on FEBRUARY 26, 2014 in JAMII
Mwenyekiti wa kamati ya mashinda ya Tunzo ya Ushairi nchini Tanzania Ibrahim Seushi akizungumza wana wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Tuzo hizo mapema hivi karibuni. Tuzo hizo zitaitwa Ebrahim Hussein ikiwa ni kumuenzi nguri na mkongwe huyo wa mashairi hapa nchini.Jaji Kiongozi wa Tuzo za Ebrahim Hussein Profesa Mugabyo Mlinzi Mulokozi akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa tuzo hizo mapema hivi karibuni.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Hajaty Shani Kitoga akiimba shairi la Wakati Ukuta ambaole ni moja ya kazi za Profesa Ebrahim Hussein wakati wa uzinduzi wa tuzo za mashairi zilizoanzishwa mapema hivi karibuni.Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Publisher Bw. Walter Bgoya akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa tuzo za mtunzi wa mashairi ambapo kampuni hiyo ndiyo muendeshajio wa mashindano hayo.
Profesa Ebrahim Hussein (katika) akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa tuzo za mashairi zilizopewa jina lake ikiwa ni kuenzi mchango wake katika tasnia hiyo mapema hivi karibuni.
Picha zote na Frank Shija – WHVUM
No comments:
Post a Comment