TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Friday, April 8, 2016
TUNAWEZA KUIMALIZA MALARIA - RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE
Na Mwandishi Maalum, New York
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amesema, anaimani kubwa kwamba ushirikiano uliopo baina ya serikali mbalimbali barani Afrika, mashirika ya kimataifa, makampuni binafsi na kila mtu katika nafasi yake, hapana shaka ugonjwa wa malaria unaweza kumalizwa kabisa.
Mhe. Kikwete ameonyesha matumaini hayo jana( alhamisi) wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa jitihada za kuutokomeza ugonjwa wa malaria ( Malaria No More) zilizoanzishwa na Bw. Ray Chambers akishirikiana na Bw. Peter Chernin.
Katika hafla hiyo na ambayo mshereheshaji alikuwa Bw. Wolf Blitzer mtangazaji maarufu wa Televisheni ya Kimataifa ya CNN kupitia kipindi chake cha situation Room, Rais mstaafu alitunukiwa tuzo ijulikanayo kama White House Summit Awards ikiwa ni kutambua uongozi wake, kujitoa kwake na kubwa zaidi kusimamia uanzishwaji wa muungano wa viongozi wa Afrika dhidi ya Malaria ( ALMA) muungano ambao hadi sasa una viongozi 49.
Wengine waliotunukiwa tuzo hiyo ni Bw. Ray Chambers na Sumitomo Chemical.
Akijibu swali la nini anadhani kumechangia katika kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria. Rais mstaafu amesema, zipo sababu kadhaa, lakini kubwa ni utashi wa kisiasa wa kusimamia na kuongoza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Akawaeleza wageni zaidi ya 250 walioalikwa wakiwa ni wawakilishi wa makapuni na mashirika mbalimbali yanayochongia juhudi za kuukabili ugonjwa wa malaria. Kwamba, Upatikanaji na usambazani wa dawa sahihi za kutibu ugonjwa wa malaria, utengenezaji, usambazaji na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu na unyunyiziaji wa dawa za kuuwa mazalia ya mbu ni mambo ya msingi ambayo yamechangia katika kupunguza vifi vya watoto chini ya miaka mitano.
“mchanganyiko wa mambo hayo matatu umesaidia sana kupunguza idadi ya watoto wanaofariki kwa malaria, lakini pia matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu ambapo zaidi ya vyandarua milioni 24.2 vimesambazwa, kumechangia wanafunzi kuendelea na masomo yao bila kukatishwa mara kwa mara sababu ya malaria, halikadhalia nguvu kazi imeimarika”. akasisitiza Rais Kikwete na kushangiliwa na wageni waalikwa.
Mwanzilishi wa Malaria no More, Bw Peter Chernin akimkabidhi Mhe. Rais Mstaafu, Kikwete tuzo ya White House Summit Awards ikiwa ni kutambua na kuthamin mchango na uongozi wake katika jitihada za kuukabili ugonjwa wa malaria, wengine waliopewa tuzo hiyo ni Bw. Ray Chambers na Kampuni ya Sumitomo Chemical ambayo imejenga kiwanda cha vyandarua cha A-Z Arusha Tanzania.
Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akielezea juhudi zilizofanywa na serikali ya Tanzania katika kuukabili ugonjwa wa malaria, ilikuwa wakati wa hafla ya miaka 10 ya Malaria no More iliyofayika jana alhamis New York Marekani, Mhe. Kikwete amealikwa katika hafla hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika pamoja na mengin kuwahamasisha viongozi wa Afrika kuongeza juhudi za kisera, kimkakati na bajeti hali ambayo imechangia sana katika kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano. pamoja naye ni Bw. Peter Chernin, Bw. Ray Chambers na mwezeshaji, Bw. Wolft Blitzer wa CNN.
Mhe. Rais Mstaafu katika mkutano na Bodi mpya ya Malaria no More muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya miaka 10 ya Malaria No More.
Sehemu ya Wageni zaidi ya 250 kutoka masharika na makampuni mbalimbali ambako ni sehemu ya wadau wa kubwa wanaochangia juhudi za kutokomeza na kudhibiti ugonjwa wa malaria.
Burudani pia ilikuwapo.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment