TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 2, 2015

WASANII KUTOKA TANZANIA WATUMBUIZA OMAN

Bondia wa kulipwa Farncis Cheka atupwa jela miaka mitatu, familia yapanga kukata rufaa

Na Ripota wetu, Morogoro
 
Bondi wa kulipwa nchini, Francis Cheka ambaye maarufu kwa jina la SMG, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milionai moja kwa kosa la kumpiga meneja waje wa baa, Bahati Kibanda.
 
Cheka alitiwa hatiani Julai 2 mwaka jana kwa kumpiga na kumsababishia maumivu makali Kibanda ambaye alikwenda hapo kudai fedha zake katika baa aliyokuwa anaifanyia kazi  ijulikanayo kwa jina la Vijana Social Hall.
 
Hakimu Mwanamizi wa mahakama ya mkoa wa Morogoro Said Msuya alikubaliana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kuthibitisha shitaka hilo.
 
Hakimu Msuya alisema kuwa adhabu hiyo ni fundisho kwa mshitakiwa na watu wengine wanaotumia vibaya nguvu zao kwa watu wengine na anatakiwa kumlipa mlalamikaji fidia ya Sh milioni moja.
 
Pamoja na Cheka kupewa nafasi ya kujitetea, bondia huyo hakutoa maelezo yoyote na kuiachia mahakama hiyo kutoa adhabu inayostahili kwa bondia huyo aliyejizolea sifa kemkem katika ngumi za kulipwa nchini.
 
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni, familia ya Cheka inampango wa kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali wameishukuru Serikali kutoa elimu ya Ujasiriamali

 Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Bibi Mariam A. Mtunguja (katikati) akizungumza na maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa ziara ya kutembelea vijana wa Mkoa wa Mbeya na kutoa elimu ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
 Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bw. Gullamhussein S. Kifu (katikati) wakati wa ziara ya kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa vijana wa Wilaya hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na anayefuata ni Kaimu Afisa Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Bw. Athuman Mustafa Kinza.

HOTUBA YA RAIS KIKWETE KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 38 YA KUZALIWA KWA CCM

HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KATIKA SHEREHE ZA KUTIMIZA MIAKA 38 YA CCM, KWENYE UWANJA WA MAJIMAJI, SONGEA - RUVUMA,
TAREHE 01 FEBRUARI, 2015
 
 Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akihutubia umati wa wananachi
Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM;
Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu na mjumbe wa Kamati Kuu;
Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge na Mjumbe wa Kamati Kuu;
Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM;
Ndugu Mike Mukula, Makamu Mwenyekiti wa NRM ya Uganda na ujumbe wake;
Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati Kuu;
Mheshimiwa Oddo Mwisho, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma;
Waheshimiwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa;
Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM;
Ndugu Verena Shumbusho, Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma;
Wenyeviti wa Jumuiya za CCM;
Viongozi, wananchama na wapenzi wa CCM;
CCM Oyee!

Benki ya CRDB na kampuni ya Bima ya Heritage zanyakua tuzo za BBLA 2014

 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Charles Kitwanga, (Kushoto) akimkabidhi tuzo mshindi wa Tuzo za Bodi yenye Uongozi Bora za 2014 (BBLA) katika sekta ya kibenki, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB Bw. Martin Mmari (kulia). Benki ya CRDB iliibuka mshindi katika sekta ya kibenki wakati kampuni ya Heritage Insurance iliibuka kinara katika sekta ya bima katika tuzo hizo zilizofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Charles Kitwanga, (Kushoto) akimkabidhi tuzo mshindi wa Tuzo za Bodi yenye Uongozi Bora za 2014 (BBLA) katika sekta ya bima, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni ya Heritage Insurance, Bw. Yogesh Manek (kulia). Heritage Insurance iliibuka mshindi katika sekta ya bima wakati Benki ya CRDB iliibuka kinara katika sekta ya kibenki katika tuzo hizo zilizofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI, ALI HASSAN MWINYI AZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI

 -Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) akiongozana na jaji mkuu wa Tanzania, Mohamed Othaman Chande  (watatu kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa kwanza kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Ally LILA  wakiwa katika matembezi ya kuadhimisha wiki ya sheria nchini matembezi hayo yalianzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam February 1, 2015.
 Bendi ya polisi ikiongoza matembezi ya wiki ya sheria nchini.

MH.HAMAD RASHID AWAASA WANAFUNZI KUJIUNGA NA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF ILI KUPATA MIKOPO YA ELIMU NA MIKOPO YA KUANZIA MAISHA

SIKU YA WAPENDANAO KIGAMBONI ITAKAVYOSHEREHESHWA NA WADADAZZZZZ

Watu mbali mbali mnakaribishwa kufika siku ya wapendanao huko kigamboni ambako kutakuwa na Mashindano ya kumpata mrembo wa siku hiyo kwa wale watakaoingia ukumbini na kisha kuchaguliwa kama Mrembo aliyevalia na kuweza kutokelezea zaidi ya wenzake(Miss Valentine Day) ambaye pamoja na ushindi wake atajipatia Donge Nono la Fedha Taslim kutoka kwa Waandaaji.

Wateja wa Airtel kushinda gari Moja Kila Siku Kupitia huduma ya Airtel Yatosha

Airtel Tanzania leo imezindua promosheni  kabambe ijulikanayo kama Airtel Yatosha Zaidi kwa wateja wanaotumia vifurushi vya Airtel Yatosha kuweza kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku
Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Masoko ya Airtel Bwana Levi Nyakundi alisema” promosheni hii ni nafasi ya peeke wa wateja wetu wanaojiunga na vifurshi vya Airtel yatosha vya siku, wiki na mwezi kupata faida zaidi kutokana pesa wanazozitumia.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano, (kulia) akifafanua jambo wakati wa Uzinduzi huo, kushoto ni Mkuu wa Masoko,Levi Nyakundi,  
 Hii ni promosheni ya aina yake ambapo wateja wetu wanazawadiwa kutokana na matumizi yao ya kawaida ya vifurushi vya Yatosha.  tunatoa wito kwa wale ambao hawajajiunga na vifurushi vya Airtel yatosha kufanya hivi na kupata nafasi ya kushinda gari moja kila siku”aliongeza  Mallya

FEDHA ZACHANGWA KWA AJILI YA FRANK KIBIKI ANAYETAKIWA KUCHUKUA FPOMI YA UBUNGE JIMBO LA IRINGA

Kibiki mwnye koti,akibadilishana mawazo na mmoja wa wanachama wa tujiwezeshe cha kituo kikuu cha mabasi mjini Iringa
Katibu wa kikundi cha tujiwezeshe chenye wanachama zaidi ya 560, wa
kituo kikuu cha mabasi mjini Iringa Manet Charles akizungumza baada ya kumkabidhi sh 110,000 mwanachama mwenzao Frank Kibiki, ambaye ni
mwanahabari baada ya kutangaza nia wa kuomba kuwania ubunge wa jimbo la Iringa mjini kupitia CCM.

KIJIJI CHA KILONDO SASA KUPATA UMEME

Huu ni mto  Makete  unaomwaga maji yake ziwa nyasa

TIGO KUWEKEZA DOLA MILLION 30 KANDA YA KASKAZINI MWAKA 2015

unnamedKaimu Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania Cecile Tiano(kulia) akiongea na waandishi wa habari Mkoani Arusha(hawapo pichani), wakati wa kutangaza kuongeza kwa uwekezaji wa dola za kimarekani milioni 30 kwa mikoa ya kanda ya Kaskazini mwishoni mwa wiki, kulia kwake ni Meneja Mkuu wa kanda hiyoDavid Charles.

Temeke mabingwa Wa Proin Women Taifa Cup mara baada ya kuifunga Pwani katika fainali

Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo, Mh Dkt Femella Mukangara (wa pili kushoto) akiwasili katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi wakati wa fainali ya Mashindano ya Proin Women Taifa Cup yaliyofikia Tamati leo kwa kuzikutanisha Timu za Temeke na Pwani.
Waziri wa habari utamaduni na Michezo, Mh Dkt Fenella Mukangara akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Temeke mara baada ya kuibuka washindi wa Mashindano ya Proin Women Taifa Cup ambayo yalichezwa katika Dimba la Azam huku Proin Promotions na Azam wakidhamini mashindano hayo.

VIJANA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KYELA WASHAURIWA KUTUMIA UJUZI KUJIAJIRI WENYEWE

1
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa wa pili kulia akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kyela Dr. Festo Dugange Januari 30,2015 wakati wa ziara ya kuhamasisha vijana wa Kyela. Wa kwanza kulia ni Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Amina Sanga, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na wa pili kushoto ni Afisa Vijana Mkoa wa Mbeya Bw. George Mbijima.
2
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akiwaelimisha vijana wa Wilaya ya Kyela kuhusu mwongozo unaosimamia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika katika Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya

Sunday, February 1, 2015

KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA MTWARA AFUNGA KIKAO KAZI CHA MAAFISA MA WASILIANO

1 2
Wawasilishaji kutokakampuniya PUSH OBSERVE Wakiwaelezea maafisa mawasiliano huduma wanazotoa ikiwa ufuatiliaji wa taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari na mitandao yakijamii pia utoaji wa taarifa wajumbe kupitia mitandao ya simu (Bulk messages)

MAMA NA MTOTO MPANGO WA SERIKALI KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI

3 Na Lorietha Laurence- Maelezo Dodoma
Serikali imeandaa mikakati mbalimbali ya kuboresha afya ya wanawake wajawazito ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Akijibu swali kwa Niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi, katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Dkt. Pindi Chana amesema moja ya mikakati hiyo ni mpango mkakati ulioboreshwa wa kuendeleza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi uliozinduliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete mwaka 2014. Alisema kuwa mpango huo unawashirikisha wadau mbalimbali ambao ni World Lung Foundation, Plan International, Care International, Jhpiego, UNFPA na GIZ wanaochangia katika kupanua vituo vya afya ,kujenga vyumba vya upasuaji na ununuzi wa vifaa na tiba. “Mkakati huu ni jitihada za serikali katika kuhakikisha afya ya mama na mtoto inaboreshwa kwa kukomesha vifo vitokanavyo na uzazi na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano” alisema Dkt. Chana. Alifafanua kuwa Rais Dkt Kikwete ameagiza wakuu wa mikoa kusimamia masuala ya afya kwa ngazi zote zinahusu afya ya mama na mtoto na kuhakikisha wanawasilisha taarifa za maendeleo ya utekelezaji kila baada ya miezi mitatu(3). Mpango mkakati huo umeanzishwa kutokana na bajeti finyu ya afya ya mama na mtoto ambayo imekuwa ikipungua kila mwaka wa fedha , hivyo serikali ikaona umuhimu wa kuangalia njia mbadala ya kuweze kupata fedha ili kuongeza bajeti.

BUNGE LAENDELEA NA VIKAO VYAKE MJINI DODOMA



1
2
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akijibu moja ya maswali yaliyoelekezwa kwenye wizara yake katika kipindi cha maswali na majibu Januari 30,2015  Bungeni mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akijibu swali  Bungeni mjini Dodoma.

MAGARI MAKUBWA YASOTA BARABARA KWENDA OLOLOSOKWAN .

DSC_0035
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyemtembelea ofisini kwake wakati wa ziara ya kikazi ya siku nne kwenye kijiji cha Ololosokwani na halmashauri ya Ngorongoro kwa ajili ya maandalizi ya mradi wa kijiji cha digitali unaoendeshwa na Unesco kwa kushirikiana na Ki-elektronic ya Samsung unaotarajiwa kuwasili kijijini hapo mwezi februari ukitokea jijini Dar.
DSC_0041
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) aliyeambatana na wataalamu wa elimu, afya na mawasiliano pamoja na Mratibu wa Taifa wa tiba asilia na mbadala katika Idara ya Tiba Wizara ya Afya na ustawi wa jamii. Dkt Liggy Vumilia (hayupo pichani) . Kutoka kushoto wa kwanza ni Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias, Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta pamoja na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph.

RAIS KIKWETE ALIPOTEMBELEA RAIS WA MALAWI ADDIS ABABA

1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika (kulia) wakikutana na marais wastaafu, Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini(Kushoto) na Joachim Chissano wa Msumbiji(wapili kushoto) wakati wa mkutano wa 24 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa Ethiopia leo
2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Malawi Professa Peter Mutharika jijini Addis Ababa Ethiopia leo.Viongozi hao wanahudhuria mkutano wa wakuu wa  nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.

SIKU YA SHERIA NCHINI ILIVYOSHIRIKISHA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA NHIF

1
Emmanuel Sarakyika wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akimpima shinikizo la damu mmoja wa watumishi wa Mahakama alipotembelea  kupata huduma hiyo katika banda la NHIF kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam ambapo Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini zitakazo fabika februari 04 2015 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Saalam.
2
Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF Bi Hawa Duguza akimpima urefu Bw. Ben Kigongola wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu katika banda la NHIF kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam.