Mwenyekiti wa Tancraft, Elihaika Mrema akizungumza na waandishi wa habari umuhimu wa jumuiya kubwa za wafanyabiashara na pamoja na serikali kuwaunga mkono wajasirimali wanawake nchini, Kushoto ni Esther Kasenga Msaidizi wa Katibu, Kulia Mweka hazina wa Chama cha Tancraft, Bi.Louise Judicate na Wapili kulia ni Katibu wa Tancraft, Bi. Vicky Shayo.
Na Damas Makangale
WAMILIKI Wote wa maeneo ya biashara nchini wameombwa kutoa nafasi ya maeneo ya biashara kwa wajasirimali wanawake ili kumkomboa mwanamke kutoka katika dimbwi la umaskini na utegemezi. MOblog inaripoti.
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wajasirimali wanawake jijini Dar es Salaam leo mchana, Mwenyekiti wa Tanzania Handcraft Association (Tancraft), Elihaika Mrema amesema kuwa wanawake wafanyabiashara wadogo wana matatizo na changamoto kadhaa mojawapo ni maeneo ya kuuzia bidhaa zao.
Pichani juu na chini ni Baadhi ya Wajasiriamali Wanawake wakifuatilia hotuba ya mwenyekiti wa TANCRAFT Bi. Elihaika Mrema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la Biashara la DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Kenya nchini.
“hata kama mjasirimali mwanamke ukimpa mtaji wa biashara na mafunzo changamoto kubwa ni kupata eneo la kuweza kuuza hiyo bidhaa yake aliyotengeneza kwa mikono yake mwenyewe,” amesema Mrema
Mwenyekiti, Mrema amesema kuwa chama cha Tancraft kilianzishwa mwaka 2006 chini ya usimamizi wa Board of External Trade (BET) na Small industrial Development Organization (SIDO) na kina wanachama zaidi ya 300 kutoka mikoa yote Tanzania.
Hii ni moja ya zawadi ya kikombe kwa Chama cha Wajasiriamali Wanawake Tanzania (TANCFRAFT) walichowahi kupata kwa kuonyesha bidhaa zenye ubora wa kimataifa.
Amesema kuwa Tancraft ni chama cha wajasirimali wanaotengeneza bidhaa kwa kutumia mali ghafi za kutoka nchini kama vile nguo za batik, vikapu, minyaa, vitu vya ufinyanzi,vinyago, shanga, bidhaa za ngozi, chakula na usindikaji wa aiana zote zikiwemo asali.
“malengo makuu ya chama yalikuwa ni pamoja na kuwatafutia wanachama wake soko la pamoja kwa ajili ya kuuzia bidhaa zao,” alilisisitiza Mrema
Amesema kwamba chama cha wanawake wa wajasirimali kimepata sehemu ya Dar es Salaam Free Market ambapo wajasirimali wakinamama watapata fursa ya kufanya biashara zao bila kulipa ushuru kama walivyokuwa katika maeneo ya Chang’ombe mikono.
Mkurugenzi Mtendaji wa J & L Enterprises, Bi. Louise Judicate Mushi, akitoa maelezo ya bidhaa zake za mchai chai za aina mbili black na green tea na mishumaa, amesema kwamba Green Tea ni mchai chai wa kijani kabisa ambao umesagwa kwa matumizi bora kwa afya ya binadamu
Amesema uzuri wa kinywaji hicho unaweza kunywa kikiwa cha moto au baridi, mchai chai ni dawa ya kushusha sukari, homa, presha, misuli na sumu za mwilini.
Mkurugenzi Mtendaji wa J & L Enterprises, Bi. Louise Judicate Mushi akimuonjesha aina ya chai mmoja wa waandishi wa habari kutoka kituo cha Channel Ten Bw. Salum Mkambala.
Mjasiriamali Fatuma Amour kutoka kampuni ya Famour Designer, akizungumzia ubunifu wake wa mavazi na ujasirimali utengenezaji wa nguo za wakinamama na wakinababa na Carpet za ngozi, viatu vya ngozi, vikapu na Batiki. Fatuma amesema alianza biashara miaka karibu 12 iliyopita katika biashara yake ya vitu vya asili vya kiafrika na changamoto kubwa kwake ni kujitangaza. Kushoto ni mwandishi wa habari kutoka Mwananchi Communications, Bi. Maimuna Kubegeya.
Maimuna Kubegeya akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na Mjasiriamali Fatuma Amour kwenye jengo la Biashara la DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Kenya nchini ambapo watakuwa hapo kwa muda wa mwaka mmoja.
Mwandishi wa kituo cha Televisheni cha ITV, Fatma Almasi, akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na Batiki. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Tancraft, Elihaika Mrema na wa tatu kulia ni Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Televisheni cha Channel Ten Bw. Salum Mkambala.
Baadhi ya Wajasiriamali wa DAR FREE MARKET wakionyesha bidhaa zao. Watanzania tuwaunge mkono wenzetu!
Baadhi ya Wajasiamali Wanawake Tanzania wakionyesha moja ya kazi za Uchoraji za Ujasiriamali kwa wageni waalikwa baada ya Chama cha Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TANCRATF) kuandaa mkutano na waandishi wa habari. Kulia ni Glory Matafu na kushoto ni Jacqueline Polycarp.
Picha hii inauzwa Shilingi Milioni 1.2 inapatikana kwenye Jengo la Biashara la DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Kenya nchini ambapo wajasiriamali hao wanafanya biashara zao hapo kwa muda wa mwaka mmoja.
Fatuma Amour kutoka kampuni ya Famour Designer akionyesha moja ya kazi za mikono yake.
RWANDA AND TANZANIA: TIGO PIONEERS WORLD’S FIRST MOBILE MONEY TRANSFER WITH CURRENCY CONVERSION WITH SERVICE BETWEEN RWANDA AND TANZANIA
The new service allows Tigo subscribers in Tanzania to send money from their Tigo Pesa accounts to Tigo Cash subscribers in Rwanda and vice versa
Tigo (http://www.tigo.co.tz), a subsidiary of the international telecommunications and media company Millicom (Stockholmsbörsen: MIC), a leader in thirteen markets across Africa and Latin America, today announced the launch of a pioneering cross-border Mobile Money remittance service between Tanzania and Rwanda.
The service was launched simultaneously in Kigali and Dar-es-Salaam in the presence of Rwandan High Commissioner in Tanzania Dr Ben Rugangazi, High Commissioner of Tanzania in Rwanda HE Francis Mwaipaja and Rwanda Finance Minister Honourable Claver who undertook the first mobile money transactions between the two countries.
The new service allows Tigo subscribers in Tanzania to send money from their Tigo Pesa accounts to Tigo Cash subscribers in Rwanda and vice versa. The system integrates currency conversion, whereby money is sent in either Tanzania Shillings or Rwandan Francs and delivered already converted into in the currency of the recipient’s country.
This, according to Tigo Tanzania General Manager Diego Gutierrez, is the first product of its kind in the world that allows dual currency international mobile wallet to mobile wallet transfers with currency conversion included.
Once the remittance is received, customers can use the funds to access all the services and benefits that Tigo Mobile Financial Services offer. These include airtime top ups, payments for water, electricity, TV and transportation, transfers to bank accounts, cash withdrawals at any Tigo agent across the country, and convenient transfers to other mobile money users.
To send money from Tigo Pesa (Tanzania) to Tigo Cash (Rwanda) users, customers should dial *150*90# while those in Rwanda remitting to Tanzania should dial *200*7#. This service can be used from any Tigo mobile phone. Customers in their respective countries will receive their money immediately in their routine currency.
To register for Tigo Pesa or Tigo Cash, customers can visit any agent in Tanzania or Rwanda respectively. Registration is free of charge; customers only need to present their ID.
According to Gutierrez, “This new product will save customers’ time and money. International senders currently have to go to a money changer to exchange Rwanda Francs to dollars and then bring those dollars to remittance companies to send. They can now send money directly from their phone.”
Mr Gutierrez continued: “We are delighted to give our customers the possibilities to make payments to fellow East Africans. Thanks to a stable and state-of-the-art technology, users in Rwanda are able to send money to their families, friends and to their business partners across the border alike.”
Tongai Maramba, the General Manager of Tigo Rwanda said: “We are pleased to offer Tigo Cash customers the ability to send and receive international transfers directly via their phones. It is an added convenience that they can receive directly as Rwandan Francs because the traditional money transfer companies mostly deliver only dollars. This product enables consumers not to worry about exchanging money.”
Murenzi Abdallah, a transporter working with a Kigali based transport and logistics company on the route Dar-es-Salaam-Kigali-Goma expressed: “I am excited about the opportunity to receive money directly on my mobile while in Tanzania. My life will be a lot easier in terms of making different tax payments at border posts and other needs on my long and difficult journeys.”
Millicom offers Mobile Financial Services in Tanzania, Ghana, Rwanda, DRC, Chad, Bolivia, Colombia, El Salvador, Guatemala, Honduras, Senegal and Paraguay and will extend its offering to more services and into more markets over time.
The new service will particularly benefit the businesses with cross-border trade, diaspora families, truck drivers, importers and exporters from both countries. Tanzania is Rwanda’s second most important trading partner. In 2013, Rwanda imports from Tanzania amounted to 80,883,702 US dollars while Tanzania received imports valued at 231,695,265 US dollars from Rwanda the same year.
KUMEKUCHA TAMASHA LA KIMATAIFA LA 33 LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO
Kikundi cha Sanaa cha TaSUBa wakifanya vitu jukwaani kwenye moja ya tamasha hilo 2013. jukwaaniMoja ya kikundi cha Sanaa cha Acrobat kikionyesha uwezo wao wa sanaaa hiyo 2013Moja ya mchezo wa igizo la hisia kali, lililofanywa na walimu wa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo 2013Moja ya vikundi vya kigeni kutoka Norway kikiwajibika jukwaani 2012
…………………………………………………………………………
…Kufanyika Septemba 22 hadi 28
…Vikundi zaidi ya 40 vinatarajiwa kutoa burudani
…Vikundi zaidi ya 40 vinatarajiwa kutoa burudani
….wadau na wadhamini milango ipo wazi sasa
Na Andrew Chale, Bagamoyo
TAMASHA la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambalo kwa mwaka huu (2014) litakuwa la 33, ambapo linatarajia kulindima kwa siku saba, kuanzia Septemba 22 hadi 28, kwenye viunga vya Chuo cha Sanaa Bagamoyo.
Tamasha hilo la 33, mwaka huu, lenye kauli mbiu, “Sanaa na Utamaduni katika kukuza Utalii”, limekuwa msaada mkubwa kwa wasanii na vikundi mbali mbali kujitangaza kitaifa na kimataifa pamoja na kutoa fursa za kibishara katika kipindi chote cha tamasha.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Abraham Bafadhil ‘Bura’, alieleza kuwa, tayari mipango na maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea katika kufikia malengo huku akiwaomba wadau kujitoakeza na kudhamini tamasha hilo.
“Milango ipo wazi hivyo, kwa wadhamini kujitokeza na kuchangamkia fursa hii hadimu, kwani tamasha hili ni kongwe katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Afrika kwa ujumla” alisema Bura.
Na kuongeza kuwa, tamasha hilo lenye mvuto wa kipekee ndani na nje ya Tanzania, limekuwa likipata umaarufu mkubwa kila mwaka kutokana na idadi kubwa ya watazamji wa ndani na wale wa kutoka Mataifa mbali mbali duniani.
Kwa upande wake, Katibu wa tamasha hilo, Benjamini Mahimbali alieleza kuwa, tamasha hilo limekuwa na mafanikio ikiwemo ongezeko kubwa la watazamaji na vikundi vinavyoomba kufanya maonyesho.
“Idadi ya watazamaji na imekuwa ikiongezeka kila mwaka, huku kwa mwaka jana tulikuwa na wastani wa watazamaji elfu nne mia saba kwa siku (4,700), ikiwemo wa rika zote.” Alisema Ben.
Na kuongeza kuwa, wanatarajia ongezeko hilo kuwa kubwa zaidi kutokana na maboresho na mipango mbali mbali inayotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Katika tamasha hilo maonyesho mbali mbali yanatarajiwa kuonyeshwa ikiwemo; Muziki wa aina tofauti, ngoma, maigizo, sarakasi, mazingaombwe na maonyesho kemkem ya sanaa na utamaduni wa Mtanzania na ya Mataifa mengine duniani.
Kwa upande wa fomu za kushiriki tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu wanatarajia kupokea vikundi zaidi ya 40, zinatarajiwa kutolewa kwenye ofisi za Chuo hicho pamoja na tovuti ya chuo (www.tasuba.ac.tz)
Au Kwa mawasiliano na maulizo juu ya ushiriki na udhamini waweza kufika Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) au kupitia namba;
+255(0) 715 472 745
+255(0) 655 840 405
+255(0) 754 310 425
+255(0) 712 683 408
Na Andrew Chale, Bagamoyo
TAMASHA la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambalo kwa mwaka huu (2014) litakuwa la 33, ambapo linatarajia kulindima kwa siku saba, kuanzia Septemba 22 hadi 28, kwenye viunga vya Chuo cha Sanaa Bagamoyo.
Tamasha hilo la 33, mwaka huu, lenye kauli mbiu, “Sanaa na Utamaduni katika kukuza Utalii”, limekuwa msaada mkubwa kwa wasanii na vikundi mbali mbali kujitangaza kitaifa na kimataifa pamoja na kutoa fursa za kibishara katika kipindi chote cha tamasha.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Abraham Bafadhil ‘Bura’, alieleza kuwa, tayari mipango na maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea katika kufikia malengo huku akiwaomba wadau kujitoakeza na kudhamini tamasha hilo.
“Milango ipo wazi hivyo, kwa wadhamini kujitokeza na kuchangamkia fursa hii hadimu, kwani tamasha hili ni kongwe katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Afrika kwa ujumla” alisema Bura.
Na kuongeza kuwa, tamasha hilo lenye mvuto wa kipekee ndani na nje ya Tanzania, limekuwa likipata umaarufu mkubwa kila mwaka kutokana na idadi kubwa ya watazamji wa ndani na wale wa kutoka Mataifa mbali mbali duniani.
Kwa upande wake, Katibu wa tamasha hilo, Benjamini Mahimbali alieleza kuwa, tamasha hilo limekuwa na mafanikio ikiwemo ongezeko kubwa la watazamaji na vikundi vinavyoomba kufanya maonyesho.
“Idadi ya watazamaji na imekuwa ikiongezeka kila mwaka, huku kwa mwaka jana tulikuwa na wastani wa watazamaji elfu nne mia saba kwa siku (4,700), ikiwemo wa rika zote.” Alisema Ben.
Na kuongeza kuwa, wanatarajia ongezeko hilo kuwa kubwa zaidi kutokana na maboresho na mipango mbali mbali inayotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Katika tamasha hilo maonyesho mbali mbali yanatarajiwa kuonyeshwa ikiwemo; Muziki wa aina tofauti, ngoma, maigizo, sarakasi, mazingaombwe na maonyesho kemkem ya sanaa na utamaduni wa Mtanzania na ya Mataifa mengine duniani.
Kwa upande wa fomu za kushiriki tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu wanatarajia kupokea vikundi zaidi ya 40, zinatarajiwa kutolewa kwenye ofisi za Chuo hicho pamoja na tovuti ya chuo (www.tasuba.ac.tz)
Au Kwa mawasiliano na maulizo juu ya ushiriki na udhamini waweza kufika Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) au kupitia namba;
+255(0) 715 472 745
+255(0) 655 840 405
+255(0) 754 310 425
+255(0) 712 683 408
VIONGOZI WAPYA WA IKULU SACCOS WAJITAMBULISHA KWA KATIBU MKUU KIONGOZI NA KUKABIDHI RIPOTI YA UTENDAJI.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Watatu kushoto) akiwa pamoja na Viongozi wa Ikulu SACCOS wakati walipokwenda kujitambulisha na kukabidhi ripoti ya utendaji ofisini kwake ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa SACCOS hiyo Bwana Theofrid Kikombele, Wapili kushoto ni Katibu wa SACCOS hiyo Bwana David Kivembele na kulia ni mshauri mkuu wa SACCOS hiyo Bwana Joseph Sanga.
(Picha na Freddy Maro.)
…………………………………………………………………………………………..
Na Freddy Maro. Ikulu.
Uongozi Mpya wa ikulu SACCOS leo umejitambulisha rasmi kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, ikulu jijini Dar es Salaam na kukabidhi ripoti ya utendaji ya SACCOS hiyo.
Waliojitambulkisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi ni pamoja na Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS Bwana Theofrid Kikombele,Makamu Mwenyekiti Bwana David Kivembele na Mshauri Mkuu Bwana Joseph Sanga.
Akizungumza mara baada ya kujitambulkisha, Mwenyekiti wa SACCOS hiyo Bwana Theofrid Kikombele alisema uongozi huo umepanga mikakati madhubuti ya kuiendesha SACCOS hiyo kwa uwazi na ufanisi zaidi ikizingatia kutenda kazi kwa weledi na kuwahamasisha wafanayakazi wengi zaidi kujiunga.
Mkakati mwingine, alisema Bwana Kikombele ni kwa SACCOS hiyo kuanzisha vitega uchumi mbalimbali kwa lengo la kupanua mtaji ili kuweza kuwahudumia vyema wanachama wa SACCOS hiyo kwa kuwawezesha kukopa zaidi kwaajili ya shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo.
Wakati wa mkutano huo kati ya Katibu Mkuu na Uongozi wa Saccos hiyo Viongozi hao walikabidhi ripoti ya utendaji wa SACCOS hiyo na walimuomba Katibu Mkuu Kiongozi kujiunga na SACCOS hiyo, ombi ambalo aliliafiki na kuahidi kutoa ushirikiano kuboresha SACOSS hiyo.
FAMILY DAY YA WAFANYAKAZI WA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA)
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki inayoundwa na mikoa mitano ya Dar es Salaam, Morogoro,Pwani, Lindi na Mtwara , Eng.Oscar Mwanjesa akiongea jambo kwa wafanyakazi wa TCRA walioambatana pamoja na familia zao katika siku ya Family Day iliyofanyika katika ufukwe wa hoteli ya Livingston Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki inayoundwa na mikoa mitano ya Dar es Salaam, Morogoro,Pwani, Lindi na Mtwara , Eng.Oscar Mwanjesa. Akisakata dansi na wafanyakazi na Katibu Mhitasi Halima Magonga (kulia)wakati wa kuadhimisha siku ya Familia(FamilyDay) iliyofanyika katika ufukwe wa Livingstone Wilayani Bagamoyo.Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakishindana kufukuza kuku wakati wa Family Day iliyofanyika katika ufukwe wa Livingston Bagamoyo ,Hafla hiyo iliwashirikisha wafanyakazi na familia zao.Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki inayoundwa na mikoa mitano ya Dar es Salaam, Morogoro,Pwani, Lindi na Mtwara , Eng.Oscar Mwanjesa akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa TCRA Juhudi Ngoza Kuku baada ya kuwashinda wenzake wakati wa Family Day iliyofanyika katika ufukwe wa hoteli ya Livingston Wilayani Bagamoyo .Anayeshudia ni Mhasibu wa Mamlaka hiyo Patrice Lumumba.Watoto wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki wakishindana kufukuza kuku wakati wa Family Day iliyofanyika katika ufukwe wa Hotel ya Livingston Wilayani Bagamoyo.Mhasibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki Patrice Lumumba akiongea jambo kwa wafanyakazi wenzake pamoja na familia zao wakati wa siku ya Family Day iliyofanyika katika Hotel ya Livingstoni Wilayani Bagamoyo jana.Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki inayoundwa na mikoa mitano ya Dar es Salaam, Morogoro,Pwani, Lindi na Mtwara , Eng.Oscar Mwanjesa akimkabidhi Kuku David Mapunda baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa kukimbia na gunia wakati wa siku ya Family Day iliyofanyika katika ufukwe wa hoteli ya Livingston Wilayani Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment