Akizungumzia tamasha hilo, mratibu wake, Natasha Stambuli alisema
kuwa wabunifu wa ndani wengi wamejitokesha kushiriki tamasha hilo.
Alisema kuwa kutokana na mwamko huo tamasha hilo limewakutanisha wajasiriamali hao pamoja na wanunuzi kwa maana ya wateja ili wawaunge mkono.Alisema kuwa bidhaa kama vile nguo, viatu vidani na bidha nyingine vimeuzwa katika tamasha hilo.Alisema “kwa awamu hii ambayo ni ya saba tukiwa bado na mdhamini wetu kinywaji cha Smirnoff watu wengi wamejitokeza na kupata huduma kadhaa ambapo wamekuwa wakinunua bidhaa huku wakipata burudani ya muziki”.Kwa upande wake Meneja wa vinywaji vikali kutokea, Serengeti Breweries Limited (SBL) Shomari Shija alisema kuwa kampuni hiyo kupitia kinywaji chake cha Smirnoff imeamua kudhamini tamasha hilo kwa kuwa inatambua mchango wa ujasiriamali katika maendeoleo.Mmoja kati ya wajasiliamali walioshiriki katika tamasha hilo, Sackry Papillon wa huduma ya mwili, The Ryb Spa iliyopo Kijitonyama alisema kuwa tanmasha hilo limemkutanisha na wadau mbalimbali hasa vijana wanaopenda huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment