TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Friday, April 8, 2016
JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LIMEFANIKIWA KUWAKAMATA WATU 63 WANAOZANIWA KUWA MAJAMBAZI.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro kizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limekamata majambazi sitini na tatu (63) wa matukio ya unyang'anyi wa kutumia silaha katika oparesheni maalum iliyoendeshwa kwa wiki nzima na Jumla ya silaha sita, (6) ikiwemo SMG 1, SHORTGUN PUMP ACTION 3 na RIFLE 2.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro akionesha silaha huizo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimsiliza Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata watu 63 wanaozaniwa kuwa majambazi wa kutumia silaha katika operesheni endelevu ya kuwasaka majambazi wanaofanya matukio mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi kanda maalumu Simon Sirro aamesema, miongoni mwa majambazi waliokamatwa ni Ibrahim Juma(31) mkazi wa Kiwalani Kigilagila, Samweli Mbonea (40) Fundi gereji Mkazi wa Kiwalani pamoja na Anthony Kanywenywe (60) Mwindaji na mkazi wa Kiwalani.
Amesema majambazi hao walikutwa na taa kubwa nne za magari, pawa windo moja na nati za magari na watuhumiwa sita kati ya waliokamatwa wamekiri kushiriki katika matukio ya unyanganyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali likiwemo la Riki Hill Hotel katikati ya jiji na Lake oil Buguruni.
Katika tukio jingine kikosi maalumu cha kupambana na majambazi kimefanikiwa kukamata silaha sita aina ya SMG moja ,Short gun pump action tatu na Rifle mbili katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
amesema silaha aina ya SMG iliyokatwa kitako ilipatikana baada ya askari kuwafyatulia risasi majambazi hao waliokuwa eneo la vingunguti ndipo walipoitupa silaha hiyo ikiwa kwenye mfuko mweusi wa plastiki na wao kukimbia katika bonde la Mto Msimbazi.
“Tunaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao na upelelezi unaendelea ili kubaini mmiliki halali wa silaha hiyo hatupotayari kuendelea kuona maovu yakiendelea kufanya jeshi lipo imara na tutapambana nao,” alisema Sirro.
Ameongeza kuwa jeshi hilo pia lilifanikiwa kukamata silaha Rifle mbili katika eneo la Masaki ambazo zilikuwa zimeficha na kufunikwa kwa taulo zikiwa na maandishi ya Collessium Fitness Club moja ikiwa na namba A 6777013 iliyosajiliwa nchini kwa namba TZCAR 58596, na nyingine ikiwa na namba L 691848176 iliyosajiliwa kwa namba TZCAR 75062.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi Kanda maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata jumla ya risasi 15 za silaha ndogo aina ya bastola zikiwa kwenye magazine, Risasi hizo alikutwa nazo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mamboleo Willium (41) Mfanyabiashara mkazi wa Mikocheni.
Katika mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kuwa na risasi hizo kinyume na sheria na kushindwa kueleza mahali alipozipata, mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na uchunguzi unaendelea kufanyika
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment