TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Friday, April 8, 2016
IDARA YA UHANDISI YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD MWENYEJI MKUTANO WA AE&M ABU DHABI.
IDARA ya Uhandisi ya Shirika la Ndege la Etihad itakuwa mwenyeji na mdhamini wa mkutano ujao wa uhandisi na ukarabati wa ndege wa mtandao wa MRO uliopo Mashariki ya Kati, Mkutano huo unaotazamiwa kufanyika mjini Abu Dhabi mwezi Aprili 26-27, 2016. Mjadala mkuu utakuwa juu ya ukuaji wa mtandao wa MRO wenye historia isiyopungua miaka 20, wenye wadau katika sekta za – Ndege, MROs, OEMS na Wauzaji – kuwaleta pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya kimasoko.
Mada mbalimbali kama maendeleo katika masoko ya usafiri wa anga huko mashariki ya Kati, sekta ya utabiri wa masoko ya MRO pamoja na jinsi mashirika ya ndege yanajenga mahusiano na wadau wengine wa MRO.
Miongoni mwa wazungumzaji sekta inayoongoza ni Jeff Wilkinson, Makamu wa Rais shirika la ndege la Etihad kwa upande wa Ufundi alisema: " Ni furaha yetu kuwa mwenyeji wa wajumbe wa uhandisi na ukarabati wa ndege hapa mjini Abu Dhabi – kitovu kipya cha masuala ya teknolojia ya anga na usafiri kanda ya mashariki ya Kati”
Ikiwa ni mwaka mmoja tangu kufanikisha maonyesho mengine kama haya, idara ya uhandisi ya Shirika la ndege la Etihad kwa mara nyingine tena itatoa ziara ya kituo chake kwa wajumbe baada ya kuhitimisha mkutano huo, hivyo kuwapa fursa wajumbe kukutana na timu ya uongozi ya idara ya uhandisi pamoja na kutoa fursa ya kutembelea karakana na warsha mbalimbali ndani ya kituo .
"Tumeandaa ziara ya kituo cha kisasa kabisa cha idara ya uhandisi ya shirika la ndege la Etihad, karakana zake pamoja na warsha zitakazo fanyika katika kituo hicho kikubwa kuliko vyote katika mtandao wa MRO kanda ya mashariki ya kati. Hii ni pamoja na karakana sita (6) zenye uwezo wakuhifadhi hadi ndege kubwa tatu (3) aina ya A380 kwa wakati mmoja. "
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment