TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, July 28, 2014

AIRTEL RISING STAR MICHUANO YA VIJANA YAZINDULIWA JIJINI DAR

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki akisalimiana na wachezaji wa timu za Ilala wakati akizindua rasmi mashindano ya vijana ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dar es Salaam jana.
 Mshambuliaji wa timu ya Ilala, Rashid Mohamed (kulia) akimtoka beki wa timu ya Buguruni Youth Center, Khamis Mohamed katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dar es Salaam jana.
 Mshambuliaji wa timu ya Ilala, Edwin Francis (kushoto) akituliza mpira mbele ya  beki wa timu ya Buguruni Youth Center, Salum Abdallah katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dar es Salaam jana.
 Mshambuliaji wa timu ya Ilala, Rajabu Ally (kushoto) akimtoka beki wa timu ya Buguruni Youth Center, Hassan Omari  katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dar es Salaam jana.
 Mshambuliaji wa timu ya Ilala, Francis Edwin (kushoto) akiwania mpira na beki wa timu ya Buguruni Youth Center, Hassan Juma katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dar es Salaam jana.

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaendesha warsha ya uandishi bora wa tafiti kwa wataalamu wake

_1055413.JPG-3 Research methodology
Aziz Kilonge Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga warsha ya mafunzo ya uandishi bora wa tafiti ili kukidhi hitaji la msingi la kuhitimu taaluma ya ununuzi na ugavi iliyoratibiwa na kuendeshwa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kuazia tarehe 21 julai mpaka 25 julai 2014. 

kwenye ukumbi wa baraza la maaskofu TEC-Kurasini jijini Dar es salaam akiwa katika [icha ya pamoja na wakufunzi, washiriki pamoja na baadhi ya wakuu wa taasisi hiyo .kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa PSPTB Dr. Clemence Tesha, kutoka kushoto ni Dr. E. Tumsifu-mwezeshaji wa washa na Ally Songoro Mkurugenzi wa Mafunzopamoja na washiriki wa warsha hiyo.
_1055431.JPG-1 research methodology
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa (PSPTB) Dr. Clemence Tesha, kutoka kushoto ni Dr. E. Tumsifu-mwezeshaji wa washa na Ally Songoro Mkurugenzi wa Mafunzopamoja na washiriki wa warsha hiyo pamoja na wanawarsha.
_1015339.JPG-2-research methodology
Picha ya pamoja ya washiriki na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa maelezo zaidi kuhusu taarifa mbalimbali za bodi wataalamu wa Ununuzi na Ugavi kwa kubofywa hapa www. psptb.go.tz

VIJANA WANUFAIKA NA SHIRIKA LA NYUMBA NHC

1

Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Bi Rachel Kasanda akikabidhi mashine za kufyatulia matofali kwa Hassan Soud Katibu wa kikundi cha Changamoto kwa niaba ya vikundi vingine vya wilaya ya Ilala ambazo zimetolewa na shirika la Nyumba nchini NHC jana wakati wa mpokezi ya Mwenge wa Uhuru Ilala Boma mara baada ya Meneja wa Shirika hilo wilaya ya Ilala Bw. Jackson Maagi kumkabidhi kiongozi huyo wa mbio za mwenge ikiwa ni juhudi za shirika hilo kusaidia kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana ili waweze kujiajiri kwa kuyatua matofali na kuuza.
3
Askari wa Kikosi cha FFU wakiulinda mwenge mara baada ya kuwasili Ilala Boma mahali ambapo ndiyo kituo ulipolala mwenge huo.
4
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Jackson Maagi wa pili kutoka kushoto akiwa pamoja na wafanyakazi wnzake kabla ya kukabidhi mashinne hizo jana.
2
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Jackson Maagi akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hizo jana
=========================================
HOTUBA FUPI YA MENEJA WA NHC ILALA KWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA

Ndugu kiongozi wa Mbio za mwenge, Ninayo furaha kubwa sana kusimama mbele yenu na kuongea nanyi kama mwakilishi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge; Shirika la Nyumba la Taifa lina mpango mkakati wake wa miaka mitano ambao moja ya malengo yake sita makuu ni kuboresha taswira ya Shirika. 

  Katika utekelezaji wa lengo hili, Shirika lina sera ya huduma kwa jamii ambayo imejikita katika kusaidia vijana kujiajiri. Ili kuwezesha vijana kujiajiri, Shirika limeamua kuzisaidia Halmashauri za Miji na Wilaya kote nchini mashine za kuwezesha vikundi vya vijana kutengeneza matofali ya kujengea nyumba. Nchi yetu ina Halmashauri 160 na kila Halmashauri itapewa mashine 4 kwa ajili ya kusaidia vikundi vya vijana. Katika mpango huu jumla ya mashine 640 zitatolewa na Shirika na kugharimu shilingi 288,000,000/.

  Aidha, kila Halmashauri itapatiwa shilingi laki tano (500,000/=) kama mtaji kwa vijana kuanzia shughuli yao ya kutengeneza matofali. Kadhalika, Shirika limegharamia shilingi 800,000/= kwa kila Halmashauri kwa ajili ya kuwalipa wakufunzi kutoka VETA wanaotoa maelekezo kwa vijana namna ya kutumia mashine hizo.  

Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge,katika kutekeleza mradi huu jumla ya shilingi milioni mia saba (700,000,000/=) zitatumika. Aidha, tunatarajia kuwa ajira zaidi ya 8,000 za moja kwa moja na ajira nyingine zaidi ya 200,000 zisizo za moja kwa moja zitapatikana. Katika mpango huu kila Wilaya inatakiwa kuwa na vijana 40 watakaokuwa katika vikundi vya watu 10 kila kimoja. Msaada huu ni mkubwa lakini kutokana na ukubwa wa tatizo la ajira jitihada zaidi kutoka kwa wadau mbalimbali zinatakiwa. 

Ni matarajio yetu kuwa taasisi nyingine ama mtu mmoja mmoja atashiriki kukwamua vijana hawa. Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge, kupitia maadhimisho haya, Shirika linatoa mashine nne (4) kwa vikundi 4 vya vijana vilivyoundwa katika wilaya ya Ilala ambapo kila kikundi kina jumla ya vijana10 watakaotumia mashine moja. Hivyo jumla ya vijana 40 katika Wilaya hii watapata ajira kutokana na mashine hizi. Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge, mwisho Shirika linatoa rai kwa Taasisi za serikali, mashirika ya umma, binafsi na watu mbalimbali, kuunga mkono juhudi za Serikali za kupunguza tatizo la ajira kwa vijana. 

Ni matumaini yetu kuwa tutawaunga mkono kwa kununua matofali yao ama kusaidia upatikanaji wa mashine nyingine zaidi ili wengine ambao hawajafikiwa na mradi huu wafikiwe na wapate kufaidika. Kipekee tunaomba Serikali za Mitaa (kwa maana ya Halmashauri zetu za wilaya, miji, manispaa ama jiji) wawe ni wanunuzi wakuu wa matofali yatakayotengenezwa na vikundi hivi vya vijana ambayo ni ya gharama nafuu ili kusaidia miradi mbalimbali ya ujenzi na kuwaongezea kipato chao. Tunawaomba pia msaidie kusimamia mradi huu ili uweze kuwa endelevu.

MAPOKEZI YA DIAMOND BAADA YA KUSHINDA TUZO YA MSANII BORA WA KIUME AFRIKA MASHARIKI






Rais Kikwete aandaa futari kwa yatima, walemavu wa ngozi na watoto waishio kwenye mazingira magumu ikulu Dar es salaam

Rais Kikwete akipakua futari  Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni.
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
================
kwa habari zaidi bofya hapa.
www.ambassadorodemocracytanzania.blogspot.com

AJALI HAINA KINGA,MADEREVA TUWE MAKINI BARABARANI,HII IMETOKEA JIJINI MBEYA MAPEMA LEO.

Wasamalia wema wakijaribu kulinasua gari aina ya Toyota Corolla (namba zake za usajili hazikuweza fahamamika mara moja kutokana na kutokuwepo) lililoingia kwenye mtaro baada ya dereva wake kuzidiwa maarifa ya kiudereza na kujikuta akiingia mtaroni,katika eneo la Mafiat mkabala na kituo cha mafuta cha Oilcom jijini Mbeya asubuhi hii.Dereva wa Gari hilo pamoja na mtu mwingine mmoja wamejeruhiwa na kukimbizwa hospital kwa matibabu.Chanzo cha ajali hiyo inaelezwa ni mwendo kasi aliokuwa nao Dereva wa gari hilo.
Wasamalia wema hao wakiangalia namna ya kuweza kulichomoa gari hilo.
Hayaaaa..... Moja.... mbili.... tatuuu twendeeeeeeee......
Mara wakafanikiwa kulitoma kwenye mtaro huo.Picha na Fadhil Atick,Mbeya

TAARIFA YA JUKWAA LA KATIBA KUHUSU BUNGE MAALUM LA KATIBA

 Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa tamko kuhusu Bunge la Katiba litakaloanza Agosti 5, 2014 ambapo walishauri Bunge hilo likae wiki mbili badala ya miezi miwili kama ilivyopangwa ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za Umma. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Kamati na Uongozi Jukata Omar Ali Omar,  Meneja Habari na Mawasiliano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Kenny Ngomuo, Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda na  Mratibu wa Jukata, Diana Kidara.
 Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda, akisoma tamko hilo.
 Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

SERIKALI YAIFUNGA HOSPITALI YA IMTU

IMTU_HOSPITAL_90a29.png

Serikali imeifungia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), baada ya kuifanyia ukaguzi na kubaini kasoro kadhaa za uendeshaji wake.
Ukaguzi huo ulifanywa jana na jopo la wataalamu kutoka Manispaa ya Kinondoni, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, baada ya IMTU kukumbwa na kashfa ya utupaji wa mabaki ya viungo vya binadamu katika Bonde la Mto Mpiji, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Ukaguzi huo ulifanywa jana na jopo la wataalamu kutoka Manispaa ya Kinondoni, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, baada ya IMTU kukumbwa na kashfa ya utupaji wa mabaki ya viungo vya binadamu katika Bonde la Mto Mpiji, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hospitali hiyo imefungiwa wakati Kamati ya Watu 15, iliyoundwa na Serikali ikiendelea kuchunguza kashfa hiyo.
Hata hivyo, wakati taarifa za kufungiwa zikitolewa habari za ndani zinaonyesha kuwa hapakuwa na mgonjwa yeyote hospitalini hapo, ikielezwa kuwa wagonjwa wote waliondoka baada ya kuibuka kwa kashfa ya viungo IMTU ikihusishwa.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk Bunini Kamba alisema kuwa wameamua kuifungia hospitali hiyo kwa muda usiojulikana, baada ya kukuta upungufu mbalimbali katika maeneo ya kutolea huduma, jambo linalohatarisha usalama wa wagonjwa.
"Maabara tumekuta dawa ambazo muda wake wa kutumika umepita na hazikuwa katika mpangilio maalumu. Wodini hakuna usimamizi maalumu, hasa kwa wagonjwa wenye majeraha," alisema Dk Bunini.
Aliongeza: "Hakuna wauguzi wa kutosha na mashine ya kuchoma taka ngumu haifanyi kazi vilivyo. Tumeona kuwa hospitali hii haistahili kuendelea kutoa huduma kwa jamii."
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Profesa Yasin Mgonda alisema: "Tumesikia uamuzi huo uliotolewa baada ya kufanyika ukaguzi. Tutajirekebisha na tutakapokamilisha tutawaita kuja kutukagua tena."
Alisema kuwa pamoja na sababu nyingine, hospitali yake imefungiwa baada ya kubainika kuwa bomba la maabara limeharibika na halitoi maji.
Nyingine ni kutojaza vitabu vya wagonjwa kwa mujibu wa taratibu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, pia duka lake la dawa kuwa halijasajiliwa lakini akasema sababu hiyo imewashangaza kwani wanachojua wao duka hilo limesajiliwa.
Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Primus Saidia aliliambia gazeti hili kwamba anaipongeza Serikali kwa uamuzi huo akisema utanusuru maisha ya wananchi waliokuwa wakipata huduma hospitalini hapo.
"Tunaipongeza Serikali, ila tunaiomba iwatafutie wanafunzi wa chuo hicho maeneo mengine ya kujifunzia," alisema Dk Saidia.
Juzi, Dk Saidia alisema kuwa wote waliohusika na kashfa ya utupaji mabaki ya viungo vya binadamu wanastahili kuchukuliwa hatua kali kwa sababu kitendo hicho kimekiuka sheria, taratibu, haki za binadamu, maadili ya ufundishaji na taaluma ya udaktari.
"Kama ni taasisi ya utafiti imepoteza sifa ya kufanya utafiti na kama ni ya mafunzo basi imepoteza sifa ya kutoa mafunzo ya tiba. Kama ni hospitali itakuwa imepoteza sifa za kutoa tiba kwa binadamu," alisema Dk Saidia.
Naye spika wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho (IMTUSO), William Mapunga alisema kuwa kufungiwa kwa hospitali hiyo kutawaathiri, kwani watakosa sehemu ya kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo, akiiomba Serikali kuliangalia suala hilo kwa mapana.
Chanzo:Mwananchi

WAZIRI MAHENGE AKIFUTIA VIBALI VYA KUNUNUA KUNI NA MAGOGO KIWANDA CHA SUNFLAG TANZANIA LTD ARUSHA.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhlopby_0m03MR9SrLL_s-j9b1m5owT5DxLRcJkjAutfYaPpLPGzjhPMtSXPLul-0UTdJ3jlrMLXs9DprL0mu2FKGS2qIS-PpjzjOkJeGGuxV2rhkt_rtm-ngsMUjljDMFnLuJ5HXJucIA/s1600/RUNDO+LA+VIPANDE+WA+MAGOGO+KIWANDANI.2.JPG Mahmoud Ahmad Arusha 

SERIKALI imesitisha vibali vyote vilivyotolewa vya kununua kuni na magogo kwa ajili ya nishati ya kuendesha viwanda mbalimbali nchini na badala yake imevitaka ndani ya muda wa miezi mitatu kuanzia leo viwe vinatumia teknolojia ya makaa ya mawe, umeme na gesi kwa ajili ya kuendeshaji wa viwanda hivyo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira Dkt Binilith Mahenge baada ya kufanya ziara kiwanda cha kufuma nguo cha Sunflag Tanzania ltd, kilichopo eneo la Themi jijini Arusha na kushutushwa na shehena kubwa ya magogo yaliyorundikwa katika kiwanda cha Sunflug ambayo kiwanda hutumia kwa ajili ya nishati.

” Hali hii inatisha sana katika suala la mazingira na kamwe serikali halitalivumilia kwa kiwanda kama hiki kukata miti kwa kiwango kikubwa hicho na huu ni uharibifu mkubwa wa mazingira “alisema waziri mahenge

Kufuatia hali hiyo Waziri Dkt Mahenge amefuta vibali vyote vilivyotolewa kwa kiwanda hicho kwa ajili ya kununua kuni kwa ajili ya Nishati

Kufuatia hali hiyo ya kutisha ya kuwepo na shehena ya magogo Serikali imeuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuacha mara moja matumizi ya nishati ya magogo kuanzia sasa na imetoa muda wa miezi mitatu kiwanda kiwe kimeaanza kutumia nishati ya gesi, umeme na makaa ya mawe.

Ameuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha kinawalipa walinzi watakaowekwa na serikali ngazi ya mkoa ili kuzuia uingizwaji wa magogo na kuni kiwandani hapo kwa ajili ya nishati.Katika hatua nyingine waziri amekitoza faini ya shilingi milioni 80 kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira ,na kukiagiza kushirikiana na mkoa pamoja na baraza la taifa la mazingira kanda ya kaskazini kutafuta eneo litakalopandwa miti milioni 7 .Waziri amezitaja sababu mbali mbali zinazosababisha afrika kuendelea kuwa maskini kuwa ni pamoja kuwa tuko nyuma katika matumizi ya sayansi na teknolojia, hatuna elimu kubwa ya kukabiliana na majanga mbalimbali ikiwemo njaa na mafuriko yanayoharibu miundo mbinu ,kiwango kikubwa cha uharibifu wa mazingira ,mabadiliko ya tabia nchi, hivyo mkazo zaidi unawekwa kupunguza matumizi ya kuni na badala yake kusisiotiza matumizi ya sayansi na teknolojia.

Waziri huyo wa Mazingira ambaye pia ni mbunge wa makete mkoani Njombe amesisitiza kuwa matumizi ya nishati ya magogo katika uendeshaji maboila katika kiwanda umepitwa na wakati kutokana na mabadiliko ya Teknolojia

Hali hii imeshutua sana waziri Mahenge baada ya kuona shehena kubwa ya magogo hayo ambayo inaaminika yamevunwa kwa kipindi cha miaka mingi ambapo kila siku kiwanda hicho hutumia tani zaidi ya 1,500 za magogo kama nishati.
Akizungumza wakati wa ziara ya kiwanda hicho Mkurugenzi Mkuu wa baraza la taifa la mazingira katika ofisi ya Makamu wa Rais Eng.Boneventura Baya amesema hali hii ni mbaya na haikubaliki kabisa imechangia kwa kiwango kikubwa katika uharibifu wa mazingira.
Amemwagiza Mwanasheria wa Baraza la taifa la mazingira ,Machale Heche kuchukua hatua za haraka kuanzia leo kusimamisha uingizaji wa magogo katika kiwanda hicho na kusisitiza kuwa kuanzia jana hakuna mzigo au shehena ya aina yeyote ya kuni na magogo itakayoingizwa kiwandani hapo na oda zote zilizokuwa zimetolewa na kiwanda hicho za ununuzi wa kuni na magogo zimesimamishwa.
Mhandisi Baya alisema kiwanda hicho kimekuwa kikivuna miti ya asili na ile ya kupanda hali ambao imechangia uharibifu mkubwa wa mazingira.
Amesema magogo yamevunwa kwa zaidi ya miaka saba hivyo ameonya kwamba tuogope kuchezea suala la mazingira.
Kwa upande wake Mwanasheria katika baraza la Mazingira la taifa Manchale Heche amesema kutokana na shehena kubwa ya miti iliyovunwa na kiwanda hicho uongozi wa kiwanda hicho unapaswa kupanda zaidi ya miti milioni saba ili kufidia uharibifu huo.
Amesisitiza kwamba kiwanda hiki kimechangia mabadiliko makubwa katika mfumo wa hali ya hewa. 

MH:MWIGULU NCHEMBA ALIVYOHUTUBIA TAIFA JIJINI MWANZA KATIKA MKUTANO WA KIHISTORIA

Add caption

VIPIMO VYA MCHEZAJI WA QPR, LOIC REMY ALIVYOFANYIWA NA LIVERPOOL VYAGONGA MWAMBA.

Uhamisho wa pauni milioni 8.5 wa Loic Remy, 27, kutoka QPR kwenda Liverpool umeshindwa kukamilika.
Liverpool hawataki kusema kwanini uhamisho huo umeshindikana, lakini inasemekana huenda mchezaji huyo ameshindwa kupita vipimo vya afya.
Remy alisafiri hadi Marekani siku ya Jumatatu ambapo Liverpool wanafanya ziara.
Liverpool walipanga kumpa jezi namba 7 kama mkataba ungekamilika.
Remy sasa huenda akalazimika kurejea QPR.

SIMANZI ZAENDELEA KUTAWALA NDANI YA NYUMBA YA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT)

Jaji Vyonne Cherry au Monalisa akitoa maoni kwa washiriki waliokuwa wameshiriki kwenye filamu fupi iliyochezwa na washiriki wa TMT
  Kundi la Kwanza la Washiriki wa TMT waliocheza filamu fupi iitwayo LUGHA GONGANA wakiwa mbele ya meza ya Pilato katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa mwanzoni mwa wiki.
=====================
kwa taarifa zaidi bofya hapa.
www.missdemokrasia.blogspot.com

MAITI ZA BINADAMU ZATUMIKA KUFUNDISHIA WANAFUNZI WA UDAKTARI TANZANIA.


Viungo vya Binadamu ambayo hutumika kufundishia madaktari.

Dar es Salaam.  
Wakati sakata la kuokotwa kwa viungo vya binadamu likiendelea kutikisa nchi, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), kimesema kuwa hutumia maiti 25 kwa kuwafundishia wanafunzi kila mwaka. 

Pia chuo hicho hakijawahi kuagiza maiti kutoka nje ya nchi na kwamba ni mtu mmoja tu aliyewahi kutaka maiti ya mtoto wake itumike kufundishia. 

Kauli hiyo ya MUHAS imekuja siku chache baada ya Serikali kuamua kuifungia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), baada ya kubaini kasoro kadhaa katika utendaji wake. 

Juzi, Serikali ilifanya ukaguzi wa kushtukiza IMTU, baada ya hospitali hiyo kukumbwa na kashfa ya utupaji wa mabaki ya viungo vya binadamu katika Bonde la Mto Mpiji, jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki iliyopita. 

KWA TAARIFA ZAIDI BOFYA HAPA.
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com

SERENGETI BOYS KWENDA AFRIKA KUSINI LEO

Mshambuliaji wa timu ya Serengeti boys Athanas Mdamu akichuana na beki wa Afrika Kusini Notha Ngcobo

Mshambuliaji wa timu ya Serengeti boys Athanas Mdamu akichuana na beki wa Afrika Kusini Notha Ngcobo.

Msafara wa watu 25 wa kikosi cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) unaondoka (Julai 28 mwaka huu) kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos).

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto, Johannesburg kuanzia saa 9 kamili mchana kwa saa za Afrika Kusini.

Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Mshindi atacheza raundi ya mwisho ya michuano hiyo ya Afrika na mshindi wa mechi kati ya Misri na Congo Brazzaville.

Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitafanyika mwakani nchini Niger.

Wachezaji wanaounda kikosi cha Serengeti Boys katika msafara huo utakaoondoka saa 2 usiku kwa ndege ya Fastjet ni Abdallah Jumanne Shimba, Abdulrasul Tahil Bitebo, Abutwalibu Hamidu Msheri, Adolf Mtsigwa Bitegeko, Ally Aziz Mnasi, Ally Shaban Mabuyu na Athanas Enemias Mdamu.

Wengine ni Badru Haji Othman, Baraka Yusuph Baraka, Issa Backy Athuman, Juma Ally Yusuph, Kelvin Longnus Faru, Martin Kiggi Luseke, Metacha Boniface Mnata, Mohamed Mussa Abdallah, Omary Ame Omary, Omary Natalis Wayne, Prospal Alloyce Mushin na Seif Said Seif.

Benchi la Ufundi linaongozwa na Kocha Mkuu Hababuu Ally Omary akisaidiwa na Stewart John Hall (Mshauri wa Ufundi), Peter Manyika (Kocha wa makipa), Richard Yomba (Daktari), na Edward Venance (Mtunza vifaa).

Msafara wa timu hiyo itakayorejea nyumbani Agosti 4 mwaka huu unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Khalid Mohamed Abdallah.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

RAIS KIKWETE, WAZIRI MKUU PINDA NA JAJI MKUU WAKARIBISHWA FUTARI KWA MAKAMU WA RAIS DKT BILALI

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiweka sawa  kanzu ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kabla ya kushiriki katika futari waliyoandaliwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam Ijumaa jioni Julai 25, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman wakiwasili kushiriki katika futari waliyoandAaliwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam Ijumaa jioni Julai 25, 2014.PICHA NA IKULU

WAZIRI MKUU MHE MIZENGO PINDA AANDAA FUTARI NYUMBANI KWAKE DAR ES SALAAM

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum alipowasili kwenye makaazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda (nyuma yao) Oysterbay jijini Dar es salaam kwa ajili ya Futari Jumamosi Julai 26, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na wa pili kulia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova
 Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakijumuika na waumini wengine katika Swala ya Magharibi katika  makaazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda Oysterbay jijini Dar es salaam alikoandaa Futari Jumamosi Julai 26, 2013
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na baadhi ya waalikwa kwenye futari aliyoandaa, wakiwemo waigizaji Mpoki wa Ze Komedy, Stephen JB, na watangazaji wa redio
 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ndg Ramadhani Madabida wakipakua futari
 Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akijumuika na waalikwa wengine kupakua futari
===========================
habari zaidi na Picha Bofya hapa. www.ambassadorofdemocracytanzania.blogspot.com

CHADEMA WILAYANI MAKETE WAFANYA UCHAGUZI MKUU KWA MARA YA KWANZA

 Msimamizi wa Uchaguzi Bw. Alfred Kayombo (kulia) akimtangaza mshindi wa nafasi ya mwenyekiti Bw. Ibrahim Ngogo.
Kwa mara ya kwanza katika historia, chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Makete mkoani Njombe kimefanya uchaguzi wa uongozi mbalimbali ambapo Bw. Ibrahim Ngogo amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa ngazi ya wilaya.

Na Edwin Moshi, Makete
Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo Bw. Alfred Kayombo amesema Bw. Ibrahim Ngogo amepata kura 25 akifuatiwa na Isaac Sanga aliyepata kura 6 na Shaaban Mkakanze aliyepata kura 1.

Bw. Kayombo amesema kutokana na umuhimu wa demokrasia ndani ya chama hicho, wameamua kufanya uchaguzi huo kwa mara ya kwanza toka chadema iingie wilayani hapa, hivyo kuonesha kuwajali wanachama wake
Mbali na viongozi hao wa juu wa chama pia Bw. Lazaro Chaula amechaguliwa kuwa katibu mwenezi wa Chadema wilaya ya Makete kwa kupata kura 30, Bi. Rose Mbilinyi amechaguliwa kuwa Mtunza hazina wa wilaya kwa kupata kura 26.
Aidha Bw. Atukuzwe Mahenge amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la vijana (BAVICHA) wilaya na Bw. Shadraack Mwachota akichaguliwa kuwa katibu wake na wote wamepita bila kupingwa.
Bi. Beatrice Kyando amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chadema wilaya (BAWACHA), Bi Christina Timoth akichaguliwa kuwa katibu wa BAWACHA, na Bi. Mariam Asheli akichaguliwa kuwa Katibu wa uhamasishaji wa BAWACHA na wote wamepita bila kupingwa.
katika uchaguzi huo pia Bw. Abiud Elia amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la wazee kwa kura 3, Abeli Juma Sanga akipata kura 1 na kuchaguliwa kuwa Makamu mwenyekiti, pamoja na Simon Nyasanga kuwa katibu wa baraza la wazee wilaya.
Katika hatua nyingine wamechaguliwa wajumbe 4 waliochaguliwa kuingia kwenye kamati tendaji ambao ni John Sanga, Patison Pela,Orignal Sanga na Alafat Msigwa, huku Bw.Illomo Werner Naftal akichaguliwa kuwa mwakilishi wa wilaya kwenye mkutano mkuu taifa.
Akiahirisha mkutano huo mwenyekiti wa Chadema wilaya Bw. Ibrahim Ngogo amewasihi wajumbe kuondoa makundi na kutokubali kutumia kwa ajili ya kukibomoa chama na badala yake washikamane wawe kitu kimoja kukijenga chama.
"Makamanda uchaguuzi umeisha haitakiwi tuwe na makundi, tushikamane kukijenga chama chetu, hilo ndilo la msingi kwa sasa, sisi viongozi mtupe ushirikiano" amesema Ngogo

Nakumatt yafungua tawi la kwanza nchini Tanzania, yapanga kufungua mengine mawili siku zijazo

 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Janet Mbene akiangalia bidhaa wakati wa ufunguzi huo .
Wafanyakazi wa Nakumatt Mlimani wakifurahia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mall hiyo Mlimani City jijini Dar es salaam
Furaha ya kuanza kazi Nakumatt Mlimani 
Mkurugenzi Mtendaji wa Nakumatt Holdings, Atul Shah akimuonesha baadhi ya bidhaa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Janet Mbene wakati wa ufunguzi huo
KAMPUNI ya Nakumatt Holdings, imezindua rasmi tawi la kwanza kati ya matawi yake matatu makubwa nchini Tanzania ambayo awali yalimilikiwa na Kampuni ya Shoprite ya Afrika ya Kusini. 

Ikiwa ni mpango wake mpya wa kuboresha zaidi huduma zake, Nakumatt holdings, imezindua tawi hilo kubwa ambalo litakuwa utambulisho muhimu wa huduma zake katika eneo la biashara la Mlimani City litakaloitwa Nakumatt Mlimani. 

Tawi hilo la 48 la Nakumatt limepambwa kwa rangi na mwonekano wa alama za Nakumatt na kwa ubunifu wa hali ya juu. Pamoja na Nakumatt Mlimani, kampuni hiyo pia iko mbioni kuzindua tawi lengine kubwa litakalojulikana kama ‘Nakumatt Pugu Road’ jijini Dar es salaam ambako pia kutakuwa makao yake makuu. Pia itafungua Nakumatt Arusha siku zijazo. 

 Kwa kufungua matawi yake matatu moja baada ya jingine, Nakumatt pia itakuwa imefikisha matawi 50 katika mtandao wake wa huduma za uuzaji bidhaa na hivyo kutekeleza mkakati wake wa maendeleo ambao ulizinduliwa mwaka 2011.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka lake la kwanza in Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Nakumatt Holdings, Atul Shah alisema kufunguliwa kwa matawi matatu mapya yaliogharimu takriban dola za Marekani milioni 3 ni sehemu ya mpango wa upanuzi wa huduma za uuzaji bidhaa katika kanda ya Afrika. Kutokana na uzinduzi wa Tawi la Nakumatt Mlimani, Shah alisema kuwa Nakumatt sasa ina maduka mawili makubwa yanayofanya kazi nchini Tanzania. 
Nakumatt Mlimani inaungana na duka jingine la la Nakumatt Moshi lililofunguliwa mwaka 2011 katika mji huo ambako kuna Mlima Kilimajaro. 
”Uzinduzi wa Nakumatt Mlimani ni ndoto ya muda mrefu ambayo sasa imekuwa kweli ambapo tumekuwa tukifikira mahali pa kuweka duka letu jijini Dar es salaam na maeneo mengine nchini Tanzania,” alisema Shah na kuongeza: “Uzinduzi huu pia ni hatua nzuri itakayopelekea uzinduzi mwingine wa duka letu la 50 katikati ya Agosti ambapo tutakuwa tumefanikiwa kufikia malengo yetu tuliyojiwekea kuyafikia Februari mwakani.” Maduka matatu ya Shoprite yalifungwa mwezi uliopita ili kufanikisha kazi ya kuyaboresha zaidi sambamba kwa kuzingatia viwango na uzoefu wa Nakumatt. 

Pia Nakumatt inatarajia kufungua matawi mengine matatu ya biashara nchini Kenya kabla ya mwisho wa mwaka huu. Pia kampuni hiyo itakuwa na duka kubwa katika eneo kubwa la kifahari la Green Square mjini Kericho nchini Kenya. Shah alisema Nakumatt ina mkakati wa kukuza biashara wa kampuni ambao unategemea zaidi uwepo wa vitega uchumi ambapo kampuni inaweza kuendesha shughuli zake za maduka ya supermaketi. Shah aliongeza kwa kusema:

 “ Kwa sasa tunaendesha shughuli zetu katika nchi 12 na tunashirikiana na wamiliki wa maeneo ya biashara nchini Kenya ambao wanaweza kutoa huduma za kujenga maeneo ya maduka makubwa katika maeneo ya Machakos, Nyeri, Kajiado, Garissa, Embu, Naivasha,Narok Busia and Homabay.” 

Ili kutimiza masharti ya Nakumatt, Shah aliwahimiza waendelezaji wa maeneo ya biashara na Mameneja wa Miradi kushauriana na wataalam wa Nakumatt kuhusu namna ya kuboresha uchoraji wa ramani na ujenzi wenye mvuto kwa wateja katika maduka ya kampuni hiyo.

NSSF YAFUTURISHA WASTAAFU WAKE MKOA WA TANGA

Principle Operation Officer wa NSSF, Joyce Mruma akigawa zawadi kwa wastaafu wa NSSF wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na shirika hilo. 
Ofisa Mwandamizi wa Operesheni wa NSSF, Lydia Ignace akitoa zawadi kwa wastaafu wa Shirika hilo waliohudhuria hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga.
=============================
HABARI ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI BOFYA HAPA.
 www.missdemokrasia.blogspot.com