TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, April 5, 2016

TAARIFA KWA UMMA MAKUSANYO MWEZI MACHI 2016

ISO 9001:2008 CERTIFIED

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya na kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato mwezi Machi 2016 kwa asilimia 101.
Lengo hilo limevukwa baada ya TRA kukusanya shilingi trilioni 1.31 kati ya lengo la shilingi trilioni 1.30.


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata amesema ongezeko la makusanyo linatokana na jitihada zinazofanyawa na TRA katika kuongeza kasi ya usimamizi wa ufuatiliaji na ukadiriaji wa kodi kwa usahihi.
“Tumejitahidi kudhibiti biashara za magendo katika maeneo ya Ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi, mipakani na maziwa yote, Alisema Kamishna Mkuu.

Amesema hadi kufikia Machi 2016, tayari TRA imekusanya shilingi Trilioni 9.89 sawa na asilimia 99 ya lengo la makusanyo ya shilingi trilioni 9.99 mwaka wa fedha 2015/2016.
Bw. Alphayo amewasisitiza wafanyabiashara ambao hawajasajili biashara zao kufanya hivyo mara moja kupitia ofisi za TRA zilizoko katika maeneo ya biashara zao na kwa wale wanaoshiriki vitendo vya uingizaji bidhaa za magendo nchini amemewata kuacha mara moja kwani vinaipotezea serikali mapato.
“Wakikamatwa katika msako unaoendelea watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutaifisha bidhaa hizo, kutozwa faini pamoja na kifungo”, amesisitiza.

Kwa Wafanyabiashara ambao wanastahili kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) Kamishna Mkuu amewataka kujisajili katika ofisi yoyote ya TRA na wahakikishe wanataarifa muhimu ikiwemo anuani inayotambulika na namba simu zinazofanya kazi.
“Natoa wito kwa wafanyabiashara wote waliosajiliwa na VAT lakini hawatumii mashine za kielektroniki za kodi (EFDs) watumie mashine hizo kwa mujibu wa sheria. Wakibainika hawazitumii watachukuliwa hatua za kisheria kwani zoezi la ukaguzi wa biashara linaendelea mtaa kwa mtaa katika mikoa yote. 

Aidha wananchi wanakumbushwa kudai risiti za kodi kwa thamani halisi ya manunuzi kila wanapofanya manunuzi au kupata huduma”, alisema Kamishna Mkuu na kuongeza kuwa wananchi wema na wazalendo wenye taarifa za ukwepaji wa kodi wazifikishe TRA kwa usiri. TRA inawaahidi donge nono ikiwa ni pamoja na kutunza siri za taarifa hizo. Vilevile wanapoadaiwa rushwa au kutendewa isivyo wasisite kutoa taarifa mara moja.
Imetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA- Makao makuu

No comments:

Post a Comment