Mhe mhagama alitoa agizo hilo wakati wa mkutano wake na Kamati hiyo uliofanyika
Aprili 1, 2016 katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es
Salaam kwa lengo la kuangalia namna bora ya kukabiliana na changamoto
zinazoikabili sekta ya usafirishaji.
Katika kikao cha Kamati hiyo inayoundwa na Wamiliki wa malori, daladala,
mabasi, vyama vya abiria, Idara ya Usafirishaji, Shirika la viwango, Wakala wa
Vipimo, Jeshi la polisi, watu wa usalama barabarani, TANROADS na Umoja wa
Wasafirishaji Abiria Dar es Salaam (UWADAR) mhe. Mhagama alisisitiza kuwa
Serikali haitawafumbia macho wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao hawazingatii
mikataba ya kazi kwa madereva.
“Ninaagiza mikataba ya maderva iangaliwe upya na ikiwezekana yaainishwe majina
ya wamiliki wa magari wanaokiuka haki na sheria zilizopo za kuwapa madereva
mikataba na stahiki zao ili sheria iweze kuchukua mkondo wake,”alisema Mhagama
Kutokana na changamoto mbalimbali za madereva zilizobainishwa
wakati wa mkutano huo Mhe.Waziri aliwataka wajumbe wote kuangalia namna
nzuri ya kukabili changamoto hizo ili kuhakikisha malalamiko ya madeva yanaisha
na kufanya sekta hiyo kuwa na amani na
utulivu.
“Lengo kuu ni kuona sekta ya usafirishaji inakuwa salama na yenye amani kwani
ikumbukwe sekta hii ni nyeti, inabeba roho za watu wengi kila iitwapo leo kwa
kuwasafirisha mikoani na nje ya mikoa.” Alisisitiza Mhagama.
Nae mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Leonard Chamuliho aliomba kamati kuyafikia
maazimio ya muhimu yaliyojadiliwa na huku akisisitiza agizo la mhe. Mhagama la
kuwataka wamiliki na waajiri wote kuzifuata na kuzitekeleza sheria za mikataba
kwa waajiriwa wote.
No comments:
Post a Comment