TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, October 1, 2014

MKUTANO WA SIKU MBILI JUU YA MABADILIKO YA TABIANCHI, UHAKIKA WA CHAKULA NA HAKI ZA ARDHI ULIOANDALIWA NA OXFAM PAMOJA NA FORUM CC WAANZA LEO KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE DAR ES SALAAM.

 Jenerali Ulimwenguambaye ndiye mwezeshaji  akiendelea kutoa Mwongozo katika mkutano wa siku mbili juu ya mabadiliko ya Tabianchi, uhakika wa Chakula na haki za Ardhi mkutano ulioandaliwa na Oxfam pamoja na Forum CC
Robert Muthami Program Support Officer kutoka Pan African Climate Justice Alliance (PACJA) akitoa ufafanuzi juu ya baadhi ya mambo yanayohusu mabadiliko ya Tabianchi.
 Meza  ya Majaji wakiwa wanasikiliza kwa makini malalamiko ya walalamikaji kutoka Loliondo juu ya kuchukuliwa ardhi pamoja na Malalamiko kutoka Wilaya ya Kishapu.
Kushoto ni mmoja wa walalamikaji kutoka Loliondo akielezea kwa uchungu jinsi Muwekezaji alivyo wanyang’anya Ardhi yao na mpaka sasa hakuna kitu ambacho kinaendelea na wanahitaji kupata Msaada wa kisheria ili wapate rudishiwa Ardhi yao.
 
 Kushoto ni Mama kutoka Loliondo akitoa malalamiko yake Mbele ya Mahakama ya wazi Jinsi mwekezaji alivyochukua Ardhi, kusababisha uharibifu na akina mama kuteseka pamoja na wengine kuharibu Mimba zao pia kupoteza watoto ambapo mpaka sasa kuna mtoto hajaonekana.
 Mlalamikaji Mwengine kutoka Loliondo akielezea Mbele ya Mahakama ya wazi  jinsi ya eneo lao lilivyochukulia na mwekezaji, na kutaka agizo la Mh. Waziri Mkuu lifanyiwe kazi la kwamba ardhi ile ni ya wafugaji na wanatakiwa warudishiwe
Mmoja wa walalamikaji kutoka Wilaya ya Kishapu akitoa malalamiko yake mbele ya Mahakama ya wazi juu ya walivyo chukuliwa maeneo kwa ahadi ya kuyaendeleza na kuto fanya hivyo, na kuomba eneo hilo ambalo ni mashamba warudishiwe ili waendelee na kilimo kwa kuwa eneo hilo kuna shida ya njaa.
Mchangiaji kutoka Oxfam Bwana Marc akizungumza juu ya haki za binadamu na moja ya haki hizo ni haki ya kila mwanadamu kuwa na Chakula, na kuongezea kuwa hata Umoja wa Mataifa unafahamu hilo Pia amesisitiza kuwa ni jukumu la kila mtu kujua sheria za umiliki wa Ardhi
Mjumbe wa Bodi kutoka Forum CC akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo
 
 Mmoja wa wachangiaji akizungumza Jambo
Mh. Jaji Richard Mzilay Akitoa Maelezo ya kina juu ya Walalamikaji kutoka Loliondo ambao walikuwa wana malalamiko ya Ardhi na Kishapu ambapo walikuwa wanataka Eneo lao lirudishwe, Ametoa maelekezo ya yale ambayo wanatakiwa wayafuate.
 
Washiriki wa Mkutano huo
 Mama Shujaa wa Chakula 2014 akichangia maada
 Burudani Elimisha ikiendelea
 Wadau wameguswa na kujumuika kucheza
 Picha ya pamoja

Tuesday, September 30, 2014

JAMII ITII SHERIA BILA SHURUTI.

Katika maisha ya kila siku, mwananchi anapaswa kutambua wajibu wake katika jamii ikiwa ni pamoja na kutii Sheria bila shuruti.
Katika maisha ya sasa nchini kumekuwa na vitendo vya ukiukwaji wa Sheria katika jamii na jamii imekuwa ikihusika katika matendo makubwa ya kijinai ambayo ni kinyume na sheria.
Hali hii imekuwa ikitokana na aidha jamii kutojua sheria, na muda mwingine ni kupuuzia tu maagizo na sheria mbalimbali.
Siku za hivi karibuni kumekuwepo na ukatili mkubwa ukitendeka katika jamii kwa kutokea kwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo wasiojua nini maana ya utu kwa makusudi wanakatiza uhai wa maisha ya binadamu wenzao na wengine kuwakata baadhi ya viungo vyao kwa tamaa ya kujipatia fedha pamoja na imani za kishirikina.
Jamii sio tu inaelewa kuwa kumdhuru mtu ni kosa la jinai bali pia jamii inatambua kuwa kuua pia ni kosa kubwa la jinai ambapo katika Sheria ya Kanuni ya adhabu Sura ya 16 kifungu cha 197 kimeeleza jinsi ambavyo kosa la kuua kwa kukusudia linamgharimu mtu adhabu ya kifo, lakini licha kuwepo kwa sheria hiyo, bado jamii inajihusisha na makosa ya kuua kila kukicha.
Katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria, suala la mauaji ya watu wenye Ualbino limekuwa ni tatizo kubwa kwani mauaji haya yanafanyika katika mazingira tu ya watu kuwa na imani potofu za kuukwaa utajiri wa haraka haraka.
Wakili wa kujitegemea Bwana Edwin Webiro anaeleza kuwa watu wengi wanafahamu kuwa kuua ni kosa kubwa lenye adhabu ya kifo ama kifungo cha maisha, bado watu hao hawajali juu ya uwepo wa Sheria ya kunyonga kwasababu wamekuwa wakiiona haitekelezwi ipasavyo, jambo linalowafanya wao waone ni haki kwao kufanya unyama wowote kwa watu wasio na hatia (watu wenye ulemavu).
Katika hali nyingine jamii pia imekuwa ikikiuka Sheria na kusababisha madhara makubwa pale ambapo ajari nyingi zimekuwa zikitokea mfululizo hivi karibuni na kusababisha vifo na kuacha ulemavu wa kudumu wa jamii.
Ajali hizi zimekuwa zikisababishwa na uzembe wa baadhi ya madereva wa mabasi pamoja na magari madogo kwani kumekuwa na ukiukwaji wa Sheria za barabarani ambapo kwa makusudi madereva hao wamekuwa wakikiuka sheria mbalimbali na kufanya mambo yanayosabisha ajari.
Sheria ya Usalama barabarani Sura ya 168 Kifungu cha 44 Inazuia mtu kuendesha chombo cha moto akiwa ametumia kilevi, lakini Sheria hii inajulikana vema kwa madereva lakini kwa makusudi hawaijali wala kuizingatia na badala yake wamekuwa wakitumia kilevi kabla ama wakati wakiwa wanaendesha vyombo vya moto.
Swali la kujiuliza ni kwamba, kwanini madereva wamekuwa wakitumia kilevi wakiwa wanaendesha magari?
Josephat Munishi ni Dereva wa daladala moja linalofanya safari zake Jijini Dar es Salaam anaeleza kuwa kutumia kilevi wakati wa kuendesha gari ni kosa kisheria.
“Muda mwingine kilevi kinakupa nguvu na kujihisi kutochoka na unapata hamasa ya kuendesha gari, kama unavyojua kazi yetu ni ngumu kutwa nzima unasumbuana na abiria, sasa bila kinywaji kidogo hauwezi pata nguvu ya kufanya kazi’’, alisema Munishi.
Jamii kwa mara nyingeine imekuwa ikikiuka Sheria na kujikuta katika maovu makubwa ambapo baadhi ya wasichana wamekuwa wakijihusisha na utoaji mimba (Abortion)kinyume na Sheria.
Kwa hali ilivyo sasa wasichana wadogo hasa wanafunzi na hata watu wazima wamekuwa wakijihusisha sana na utoaji mimba kinyume na sheria huku wengi wao wamekuwa ni wale ambao wamepata mimba hizo katika mazingira ambayo hawakutegema.
Watoto wengi wa kike wamekuwa wakijihusisha na mapenzi wakati bado wakiwa shule, na pindi wanapojigundua kuwa wana ujauzito njia pekee ambayo wanahisi ni bora kuepukana na matatizo hayo wamekuwa wakitoa mimba, kitu ambacho ni kinyume na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika kifungu cha 219 Cha Sheria ya Kanuni ya adhabu Sura ya 16, kinaeleza wazi kuwa kitendo cha kuharibu ujauzito ambao unapelekea kukatisha maisha ya mtoto ambaye angezaliwa, ni kosa la jinai lakini sababu kubwa ambayo wamekuwa wakiitoa wanawake wengi ni kuwa mimba hizo zinakuwa ni zile ambazo hazikupangwa kutokea (unplanned pregnancy).
Jamii inapaswa kuzingatia Sheria mbalimbali na iepuke kutoa sababu na visingizio za kutojua sheria hizo, kwani ni vema kutii sheria bila shuruti kama vyombo vyetu vya Usalama vinavyotutaka.

THE SECOND AFRICA GLOBAL BUSINESS FORUM WILL TAKE PLACE IN DUBAI ON 1st AND 2nd OOCTOBER 2014.

APO 
PRESS RELEASE
APO (African Press Organization) Invited As VIP Guest
 DUBAI, UAE, September 30, 2014/ — APO (African Press Organization) (www.apo-opa.com) has been invited as VIP Guest to attend the second Africa Global Business Forum (www.africaglobalbusinessforum.com), the region’s leading international trade and investment Forum on Africa, to take place at the Atlantis The Palm, Dubai on 1st and 2nd October 2014.
JU
Photo: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=782 (Nicolas Pompigne-Mognard, Founder and CEO of APO (African Press Organization)
 Organised by Dubai Chamber of Commerce and Industry with content developed by The Economist Events and under the patronage of H.H. Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, UAE Vice-President and Prime Minister and Ruler of Dubai, the forum will explore new business partnerships and opportunities arising between Africa and Dubai.
 The 2nd Africa Global Business Forum 2014 is by invitation only and will assemble high-level decision makers on the global business scene, including African Heads of State, Ministers, prominent CEOs operating globally, heads of private banks, sovereign wealth funds and private equity firms.
 International speakers include: H.E. Paul Kagame, President of Rwanda; H.E. Armando Guebuza, President of Republic of Mozambique; H.E. Amama Mbabazi, Prime Minister of Uganda; Donald Kaberuka, President, African Development Bank Group.
 Emirati speakers include H.H. Sheikh Ahmed Bin Saeed Al Maktoum, Chairman and CEO, Emirates Airline and Group; H.E. Reem Al Hashimy, UAE Minister of State and Managing Director, Dubai Expo 2020; H.E. Sultan Al Mansoori, UAE Minister of Economy ,H.E. Mohammed I. Al Shaibani, Executive Director and Chief Executive Officer of Investment Corporation of Dubai (ICD), H.E Sultan Ahmed Bin Sulayem, Chairman, DP and many more.
 In its strategy of expanding into the African continent, Dubai has become a major trading partner for the region as the emirate’s non-oil trade with the continent increased by 141%, up from AED 37.9 billion in 2008 to AED 91.3 billion ($25 billion) in 2013.
 According to a Dubai Chamber statistics, African companies operating in Dubai have seen a percentage growth of 171% from the period from 2008 to mid-2014.
 Contact:
Aïssatou Diallo
 About APO
 APO (African Press Organization) (http://www.apo-opa.com) is the sole press release newswire in Africa and is a global leader in media relations relating to Africa.
With offices in Senegal, Switzerland, Dubai, Hong Kong, India and Seychelles, APO owns a media database containing over 100,000 contacts and is the main online community for Africa-related news.
 It offers a complete range of services, including press release distribution and monitoring, online press conferences, interactive webcasts, media interactions, strategic advice, public diplomacy, government relations and events promotion. To find out more, please visit http://www.apo-opa.com.
 Follow us on Twitter: https://twitter.com/apo_source
 SOURCE 
APO (African Press Organization)

SAKATA LA MAKABURI LACHUKUWA SURA MPYA.

Mahmoud Ahmad Arusha
Sakata la kuhamisha makaburi lachukuwa sura mpya baada ya KAMATI ya kusimamia makaburi ya waislamu yaliyopo eneo la Levolosi jijini Arusha, kusisitiza kuwa haijafanya mazungumzo yeyote na halmashauri ya jiji la Arusha, kuhusu kufukuliwa kwa makaburi hayo yaliyopo eneo la Levolosi na badala yake kujengwa kituo kikubwa cha mabasi madogo yanayotoa huduma zake jijini Arusha na maeneo ya jirani, Daladala.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ustaadhi Omari Bokolo, akizungumza kwenye eneo la makaburi hayo amesema eneo hilo halijabadilishwa matumizi  na wala hawana mpango huo wa kubadili matumizi ya eneo hilo kwa sasa  .
Amesema kuwa eneo hilo la makaburi sio mali ya halmashauri ya jiji la Arusha kama ilivyodaiwa.bali eneo hilo linamilikiwa mtu binafsi ambae ni marehemu Said Sela Said tangia mwaka 1940, ambae kabla hajafariki aloilitoa wakfu kwa waislamu watakaokuwa wakifariki jijini Arusha  kuzikwa hapo .
Ustaadhi Bokolo, amesema kamati hiyo ya kusimamia makaburi ya waislamu katika jiji la Arusha, imeshutushwa na tamko la mkurugenzi wa jiji la Arusha Idd Juma, alilolitoa mwishoni mwa wiki kuwa tayari ameshazungumza na viongozi wa kiislamu na kukubaliana eneo hilo kubadilishwa matumizi kutoka makaburi na kujengwa  kituo cha daladala.
Amesema kamati inazo nyaraka zote za tangia mwaka 1940 hadi leo na kuutaka uongozi wa halmashauri ya jiji kurejea kwenye kumbu kumbu ili kuelewa umiliki halali wa eneo hilo .Amesema kuwa mwaka 2006 baada ya kutokea mgogoro wa  umiliki kutokana na mbinu chafu zilizofanywa na baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na baadhi ya madiwani, kamati hiyo ilimwandikia waziri wa Ardhi wakati huo, Dakta John Magufuli, ambae alithibitisha kuwa eneo hilo haikuwa mali ya halmashauri ya manispaa ya Arusha kwa wakati huo na kuitaka kamati hiyo kuliendeleza .
Ameongeza kuwa mwaka 2013 waziri wa Ardhi ,Profesa Anna Tibaijuka, katika mlolongo huo aliiagiza halmashauri ya jiji la Arusha kukaa  na kamati hiyo kutatua mgogoro huo lakini hilo halijawahi kufanyika  na badala yake halmashauri ya jiji inatangaza kubadilisha matumizi ya eneo hilo.
Wajumbe wa kamati hiyo wamehoji  uhalali wa halmashauri kumiliki eneo hilo sanjari na kushangazwa na hatua ya kutaka kujenga kituo cha daladala kati kati ya jiji badala ya huduma hiyo kujengwa maeneo ya pembezoni ambayo hayana msongamano na wakaitaka halmashauri kusitisha mara moja mpango huo vinginevyo wataiburuza mahakamani .
Mwishoni mwa wiki mkurugenzi wa jiji ,Idd Juma, amesema kuwa wanakusudia kubadili matumizi ya eneo hilo kutoka makaburi na kujengwa kituo cha daladala ili kuondoa msongamano  wa daladala katikati ya jiji la Arusha.

TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA GIZ.

GIZ - 1Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John akitoa tamko kuhusu  Siku ya Soko la Afya  iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la GIZ , itakayofanyika Oktoba 2 katika ukumbi wa Diammond Jubelee jijini Dar es salaam.
GIZ - 2Naibu Meneja wa Miradi ya Afya wa GIZ Bw. Christian Ptleiderer akizungumza na waandishi wa habari kutoa wito kwa mashirika mengine yanayotoa huduma za afya nchini kuendelea kusaidia na kusambaza huduma zao katika maeneo yenye changamoto ya miundombinu na uhaba wa watumishi wa afya.Kulia ni Mtaalam na Mawasiliano wa shirika la GIZ nchini Bi. Vida Mwasalla.
 
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
30/9/2014.Dar es salaa.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Shirika la Ujerumani la GIZ katika uanzishaji na uendelezaji wa programu mbalimbali za utoaji wa huduma za afya zinazolenga kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akitoa tamko kuhusu Siku ya Soko la Afya  nchini iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Ujerumani la GIZ  itakayofanyika Oktoba 2,  jijini Dar es salaam.
Amesema Tanzania na GIZ zimekuwa zikishirikiana katika uboreshaji wa miradi mbalimbali ya afya kwa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kuanzia ngazi ya taifa, mikoa na Halimashauri za wilaya.
Ameeleza kuwa mikoa ya Lindi, Mbeya, Mtwara na Tanga imeendelea kunufaika na miradi mbalimbali ya ushirikiano  chini ya shirika hilo inayolenga kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma za afya katika maeneo hayo, uimarishaji wa mifuko ya Afya ya Jamii na ushiriki wa moja kwa moja kusaidia upatikanaji na uendelezaji wa wataalam wa kutoa huduma za afya maeneo ya vijijini. 
Ameongeza kuwa GIZ imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika kuhakikisha kuwa jamii inamudu huduma bora za afya kupitia Mifuko ya Hifadhi ya Afya ya Jamii iliyopo katika maeneo yao.
Aidha, amebainisha kuwa maonyesho ya siku ya Soko la Afya yatakayowahusisha wadau mbalimbali na mashirika yanayotoa huduma za afya nchini yanalenga kuwakutanisha wadau hao ili waweze  kujadili changamoto za utoaji wa huduma za afya nchni, kujifunza mafanikio yaliyopatikana katika baadhi ya maeneo na kuweka mikakati ya kuyafikia maeneo mengi zaidi.
Kwa upande wake Mtaalam na Mawasiliano wa shirika la GIZ nchini Bi. Vida Mwasalla ameeleza kuwa maonesho ya mwaka huu yazilenga Wizara, Taasisi , Washirika wa Maendeleo, Makampuni, Mashirika binafsi  na Wakala zinazojihusisha na utoaji na uendelezaji wa sekta ya afya nchini.
Amesema katika maonesho hayo GIZ kwa kushirikiana na Wizara ya Afya itaonyesha mikakati mbalimbali ya kuwaokoa watoto wadogo wenye matatizo ya afya, namna walivyofanikiwa kuwapata watumishi wa afya katika maeneo ya Lindi na Mtwara, maeneo  ambayo hapo awali walikuwa hawakai katika vituo vyao.
Ameongeza kuwa mbali na Siku ya Soko la Afya kuhusisha huduma za utoaji wa elimu, vipimo, machapisho mbalimbali inalenga kuwaweka pamoja wadau hao ili waweze kubadilishana uzoefu na kuweka  mikakati ya kuchangia maendeleo ya sekta ya afya hapa nchini. 
Naye Naibu Meneja wa Miradi ya Afya wa GIZ Bw. Christian Ptleiderer ametoa wito kwa mashirika mengine yanayotoa huduma za afya nchini kuendelea kusaidia na kusambaza huduma zao katika maeneo ambayo bado yanakumbwa na changamoto mbalimbali za miundombinu na uhaba wa watumishi wa afya.
Amesema wao kama GIZ kwa kuanzia wameanza na mikoa 4, na wanaendelea kujenga uwezo wa kuyafikia maeneo mengi zaidi kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani na Tanzania.

INTRA-AFRICA TRADE KEY TO BOOSTING AFRICAN ECONOMIES-DHL.

PRESS RELEASE
XC
 The DHL Global Connectedness Index revealed that Africa is the world’s least connected continent
 CAPE-TOWN, South-Africa, September 30, 2014/ — While international trade agreements such as AGOA (African Growth and Opportunity Act) and the recently announced Economic Partnership Agreement between European Union and Southern Africa are positive for the continent and should be encouraged, more emphasis needs to be placed on trade partnerships between African countries to drive seamless intra-Africa trade.
DHL
 Photo Charles Brewer: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/photos/charles-brewer-1.jpg (Charles Brewer, Managing Director for DHL Express Sub-Saharan Africa)
 This is according to Charles Brewer, Managing Director of DHL Express Sub Saharan Africa (http://www.dpdhl.com), who says that while progress is slowly being made, insufficient trade agreements exist in order to encourage and drive intra-Africa trade. As a result there tends to be a focus on doing business with regions outside of Africa, such as the United States or China.
 He says that African countries desperately need to start trading amongst themselves, and that the push for trade agreements should therefore not only be with international trading partners, but amongst African countries too.
 “The DHL Global Connectedness Index revealed that Africa is the world’s least connected continent, when considering the ease of moving people, trade, information and finance.  All African countries should therefore be focused on developing connectedness on the continent and building trade relationships. From a DHL standpoint, we are focused on making logistics more accessible and connecting Africa, which has resulted in the expansion of our retail footprint to over 3300 outlets in less than 3 years,” adds Brewer.
 When comparing intra-regional trade statistics, Africa rates amongst the lowest, with less than 20%  of what is produced in the region staying within the region. This, in essence, means that over 80% of what is produced in Africa is exported, mainly to the EU, China and the US. By comparison, 60% of Europe’s trade is with its own continent, and in North America, the figure is 40%.
 As is well documented, one of the region’s biggest challenge in terms of realizing its trade potential is an under developed infrastructure, but Brewer says that this is slowly improving as several Africa regions continue to invest large amounts of capital into infrastructure development.
 “Under developed infrastructure directly impacts the speed at which goods are moved into, out of and across the region. It also drives up logistics costs, and it is estimated that supply chain costs are up to nine times more expensive in Africa in comparison to other regions in the world. These inflated costs also ultimately hamper economic growth in the region.”
 Brewer adds that while progress on infrastructure development and investment should continue, a push now needs to be made by African countries towards developing and implementing trade agreements which will encourage trade between the regions.
 “Angola is the only country in Africa that has a formal and declared de minimus, and whilst all other Sub Saharan Africa countries have informal agreements, the fiscal clearance levels vary greatly. For example, in Tanzania, anything with a value greater than USD 5 will require formal clearance, which creates an additional administrative burden and potential clearance delays with minimal returns for the government in terms of duty revenues.”
 “With that said, the situation is improving, and more countries are recognising that they need to find ways to make their markets accessible and easier to do business with. A great example for the region is Rwanda, who is looking to strip away bureaucracy, remove the red tape and make their country an attractive destination for trade and investment. More African countries need to follow this example, and the region will reap the rewards,” concludes Brewer.
 Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of Deutsche Post DHL.
 Media Contact:
Megan Collinicos. Head: Advertising & Public Relations, Sub-Saharan Africa
DHL Express
 DHL – The logistics company for the world
 DHL (http://www.dpdhl.com) is the global market leader in the logistics and transportation industry and “The logistics company for the world”. DHL commits its expertise in international express, national and international parcel delivery, air and ocean freight, road and rail transportation as well as contract and e-commerce related solutions along the entire supply chain. A global network composed of more than 220 countries and territories and around 315,000 employees worldwide offers customers superior service quality and local knowledge to satisfy their shipping and supply chain requirements. DHL accepts its social responsibility by supporting environmental protection, disaster management and education.
 DHL is part of Deutsche Post DHL. The Group generated revenues of more than 55 billion euros in 2013.
 For more information: www.dpdhl.com
 SOURCE 
Deutsche Post DHL.

UPIGAJI KURA WA RASIMU INAYOPENDEKEZWA WAENDELEA LEO BUNGENI MJINI DODOMA.

PICHA 1Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akipiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 2Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Hassan Suluhu akipiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 3Makamu wa Pili wa Zanzibar ambaye pia Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Seif Ali Idd akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 4Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Andrew Chenge akipiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 5Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati namba Tano ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Asha-Rose Migiro akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 6Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Fenella Mukangara akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 7 (2)Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Juma Nkamia akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
8Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Ummy Mwalimu akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
9Waziri wa TAMISEMI ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Hawa Ghasia akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
10Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Shymar Kwegir akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

WIZARA YA HABARI WAKATI WA MECHI ZAO SHIMIWI MOROGORO.

01Wachezaji wa timu ya m
pira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waki wa katika picha ya pamoja kabla ya mtanange dhidi ya RAS Simiyu leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.
02Waamuzi wa mchezo mpira wa miguu kati ya timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na RAS Simiyu wakiongozwa na mwamuzi wa kati Ramadhani Omari (wa pili kulia) wote kutoka kituo cha michezo ya vijana chini ya miaka 20 kijulikaanacho kama Twalipo cha mjini Morogoro.
03Mchezaji wa timu ya mpira wa pete Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Agnes Mbambo akimiliki mpira wakati wa mechi yao na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenye mashindano ya SHIMIWI leo mjini Morogoro.
04Wachezaji Johari Kachwamba (kulia) na Hadija Omari Jaa (kushoto) wakiwa kwenye harakati za kuwania mpira wakati wa mechi kati ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Timu ya Habari SHIMIWI yatoa kipigo kwa RAS Simiyu. Na Eleuteri Mangi-MAELEZO 29/09/2014 Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Watumishi wa Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mjini Morogoro. Wakicheza kwa kuonana timu hiyo ikiongozwa na Nahodha wao Carlos Mlinda walilisakama lango la wapinzani wao RAS Simiyu ambapo katika kipindi cha kwanza mcheza aliyevalia jezi yenye namba 11 Erick Mfugale aliwapatia goli la kuongoza kwa kipindi cha kwanza hadi mapumziko. Kipindi cha pili kilinza kwa timu zote kusaka ushindi ili kujihakikishia hatua inayofuata. Dakika ya saba ya kipindi cha pili mchezaji aliyevalia jezi namba 8 Maurus Ndenda ndiye aliwanyanyua mashabiki wa timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kufunga goli la pili kwa shuti kali na kuingia wavuni. Hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi wa mchezo huo Ramadhani Omari, timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeshinda 2 na RAS Simiyu hawajapata kitu ambapo ubao wa matokeo ulisomeka (Habari 2-Simiyu 0). Aidha kwa upande wa mpira wa pete timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo bahati haikuwa yao wamefungwa goli 39 kwa 10 na wapinzani wao Wizara ya Ardhi, Nyumba Na Maendeleo ya Makazi.

26 WAITWA TAIFA STARS KUIVAA BENIN

Wachezaji 26 wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa ajili mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam. 
Kocha Mart Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), amesema kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam. 
Wachezaji walioitwa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam). 
Mabeki ni Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon). 
Viungo ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna Chanongo (Simba). 
Washambuliaji ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia). 
BONIFACE WAMBURA
MKURUGENZI WA MASHINDANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

ONESHO LA S!TE KUFUNGULIWA LEO (KESHO JUMATANO) MLIMANI CITY

expo_011
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said vMeck Sadick (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es jana juu ya kufanyika kwa maonyesho ya utalii yanayoratibiwa na  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Picha: MPIGAPICHA WETU
Na Mwandishi Wetu
ONESHO la kimataifa la utalii ‘Swahili International Tourism Expo’ (SITE) linaloandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) linafunguliwa rasmi leo (kesho Jumatano) katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na litamalizika Jumamosi.
Tayari maandalizi yote kuelekea ufunguzi wa onesho hilo yamekamilika na kwamba watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuja kujionea vivutio adhimu wa taifa hili.
Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) pamoja na Shirika la Ndege la Ethiopia ndio wadhamini wa onesho hilo linalotarajiwa kushirikisha mataifa mbalimnali ulimwenguni.
Wadhamini wengine ni pamoja na Zanzibar collection, Hoteli za Sea Cliff, Serena hotel, Southern Sun,NewAfrica, Hyatt Regency,Protea, Serena hotel, Bouganvillea Safari lodge, Acacia Farm lodge na Soroi Tented Camp zimedhamini huduma ya malazi kwa wageni maalumu.
Pamoja na washiriki wengine onesho hilo linatarajiwa kushirikisha wafanya biashara wakubwa na watalii kutoka Marekani, Uingereza, Ujerumani pamoja na wandishi wa habari wa kimataifa wanaokuja kwa ajili ya onesho hilo.
Wakati Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ikitoa udhamini wa mabasi ya kubebea washiriki wakati wa onesho hilo, benki ya CRDB imetoa udhamini wa fedha taslimu na inatarajiwa kuwa na banda ndani ya maonesho hayo ya aina yake.
Usafiri wa ardhini  utadhaminiwa na makapuni Zara Tours, Naeda Safaris Ltd, Wildlife Expedition Safari, huku Azam Marine wakijitokeza kudhamini usafiri wa baharini kutoka Zanzibar. Mashirika ya ndege ya Rwandair, Precision Air na Uturuki (Turkish airline) yatatoa tiketi za ndege kwa ajili ya kuwasafirisha baadhi ya wageni wakati wa onesho hilo.
Makampuni mengine yaliyojitokeza ni yale yanayomiliki majarida. Haya ni Event, Dar Life na 7th Floor Media kutoka hapa nchini na Go Places kutoka Kenya, ambavyo wanatangaza onesho hili kupitia majarida yao.
Aidha kampuni ya Montage imetoa udhamini wa kuwa mpambaji katika kumbi za mikutano.Boogie woogie pia wametoa udhamini na watakuwa na mgahawa wao wa chakula katika banda la utalii wa utamaduni ilhali wadhamini wengine Black Tomato wao watakuwa na banda la kuuza kahawa ya Tanzania.
‘Swahili International Tourism Expo’ litakuwa likifanyika kila mwaka mnamo mwezi wa Oktoba na kuhudhuriwa na washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania.

KIKONGWE WA MIAKA 90 AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 30.09.2014.
  • KIKONGWE WA MIAKA 90 AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA
  • MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI CHA MCHANGA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
KIKONGWE MWENYE UMRI WA MIAKA 90 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BAPONDO NGAO MKAZI WA KIJIJI CHA UKWILE WILAYANI MBOZI ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA MNAMO TAREHE 29.09.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI UKWILE, KATA YA ISANDULA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, WATU HAO WALIMVIZIA MAREHEMU AKIWA AMELALA NDANI YA NYUMBA YAKE NA KISHA KUMVAMIA NA KUANZA KUMKATAKATA NA KUPELEKEA KIFO CHAKE.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO KUFAHAMIKA. MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA NA MAJERAHA MAKUBWA MAWILI YA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI. MAREHEMU ALIKUWA ANAISHI PEKE YAKE MAENEO YA MASHAMBANI UMBALI WA ZAIDI YA KILOMITA TANO [05] KUTOKA MAKAZI YA WATU.
HAKUNA MTU/WATU WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI, MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO ILI AZITOE MARA MOJA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA KATIKA SHULE YA MSINGI SANZYA WILAYA YA MOMBA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VALIUD SIAME@KIMUNDE (13) MKAZI WA KIJIJI CHA KAONGA ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI CHA MCHANGA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 29.09.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KAONGA, KATA YA CHILULUMO, TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, WAKATI TUKIO HILO LIKITOKEA MAREHEMU ALIKUWA NA WANAFUNZI WENZAKE WAKICHIMBA NA KUBEBA MCHANGA KWA AJILI YA UJENZI WA NYUMBA ZA KULALA WAALIMU SHULENI HAPO.
MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUTOA UANGALIZI WAKUTOSHA IKIWA NI PAMOJA NA KUWASIMAMIA WATOTO KATIKA SHUGHULI WANAZOWATUMA KUFANYA ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Ushirikiano wa Oman, Zanzibar utaendelea kukua

11 064 -2
Mhe. Said Ali Mbarouk akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Habari nchini Oman Sheikh Dk. abdulla  wakati  alipofanya mazungumzo katika ofisi yake tarehe 29 Septemba 2014 akiwa katika ziara rasmi ya siku nne kutembelea sekta mbali mbali za Utalii, Utamaduni na Michezo.
MUSCAT, OMAN        30/09/2014
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk ameuelezea ushirikiano baina ya Oman na Zanzibar kuwa daima utakuwepo na utaendelea kukua kutokana na kutanuka kwa maeneo mapya ya ushirikiano katika Nyanja mbali mbali za maendeleo.
Amesema ni jambo la faraja kuona kuwa hivi sasa Zanzibar na Oman zinatambua umuhimu wa kutanua maeneo hayo ya ushirikiano katika sekta za uchumi, utalii na michezo kwa lengo la  kuwanufaisha watu wa pande zote mbili.
Mhe. Saidi Ali Mbarouk ameyaeleza hayo katika nyakati tofauti wakati alipokuwa na mazungumzo na Mawaziri  wa sekta za Habari, Michezo, Utamaduni na Utalii mjini Muscat Oman leo, akiwa katika ziara yake ya siku nne ya kukutana na viongozi mbali mbali wa nchi hiyo kwa lengo la kukuza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Mapema akizungumza na Waziri wa Habari wa Oman, Sheikh Dk. Abdulla Monaim Bin Mansoor Al Husani, alitoa shukrani zake kwa Serikali ya Oman kwa misaada yake kwa Zanzibar na kusifu nidhamu   ya vyombo vya habari vya nchi hiyo katika kuwaunganisha watu na kuwawezesha kujenga uchumi imara.
Alisema hatua hii ya  mfano wa kuigwa inatokana na usimamizi  madhubuti  kwa vyombo vya habari na kujali kuwajibika kwa jamii kwa vile vinatoa nafasi ya kuwapatia taarifa za kutosha juu ya harakati za kujiendeleza na kujenga ustawi na maendeleo   yao.
Ameshauri haja ya kuwepo na utaratibu wa kubadilishana wataalamu na vipindi ili kila nchi iweze kujifunza kutoka upande mwengine kwa  kutambua maendeleo yanayofikiwa na kila upande na hivyo kutoa fursa za kuwawezesha vijana na vyombo vya habari kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yao kwa pamoja hasa kwa vile ni tegemeo kubwa la taifa katika kujenga uchumi.
Katika ziara yake hiyo ya siku nne, Mheshimiwa Saidi Ali Mbarouk pia alipata fursa ya kubadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Utamaduni na Mambo ya Kale, Sheikh Hamad Hilal Al Maamari na Waziri wa Michezo, Sheikh Shallal Saad Moh’d Al Saad na kutuwama zaidi katika masuala ya kubadilishana wataalamu wa michezo na kuyahuisha majengo ya kihistoria yenye mnasaba na Oman.
Wakati huo huo,  Mhe. Said Ali Mbarouk ameitaka Oman kufungua fursa nyengine kwa kuisaidia Zanzibar katika kuanzisha Hoteli za kitalii za Halal utaratibu ambao Oman tayari imeuanzisha na kupata mafanikio yake.
Amefahamisha kuwa utaratibu wa hoteli kama hizo za Halal ni muafaka katika visiwa vya Zanzibar kwa vile zitaongeza soko la idadi ya watalii wanaohitaji kupumzika katika maeneo yenye utulivu wa maadili ya kidini na kiutamaduni.
Katika ziara yake hiyo Waziri huyo wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo alipata fursa ya kushiriki katika  karamu rasmi iliyoandaliwa kwa ajili yake  na ujumbe  wa watu watatu aliyofuatana na Mwenyeji wake Waziri wa Habari wa Oman Sheikh Dk. Abdulla Monaim iliyofanyika katika jumba la serikali la Opera mjini Muscat.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI HABARI AMELEZO ZANZIBAR

Sunday, September 28, 2014

PSPF YADHAMINI MASHINDANO YA SHIMIWI YANAYOENDELEA MKOANI MOROGORO KATIKA UWANJA WA JAMUHURI.

Baadhi ya watu wakiwa wanafuatilia mashindano hayo ya SHIMIWI yanayo endelea Mjini Morogoro katika uwanja wa Jamuhuri 
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Netball wakiwa wanajiandaa na Mchezo wao
 Afisa wa PSPF akimsajili uanachama mmoja wa wanamichezo walikuwepo katika Mashindano hayo ya SHIMIWI
 Aliyevaa Tshirt ya Blue ni Afisa Masoko wa PSS Bwana Delphin Richard akitoa maelezo kwa wanachama wa PSPF wakati Michezo hiyo ikiendelea
Michezo ikiwa inaendelea 
 Baadhi ya wachezaji wakiwa katika mapumziko.