TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, January 12, 2014

RAIS DK. SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia wananchi wa Zanzibar wakati akiingia kwenye uwanja wa Amani  na gari la wazi kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zamzibar yaliyofanyika leo yakihudhuriwa na vongozi mbalimbali wa Tanzania na Baadhi kutoka nchi za Afrka Mashariki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa Zanzibar wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Amani kwenye kilele cha sikukuu ya miaka ya 50 ya Mapinduzi.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Sehemu ya Umati uliofurika wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua vikosi vya gwaride kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Amani.
Maandamano mbali mbali kutoka kwenye Mikoa na Taasisi za serikali na zisizo za Serikali yalipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine.
Wakina mama hawakuwa nyuma kwenye maandamano ya mika 50 ya Mapinduzi kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.
Kikosi cha Mbwa kikiingia uwanjani tayari kuonyesha umati wa watu jinsi Mbwa wenye mafunzo wanavyoweza kufanya kazi zao vizuri.
Askari wakionyesha jinsi askari waliokuwa chini ya mkoloni walivyokuwa wanafanya mambo yao ikiwa kila amri kutoka kwa lugha ya kiingereza.
Kikosi cha Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana na maadui bila kutumia silaha za moto kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Kikosi cha Kifaru kinaonyesha kifaru cha kivita.
Vijana wa Halaiki wakionyesha ushiriki wao kwenye miaka 50 ya Mapinduzi “Mapinduzi Daima”.
Kikosi cha Mapinduzi kilichopambana na kuleta Mapinduzi ya Zanzibar kikipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,kwenye kikosi hicho amebaki mwana mama mmoja anayefahamika kwa jina la Fatma Abdalla Mussa watatu kutoka kulia.
Sehemu ya Jukwaa kuu la uwanja wa Amani likiwa limefurika wakati wa sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi.
Picha na Adam Mzee

MGIMWA;;- MIMI SI MBUNGE MZIGO NIMETEKELEZA AHADI KUBWA ZOTE JIMBONI NITAGOMBEA TENA

Mbunge Mgimwa

 
MBUNGE  wa  jimbo la Mufindi Kaskazin Mahmoud  Mgimwa  amesema  kuwa  kuwa  kati  ya  wabunge wachapakazi  yeye ni miongoni na  kuwa  yeye si mbunge mzigo kwa  jimbo  hilo kwani amefanikiwa  kutimiza ahadi  zake kubwa zote  alizopata  kuwaahidi  wapiga kura  wake.
Akizungumza katika mahojiano maalum  juu  ya ahadi  alizopata  kuwaahidi  wapiga kura  wake  wakati wa  wa kampeni  za uchaguzi  mkuu  mwaka 2010 ,Mgimwa  alisema  kuwa mbali ya jitihada  kubwa ambazo amezifanya  kama  mbunge  katika  kutekeleza ahadi mbali mbali  ila bado anampongeza  zaidi Rais Dr  Jakaya Kikwete ambae  alipata  kuahidi  kuweka lami katika mji wa Mafinga na tayari  lami hiyo  imewekwa na kuzidi  kumwongezea heshima kubwa yeye kama  mbunge na Chama cha mapinduzi (CCM)
Alisema  kuwa miongoni mwa ahadi ambazo  alipata  kuzitoa kwa  wapiga  kura  wake  wakati wa kampeni ni pamoja na uboreshaji wa  miundo mbinu kwa maana ya  barabara ya Mafinga – Madibila ambayo tayari  imefanyiwa  matengenezo  na ipo  katika  orodha ya barabara  zitakazowekwa lami,pamoja na ahadi  za elimu ,afya ,maji  ambazo zote  zimefanyiwa kazi.
Hivyo  alisema  iwapo asingefanikiwa  kutekeleza ahadi  zake ambazo aliwapa  wapiga kura  wake  asingekuwa na haja ya  kuendelea  kuutaka  ubunge  wa  jimbo hilo ila kwa  kuwa sehemu kubwa ya ahadi amepata  kutekeleza ni  wazi  kuwa  yeye  si mbunge mzigo   hivyo bado  ana uwezo  wa  kuendelea  kuwaongoza  wanananchi  wa  jimbo  hilo.
Mbunge  Mgimwa  alisema  kuwa  wananchi  wa  jimbo  hilo  wameendelea  kuwa na ushirikiano mzuri  katika  kujituma  kufanya kazi na  kuwa  imani  ambayo wananchi hao  wameendelea  kuionyesha  kwake imezidi  kumpa nguvu  zaidi  ya  kuwatumikia  na kuwaomba  kuendelea kujituma zaidi.

SHULE MAARUFU YA ETON UINGEREZA KUENDELEZA MICHEZO TANZANIA

Afisa Balozi -Minister Counsellor- Amos Msanjila akizungumza na Freddy Macha na Urban Pulse
Afisa Balozi -Minister Counsellor- Amos Msanjila akizungumza na Freddy Macha na Urban Pulse Balozi na wageni wote. Kwanza kabisa kulia ni Mkurugenzi wa Biashara Ubalozini, Yusuf Kashangwa- pic by Urban Pulse
Balozi na wageni wote. Kwanza kabisa kulia ni Mkurugenzi wa Biashara Ubalozini, Yusuf Kashangwa- pic by Urban Pulse Balozi Peter Kallaghe
Balozi Peter Kallaghe akizungumza  Bw John Collenette wa ACE Africa
Bw John Collenette wa ACE Africa Kocha Glen Pierce akiwa na wanafunzi, Nicolas Zafiriou, Ali Lyon na Tom Pearson
Kocha Glen Pierce akiwa na wanafunzi, Nicolas Zafiriou, Ali Lyon na Tom Pearson Kocha wa Eton, Glen Pierce akizungumza- Pic by Urban Pulse
Kocha wa Eton, Glen Pierce akizungumza- Pic by Urban Pulse Mkurugenzi wa Safari Hub, Dilip Navapurkar akizungumzaMkurugenzi wa Safari Hub, Dilip Navapurkar akizungumza
………………………………………………………….
Imeandikwa na Freddy Macha 
Mradi wa majaribio ya mwezi mmoja ulioandaliwa na Waingereza kuendeleza shule sita wilaya za Arusha na Moshi unatazamiwa kuanza wiki hii, ilitangazwa London, mwishoni mwa juma.
Mradi huu unaosimamiwa na kampuni ya kitalii, Safari Hub na Chuo cha Eton wakisaidiana na Ubalozi wa Tanzania, Uingereza, unatuma Mkuu wa Mafunzo ya Michezo Eton, Bwana Glen Pierce na wanafunzi watatu waliomaliza kidato cha sita wanaotarajia kuingia vyuo vikuu baadaye mwakani.
Nchini shughuli hii itasaidiwa na ushirikiano wa chuo cha michezo Arusha (Future Stars Academy) na shirika la ufadhili linalopigana kuondoa umaskini, (ACE Africa).
Akiongea katika tafrija ndogo iliyofanywa Ubalozini, London kuuaga msafara , Mkurugenzi Mkuu wa Safari Hub, bwana Dilip Navapurkar alisema iko haja ya kujenga ujuzi toka utotoni ili “kuhakikisha timu ya taifa ya Tanzania inafanya vizuri katika michuano ya Kombe la Afrika na Dunia na kufikia kiwango cha mafanikio tunayoyaona nchi nyingine mathalan Nigeria, Ghana, Afrika Kusini na Ivort Coast.”
Mwalimu Pierce mwenye uzoefu wa Miaka 27 chuo cha Eton aliwafundisha pia wajukuu wa Malkia Uingereza, William na Harry.  Wanafunzi atakaoongozana nao ni  Tom Pearson, 18 ( ulinzi) Nicholas Zafiriou, 18 (kiungo) na Ali Lyon, 19 (mshambuliaji ). Wamechaguliwa kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ukiwemo mpira waliocheza timu ya shule ya Eton.
Eton ilianzishwa karne ya 15 na Mfalme Henry wa 6 na ni moja ya shule bora sana duniani. Mawaziri Wakuu 19 wa Uingereza (akiwemo Winston Churchill, Tony Blair, David Cameron na Meya wa Jiji la London, Boris Johnson) walisoma hapa. Wabunge, mawaziri, waandishi maarufu (George Orwell na Ian Fleming mtunzi wa visa vya James Bond) na watoto wa wafalme mbalimbali duniani vile vile wamesoma Eton.                                                                                                                                                                                                                                                                                          Tafrija ya kuwaaga ilifanywa na Balozi Peter Kallaghe na Afisa Balozi, Amos Msanjila aliyewakaribisha  Tanzania. Mbali na kutoa mafunzo ya michezo wageni wanatazamiwa kukutana na wanahabari Jumanne, kutembelea mbuga za wanyama, Zanzibar na kupanda mlima Meru, Arusha.
Lengo la mradi huu ni safari au mradi mfupi na hatimaye kuendeleza mahusiano kati ya wanafunzi wa Tanzania na Eton.  Iko siku “timu ya mpira ya Eton itafanya ziara Tanzania na hatimaye Watanzania pia kuitembelea Eton,” Bwana Navapurkar alisema.                   
Akihimiza umuhimu wa safari hii, Balozi Kallaghe aliwaambia wageni kwamba Watanzania wanapenda sana soka na kuwaahidi wageni kuwa watafaidi uzuri wa nchi  watakapofika kama sehemu ya mafanikio ya kibiashara siku za mbeleni na kufurahia michezo Tanzania.
Akijibu maswali ya wanahabari, Bwana Navapurkar alisema gharama za safari na vifaa vimetokana na michango ya watu binafsi na shule zinazopakana na Eton ambazo zimefikia shilingi milioni 61 na nusu.
Mbali na mafunzo ya mpira wanafunzi Arusha na Moshi watapewa vifaa na kufundishwa maana ya nidhamu, elimu na michezo, aliongeza kocha Glen Pierce. “Watoto watakaopewa fursa hiyo ni wale tu watakaohudhuria shule,” alisisitiza.
Akisifia tabia  ya Watanzania, Mkurugenzi wa  Safari Hub, yenye makao Tanzania, Bwana Navapurkar, alisema Tanzania imechaguliwa shauri ni nchi yenye amani, demokrasia na utulivu wa kisiasa, ukilinganisha na nchi nyingine za Kiafrika. “Tanzania ni kito cha maendeleo ya Afrika.” Alisema.

DK.SHEIN AKUTANA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIJI NA VIJIJINI WA CHINA.

TA1A9506
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijijini Nchini China Bw,Jiang Weixin,alipofika Ikulu ya Migombani,Waziri huyo yupo nchini kushiriki sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] TA1A9479 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijijini Nchini China Bw,Jiang Weixin,alipofika Ikulu ya Migombani,Waziri huyo yupo nchini kushiriki sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA TFF

MALINZI AZINDUA KAMPENI YA ISHI HURU
tff_LOGO1
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amezindua programu ya kutoa elimu ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana iitwayo Ishi Huru.
Programu hiyo iliyozimduliwa jana (Januari 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam iko chini ya taasisi ya Africa Inside Out inayoongozwa na Rebecca Young wakati washirika (partners) ni TFF na kampuni ya Rhino Resources ya Marekani.
Rais Malinzi amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamekuwa yakiongezeka, hivyo kuwa kikwazo kwa maendeleo ya vijana ambapo ameipongeza Africa Inside Out kwa programu hiyo kwa vile itazuia vijana wengi kujiingiza katika matumizi ya dawa hizo.
“Moja athari kubwa za matumizi ya dawa za kulevya ni kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutokana na kuchangia sindano za kujidunga dawa hizo.
“TFF tutatoa ushirikiano wa kutosha katika programu hii. Lakini pia tutaingiza Ishi Huru katika programu zetu za mpira wa miguu kwa vijana. Tutahamasisha jamii katika kupambana na dawa za kulevya,” amesema.
Katika uzinduzi huo, pia Rais Malinzi alizundua semina ya waelimishaji na kuwaeleza kuwa wamepata fursa hiyo kwa vile ni vijana wanaojituma, hivyo watafikisha vizuri ujumbe wa Ishi Huru katika shule na vituo vya vijana nchini.
CAPTION: Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akizungumza kwenye uzinduzi wa programu ya Ishi Huru jijini Dar es Salaam.
RAMBIRAMBI MSIBA WA MTANGAZAJI SULTAN SIKILO
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mtangazaji wa michezo wa Radio Abood, Sultan Sikilo kilichotokea jana alfajiri (Januari 11 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Sikilo ambaye pia aliwahi kufanyia kazi Radio Times na Radio Kheri na hadi umauti unamkuta alikuwa Mweka Hazina Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo Tanzania (TASWA) amezikwa jana jioni katika makaburi ya Kibada, Kigamboni.
Msiba huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Sikilo alifanya kazi na TFF kwa kuripoti shughuli zetu nyingi za mpira wa miguu, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Sikilo, Radio Abood na TASWA na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Pia TFF imetoa ubani wa sh. 100,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina

Dk.SHEIN AZUGUMZA NA RAIS WA VISIWA VYA COMORO.

TA1A9402
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Comoro Ikililou Dhoinine,alipofika Ikulu ya Migombani Mjini Unguja leo,Rais  wa Comoro alifika nchini kushiriki katika sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar ambazo kilele chake kitafanyika katika Uwanja wa Amaan.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] TA1A9410
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Rais wa Comoro Ikililou Dhoinine,alipofika Ikulu ya Migombani Mjini Unguja leo,Rais  wa Comoro alifika nchini   kushiriki katika sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar ambazo kilele chake kitafanyika katika Uwanja wa Amaan.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
TA1A9435
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Rais wa Comoro Ikililou Dhoinine,alipofika Ikulu ya Migombani Mjini Unguja leo,Rais  wa Comoro alifika nchini   kushiriki katika sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar ambazo kilele chake kitafanyika katika Uwanja wa Amaan.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
TA1A9462 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na  Rais wa Comoro Ikililou Dhoinine,baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu ya Migombani Mjini Unguja leo,Rais  wa Comoro alifika nchini  kushiriki katika sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar ambazo kilele chake kitafanyika katika Uwanja wa Amaan.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA ASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA WA KANISA LA KKKT SUMBAWANGA NA KUUNDA DAYOSISI MPYA YA ZIWA TANGANYIKA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa 8 wa kanisa la kiinjili na kilutheri Tanzania KKKT la mjini Sumbawanga ambapo utafanyika uchaguzi Mkuu wa Kanisa hilo na kuzaa Dayosisi mpya ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika. Katika hotuba yake hiyo aliwaasaviongozi na waumini wa kanisa hilo kuepukana na vitendo vya rushwa katika kuweka uongozi kanisani hapo pamoja na kuepukana na mambo maovu na machafu ikiwemo kudumisha amani ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiimba moja ya wimbo wa maubiri na Baba Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga Askofu Damian Kiaruzi wakiwa miongoni mwa wageni waalikwa katika Mkutano huo.
Kwaya ya Kanisa hilo.
Sehemu ya waumini na waalikwa katika Mkutano huo.
Picha ya pamoja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiagana na viongozi wa kanisa hilo na baadhi ya wageni waalikwa.
(Picha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

Israel’s former Prime Minister Sharon dies at 85

56c04e938f559d01480f6a70670002f5
JERUSALEM (AP) — Ariel Sharon, the hard-charging Israeli general and prime minister who was admired and hated for his battlefield exploits and ambitions to reshape the Middle East, died Saturday, eight years after a stroke left him in a coma from which he never awoke. He was 85.
As one of Israel’s most famous soldiers, Sharon was known for bold tactics and an occasional refusal to obey orders. As a politician he became known as “the bulldozer,” a man contemptuous of his critics while also capable of getting things done.
He led his country into a divisive war in Lebanon in 1982 and was branded as indirectly responsible for the massacre of hundreds of Palestinians at the Sabra and Chatilla refugee camps outside Beirut when his troops allowed allied Lebanese militias into the camps. Yet ultimately he transformed himself into a prime minister and statesman.
Sharon’s son Gilad announced the death on Saturday afternoon. Sharon’s health had taken a downturn over the past week and a half as a number of bodily organs, including his kidneys, stopped functioning, and doctors on Thursday pronounced his condition “grave.”
“He has gone. He went when he decided to go,” Gilad Sharon said outside the hospital where his father had been treated in recent years.

DK.SHEIN ATUNUKU NISHANI

IMG_0163
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtunuku nishani ya Mapinduzi Rais Msstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Salmin Amour Juma,katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,katika shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduziya Zanzibar.[Picha na ramadhan Othman Ikulku.] TA1A8853
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtunuku nishani ya Mapinduzi Rais Msstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Amani Abeid Karume,katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,katika shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduziya Zanzibar.[Picha na ramadhan Othman Ikulku.]
TA1A8878 
Mke wa Rais wa zanzibar Mama Mwanamwema Shein akibadilishana mawazo na Rais Msstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Amani Abeid Karume (wa pili kulia ) na Rais Msstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Salmin Amour Juma,katika hafla ya kunukuku nishati iliyofanyika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,katika shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduziya Zanzibar.[Picha na ramadhan Othman Ikulku.]

KAMPUNI YA VIJANA WA KITANZANIA YA (China Word Buz) KUWAKOMBOA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA KATI

1
Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya  China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo China Bwana Cheng Wang Wu kushoto akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere huku akiwa ameongozana na Meneja Mkuu  wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda wakilakiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande, kampuni hiyo imeanzishwa nchini ikiwa na lengo la kuwakomboa na kuwasaidia wafanya biashara wadogo na wa kati nchini Tanzania ili kutafuta masoko na kuwapa taarifa sahihi za masoko na biashara nchini China ambapo wanatarajia kuendesha semina kwa wafanya biashara  katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya. 2 
Meneja Mkuu  wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere mara baada ya kwasili akitokea nchini China na ujumbe wa wafanya biashara wenzake, kushoto ni Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya  China Word Buz nchini China Bwana Cheng Wang Wu na kulia ni Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande 3 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande wa pili kutoka kulia ,Meneja Mkuu  wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda wa tatu kutoka kulia na Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya  China Word Buz nchini China Bwana Cheng Wang Wu wa tatu kutoka kushoto wakiwa na wafanya biashara wenzao. 4 
Meneja Mkuu  wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.

RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA BALOZI MPYA WA COMORO NCHINI TANZANIA

c9
Rais Jakaya Mrisho kikwete akipokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi wa Comoro Mhe Ahamed El Badaoui Mohamed Fakih ikulu jijini Dar es salaam leo January 11, 2014
c10
Rais Jakaya Mrisho kikwete akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe kwa  balozi wa Comoro Mhe Ahamed El Badaoui Mohamed Fakih ikulu jijini Dar es salaam leo January 11, 2014
c11
Rais Jakaya Mrisho kikwete akiangalia ngao aliyopewa zawadi baada ya ku[okea  hati za utambulisho kutoka kwa balozi wa Comoro Mhe Ahamed El Badaoui Mohamed Fakih ikulu jijini Dar es salaam leo January 11, 2014
c15 
Rais Jakaya Mrisho kikwete akiongea na balozi wa Comoro Mhe Ahamed El Badaoui Mohamed Fakih baada ya kupokea hati zake za utambulisho ikulu jijini Dar es salaam leo January 11, 2014. Aliyeketi kushoto ni mkalimani.
PICHA NA IKULU

TAARIFA MPYA KWA VYOMBO VYA HABARI (MSIBA)


1378039_528967223847485_1823013740_nMweka Hazina wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa), Sultan Sikilo amefariki dunia na atazikwa leo katika makaburi ya Kibada, Kigamboni katika Manispaa ya Temeke.
Msiba huo umetokea kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako marehemu alikuwa amelazwa, akitokea hospitali ya Temeke ambako nako alilazwa kwa muda mfupi.
Ikumbukwe kuwa marehemu alichaguliwa miaka mitatu iliyopita na enzi za uhai wake alipitia nafasi mbali mbali katika chama ikiwa pamoja na ujumbe. Marehemu pia alikuwa Mweka Hazina wa Timu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC).

Kutokana na msiba huu, tunawaomba waandishi wa habari za michezo nchini, wadau na jamii kwa ujumla kuwa karibu na familia yake katika kipindi hiki kigumu.

Mungu Ailaze Roho  ya Marehemu Sultani Sikilo Peponi, Amina.
 
Majuto Omary

Mwenyekiti Taswa SC

Kwa niaba ya Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa).

BENKI YA NMB YAKABIDHI TISHETI ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI KWA VIJANA WA MKOA WA KUSINI PEMBA.


1(2) 
Naibu Katibu wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Hamis , akipokea sehemu ya Tisheti maalum kwa niaba ya Makamu, kutoka kwa Meneja wa NMB Tawi la Zanzibar Town, Bakari Hamis Mohamed, kwa ajili ya Vijana wa Mkoa wa Kusini Pemba zitakazotumika katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, zinazofanyika kesho kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar. Katikati ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Abuu Msagula. Picha na OMR

POLISI WAJISHINDIA VYEREHANI NA PIKIPIKI

E88A0742Kamishna  wa Utawala na Utumishi  wa Jeshi la Polisi na Mwenyekiti wa Bodi  ya Usalama wa Raia Saccoss, Kamishna Thobias Andengenye akikata utepe kuashiria kuanza kwa bahati nasibu ya saccoss hiyo iliyofanyika jana Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam. Washindi kumi walibahatika kupata vyerehani na washindi  watano walibahatika kupata pikipiki aina ya boxer. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

MATEMBEZI YA HIYARI KWA MIGUU DAR MPAKA MORO YAANZA RASMI

001
Mratibu wa matembezi ya hiyari kwamiguu yajulikanayo kwa jina la , Matembezi ya Nchi Yangu Wajibu Wangu Utaifa Kwnza”Bw, Matukio Chuma (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa matembezi hayo kabla yakuanza matembezi kueleke Mkoa wa Morogoro yalionzia Mbezi jijini Dar es Salaam leo Januariy 11- 2014 ya kilometa 200 yatakayochua siku kumi (kushoto), Mwanakikundi kutoka Umoja wa vijana,Bw Athumani Ali ambae anawakilisha wanachama wenzie wapatao 80 (kulia), Mwanafunzi kutoka Shule ya St Joseph Univerty Bw Joseph Serengeta akiwakilisha wanafunzi wa shule hiyo. Kwa  mujibu wa muandaaji Bw, Matukio Chuma lengo la matembezi hayo yamelenga kuenzi mchango mkubwa na kuthamini kujitoa mhanga kwa waanzilishi wa utaifa wetu, (Hayati) Mwl Julius Kambarage Nyerere, Abeid Amani Karume, Edward Moringe Sokoine na wengineo ambao walisimama kidete na leo tukawa na taifa likaitwa Tanzania. 
  002
Hapa safari imepambamba moto Dar mpaka Moro eneo la Kibaha. 003
Hapa safari imepambamba moto Dar mpaka Moro eneo la Kibaha.
004
Mratibu wa matembezi ya hiyari Matukio Chuma. 
 005
Joseph Serengeta mshiriki.
  006 
Athumani Ali mshiriki.

ankarasekerspor 
Young Africans imeanza vizuri katika kambi yake ya mafunzo nchini Uturuki baada ya kuifunga timu ya Ankara Sekerspor kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika pembeni kidogo ya eneo ililofikia katika mji wa Manavgat Antalya.
Kocha wa Young Africans aliwatumia wachezaji 18 jumla katika mchezo huo ambao wenyeji mara baada ya mchezo walimpongeza kwa timu yake kwa kucheza vizuri katika mchezo huo wa kirafiki.
Dakika ya 10 ya mchezo shuti lililopigwa na mganda Emmanuel Okwi lilishinda mlinda mlango wa Ankara Sekerspor ambapo aliutema mpira huo na kumkuta Didier Kavumbagu aliyeukwamisha mpira huo wavuni na kuhesabu bao la kwanza.
Timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu na mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Ankara Sekerspor i0 – 1 Young Africans .
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na iliwachukua dakika moja Young Africans kujipatia bao la pili la mchezo kupitia kwa Emmanuel Okwi aliyeitumia vyema pasi ya mwisho ya kiungo Mrisho Ngasa aliywatoka walinzi wa Ankara Sekaspor na kumpasia mfungaji ambaye hakufanya makosa na kuukwamisha mpira wavuni.
Dakika ya 58 kocha Mkwasa alifanya mabadiliko, ambapo waliingia Hamis Kizza na Nizar Khalfani kuchukua nafasi za Didier Kavumbagu na kiungo Hassan Dilunga.
Hamis Kizza aliipatia Young Africans bao tatu la mchezo na la ushindi dakika ya 61 ya mchezo baada mpira aliogongewa na Domayo kuwapita walinzi wa Ankara Sekerspor na kumkuta Kizza ambaye alipiga shuti liliomgonga mlinzi wa Ankara Sekerspor wakati akiokoa na kujaa wavuni.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Ankara Sekerspor 0 -3 Young Africans.
Mara baada ya mchezo kaimu kocha mkuu wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa alisema anashukuru vijana wake walicheza vizuri kwa kufuata malekezo na ndio maana wakaweza kupata ushindi huo,makosa yapo machache yaliyojitokeza na ataendelea kuyafanyia kazi.
“Mechi ilikua ni nzuri ukizingatia ndo mchezo wetu wa kwanza wa kirafiki tukiwa na siku ya tatu tangu tufike hapa Uturuki, kwa mazoezi ya jana vijana wameosha mabadiliko na leo wameweza kucheza vizuri na kuweza kupata ushindi, kikubwa naamini kwa siku zilizobakia nitaendelea kufanya marekebisho na kukifanya kikosi kuendelea kuwa bora pindi kitaporejea nchini tayari kwa mzunguko wa pili wa Lig Kuu ya Vodacom” alisema Mkwasa 
Kikosi cha Young Africans kilichocheza leo ni:
1.Juma Kaseja/Ally Mustafa “Barthez” (dkk 65), 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua/David Luhende(dkk 82), 4.Mbuyu Twite (C), 5.Kelvin Yondani, 6.Frank Domayo/Ibrahim Job(dkk 80), 7.Haruna Niyonzima/Saimon Msuva (dkk72), 8.Hassan Dilunga/Nizar Khalfan (dkk 58), 9.Didier Kavumbagu/Hamis Kizza (dkk 58), 10.Mrisho Ngasa/Jerson Tegete (dkk 68), 11. Emmanuel Okwi/Said Bahanuzi (dkk 85)

Askari 45 wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha watawanywa katika Tarafa tatu mkoani humo

GEDSC DIGITAL CAMERA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akiongea na askari, viongozi wa vyama na serikali, vikundi vya ulinzi shirikishi pamoja na wananchi wa eneo la Tarafa ya Themi wakati wa kuwatambulisha askari 15 watakaoungana na wananchi wa eneo hilo katika utendaji wa kazi za kipolisi za kila siku.(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
GEDSC DIGITAL CAMERA 
Viongozi wa serikali za mitaa,Askari, vikundi vya ulinzi pamoja na wananchi wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas wakati akielezea mikakati ya Polisi 15 watakaokuwa wanafanya kazi katika tarafa ya Themi pamoja na wananchi wa eneo hilo. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
……………………………………………………………………………
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Jumla ya askari 45 ambao walikuwa wanafanyakazi Kituo Kikuu cha Polisi Arusha na Kitengo cha Usalama Barabarani wametawanywa katika tarafa tatu za jijini hapa. Askari hao kutoka vitengo mbalimbali wamesambazwa katika tarafa za Themi, Elerai na Suye wakiwa ndani ya kikosikazi ambacho kinajumuisha askari wa Upelelezi, Usalama barabarani na askari wa kawaida ambapo lengo kubwa ni kushirikiana kwa ukaribu na wananchi.
Akizungumza na wananchi katika matukio ya ukaguzi wa tarafa hizo pamoja na kuwatambulisha askari hao jana tarehe 10.01.2014 katika tarafa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas amesema kwamba, jamii katika maeneo yao ikiamua kupinga uhalifu toka ngazi ya familia kwa kushirikiana na nguvu ya askari hao hakika uhalifu utapungua kama si kutokuwepo kabisa.
“Hapo awali jeshi la Polisi lilikuwa na askari kata lakini baadae likawa na askari tarafa na kuona kwamba hiyo haitoshi sasa limeamua kuanzisha kanda za kitarafa ambapo kila tarafa itakuwa na askari 15 kutoka vitengo mbalimbali watakaoongozwa na Mkaguzi wa Polisi, hali hii itasaidia kujenga ukaribu kati ya wananchi na jeshi la Polisi na kutatua matatizo mbalimbali ya kiusalama kabla hata ya kufika ngazi ya wilaya”. Alifafanua Kamanda Sabas.
Kamanda Sabas aliendelea kusisitiza kwa kuwaomba viongozi wa tarafa hizo kuhakikisha kwamba, vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo vimeundwa viendelee kuwa hai ili ustawi wa usalama wa watu na mali zao uendelee kuwepo. Pia aliwaomba waendelee kukusanya michango toka kwa wananchi wa maeneo yao ili zisaidie kuwapa posho askari wa vikundi vya ulinzi shirikishi na kununulia vitendea kazi kwani jukumu la ulinzi ni watanzania wote na hasa wazalendo na kila mmoja aone umuhimu wa amani na usalama.
Alisema pamoja na wananchi hao kujitahidi kupambana na uhalifu na kuwakamata wahalifu lakini baadhi yao huwa hawajitokezi kutoa ushahidi mahakamani hali ambayo inasababisha watuhumiwa waachiwe huru na kupata ujasiri hivyo kuweza kujiunga na makundi mengine kuendelea kufanya uhalifu.
Kamanda Sabas alitoa namba zake tatu za simu kwa wananchi hao ili ziweze kusaidia katika mawasiliano na kuongeza kwamba, japo kuwa askari hao 15 wapo katika maeneo yao, bado wapo huru kuwasiliana naye na viongozi wengine katika kupeana taarifa za uhalifu na wahalifu huku akisisitiza pia ofisi yake ipo wazi kwa wale watakaotaka kwenda kumuona.
Kwa upande wake Diwani wa Tarafa ya Themi kutoka kata ya Unga Limited Mh.Issa Omari (CCM) alisema kwamba mpango huo wa askari 15 kupelekwa katika tarafa hiyo utasaidia katika kudhibiti vitendo vya uhalifu kwani kutakuwa na nguvu ya pamoja ya ulinzi ambayo itakuwa inajumuisha askari wa Jeshi la Polisi na vikundi vya ulinzi shirikishi.
Diwani huyo wa Unga Ltd aliwataka askari wa vikundi vya ulinzi shirikishi wasirudi nyuma bali wanatakiwa kusonga mbele na yeye pamoja na wananchi wanaliunga mkono Jeshi la Polisi kwa mpango huo; huku akiongeza kwa kusema kwamba katika kata yake uhalifu umepungua kwa kiasi kikubwa baada ya kuwepo kwa ushirikiano kati ya jeshi la Polisi, viongozi wa mtaa huo na vikundi vya ulinzi shirikishi.
Naye Diwani wa kata ya Elerai Mh. Mhandisi Jeremiah Mpinga wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tarafa ya Elerai alisema, sasa umefika wakati wananchi wa eneo lake waondoe itikadi zao za vyama badala yake wote washirikiane katika suala zima la kuimarisha ulinzi huku akiwata viongozi wa mitaa kuhamasisha uanzishaji zaidi wa vikundi vya ulinzi shirikishi ili washirikiane na askari wa jeshi la Polisi huku akiunga mkono mpango huo kwa kauli mbiu yake isemayo “ULINZI KWANZA MAISHA SALAMA”.