penguin mara baada ya kupata ajali ya kugongana na land cruser.(habari/picha na Eddy Blog Team)
Toyota land cruser mara baada ya kugongana na basi la penguin.
Muonekano wa basi hilo.
Abiria walionusurika kwenya basi hilo wakitazama basi hilo mara baada ya ajali licha ya mvua kunyesha lakini walibaki kuduwaa.
Zaidi ya abiria 20 waliokuwa wakisafiri na basi la Penguin lenye namba za usajili T 947 BVQ
kutoka Njombe kuelekea wilayani Makete mkoani Njombe wamenusurika kifo
baada ya basi hilo kugongana na toyota landcruser pick up yenye namba za
usajili T 999 ARP
Ajali
hiyo imetokea jana Februari 22 majira ya saa tisa alasiri katika kijiji
cha Mang'oto wilayani hapo na kupelekea baadhi ya abiria hao kupata
majeraha madogo madogo na wengine wakitoka salama
Kwa
mujibu wa mwandishi wa eddy blog ambaye ni miongoni mwa walionusurika
kwenye ajali hiyo amesema imetokea kwenye kona iliyokuwa katika eneo
hilo na kushuhudia abiria hao wakitoka kwenye basi hilo wakiwa
hawaaamini kilichotokea kufuatia wengi wao kulala kwenye basi huku
safari ikiendelea kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha
Mmoja
wa manusura wa ajali hiyo ambaye alikuwa akienda kumuuguza baba yake
anayeendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Ikonda Consolatha
ambaye pia hakupenda jina lake liandikwe mtandaoni amesema alikuwa
amelela lakini ghalfa aliamka kutoka usingizini bada ya kusikia kishindo
kikubwa huku akisikia abiria wenzake wakipiga kelele
Kwa
mujibu wa maelezo ya abiria hao wamesema chanzo cha ajali hiyo ni
mwendo kasi wa magari yote mawili pamoja na mmoja wao kupita eneo ambalo
si lake (kuibia barabara) na hivyo kutokana na hayo ilikuwa ni vigumu
kukwepa ajali hiyo isitokee hata kama dereva aliishuhudia toka mbali
Dereva wa Toyota
landcuser iliyokuwa imetoka kupeleka mafuta kwenye minara ya simu
wilayani Makete ambaye amezungumza na mwandishi wetu eneo la tukio
amesema yeye alikuwa mwendo wa kawaida na alikuwa akipita upande wake
lakini alifatwa na basi hilo na kudai kuwa ukweli wa chanzo cha ajali
hiyo utafahamika pale askari wa usalama barabarani watakapofika eneo la
tukio na kufanya vipimo vyao
Abiria
wengi walitawanyika eneo hilo kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha huku
magari yanayotoka na kwenda Njombe na Makete yakishindwa kupita
kutokana na ajali hiyo kuziba barabara
Hadi
mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio majira ya saa 10 jioni askari
walikuwa hawajafika eneo la tukio, lakini alikutana na gari lao njiani
eneo la tandala likielekea eneo la tukio
Habari za uhakika baada ya polisi kufika na kufanya vipimo vyao utaipata hapa hapa kesho Jumatatu
No comments:
Post a Comment