TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, March 5, 2015

OLOLOSOKWAN WAFURAHIA UJIO WA KIJIJI CHA DIGITALI ENEO LAO

DSC_0003Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya Tehama, Al Amin Yusuph akiwasilisha mrejesho wa kazi ya kikundi chake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.(Picha na zote Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi Wetu
WAKAZI wa kijiji cha Ololosokwan wamesema kwamba ujio wa kijiji cha digitali katika kijiji chao ni neema kwao kwani kitawasaidia kukabiliana na changamoto kubwa za maisha zinazowakabili.
Kauli hiyo wameitoa mwishoni mwa wiki wakati wa kuhitimisha warsha ya siku saba ya kuangalia fursa na changamoto zitakazoambatana na mradi huo wa miaka mitatu unaodhaminiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwa kushirikiana na kampuni ya Ki-elektroniki ya Samsung.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake waliohudhuria warsha hiyo ambapo wataalamu mbalimbali wanaohusika na mradi huo walikutana kujadili changamoto na namna ya kukabiliana nazo, Salangat Mako, alisema kwamba tatizo la miundombinu, Afya na Elimu wanaamini litakabiliwa na mradi huo.
Alisema kuna shida kubwa ya elimu kutokana na mazingira yaliyopo ambapo wanafunzi wanalazimika kutembea kilomita 14 kwenda na kurudi shule hali inayodhoofisha ari ya kujifunza.
DSC_0044Mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta akitoa mrejesho wa kilichojadiliwa na kikundi chake.
Aidha alisema kwamba kuna changamoto katika zahanati yao yenye wauguzi wawili huku hospitali ya wilaya ikiwa kiasi cha kilomita 50 hali inayowafanya watu wengi kutegemea mitishamba katika matibabu mbalimbali pamoja na wanawake kusaidiwa uzazi na wakunga wa jadi.
Alisema kuwepo kwa mradi huo kutasaidia wanafunzi kuweza kujisomea kwa kutumia mfumo wa mtandao wa intaneti na hivyo kuwa katika nafasi ya kuelimika vyema kutambua wajibu wao na fursa zilizopo zinazowazunguka kwa kuwa hifadhini.
Aidha kuwepo kwa kiliniki ya mtandao kutaongeza ufanisi wa zahanati iliyopo pamoja na kuipa mkono katika tiba na kuondoa watu kutegemea tiba za asili.
Akizungumzia fursa za kiuchumi alisema ni matarajio yao kwamba kuwepo kwa kijiji hicho na utamaduni wake, kutawezesha kutumia vyema fursa za kitalii ili kukua kiuchumi kwa kujua mipango inayostahili katika kuendeleza utamaduni kwa jicho la kibiashara zaidi.
DSC_0036Mratibu wa shirika la IrikRAMAT Foundation, Salangat Mako akitoa mrejesho wa suluhu za changamoto mbalimbali za kikundi cha uchumi na utamaduni wakati wa kuhitimisha warsha hiyo ya wiki moja.
Naye Mganga mfawidhi wa zahanati ya Ololosokwan Obeid Laizer ambaye yupo katika kijiji hicho kwa miaka 15 amesema ana matumaini makubwa na mradi huo kwa kuwa mchanyato wake unaonekana kujali zaidi sosholojia za watu na afya zao hasa kwa kuwa na kliniki inayotembea na tiba kwa intaneti itakayomuwezesha kuwasiliana na madaktari wenzake ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya afya.
Alisema kwamba kijiji hicho kina magonjwa mengi japokuwa makubwa ni nyumonia, ukosefu wa damu, magonjwa ya zinaa, majereha ya wanyama kutokana na kuchunga mbugani na ugonjwa wa kuhara damu.
Alisema uwapo wa maabara utawasaidia kupata uhakika wa tiba kuliko sasa ambako wanafanya kwa kukisia zaidi.
DSC_0018Mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya afya kutoka UNESCO, Bw. Mathias Herman akiwasilisha mrejesho wa kikundi kazi chake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Naye Ofisa Ustawi wa jamii Ngorongoro Beneth Bwikizo amesema kwamba mradi huo utaleta mabadiliko makubwa kwa wanakijiji hapo kutokana na shughuli nyingi za hapo kuhusanishwa na mradi huo.
Alisema mradi huo ambao unaangalia zaidi kukabili utamaduni unaokwamisha maendeleo kwa kutoa elimu na kuiunganisha na dunia nyingine kwa mawasiliano unaonekana utafanya maisha ya wakazi wa hapo kuboreka.
Alisema mradi huo wa kwanza nchini Tanzania na watatu bara la Afrika umempa hamasa kubwa baada ya kuona unaangalia changamoto zilizopo Ololosokwan ambazo ni za miundombinu katika elimu, afya na uchumi na kuzifanyia kazi.
DSC_0051Ofisa Ustawi wa jamii Ngorongoro, Beneth Bwikizo akitoa neno la shukrani kwa niaba ya ujumbe wa kijijini cha Ololosokwan uliohudhuria warsha hiyo ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa juma wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
DSC_0054Afisa Miradi msaidizi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko (kushoto) na Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Teresia Irafay wakinakili yanayojiri wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji cha kidigital (Unesco – Samsung digital village) katika kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
DSC_0057Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la IrikRAMAT linalomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maoni yake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa wiki wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa mradi kijiji cha Kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Warsha hiyo ya wiki iliandaliwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini.
DSC_0066Pichani jii na chini ni wadau mbalimbali wa elimu, afya, Tehama na masuala ya utamaduni na uchumi waliohudhuria warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
DSC_0034
DSC_0008Kutoka kushoto ni Mathias Herman wa UNESCO, Mkurugenzi wa elimu ya msingi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Sarah Mlaki pamoja na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ololosokwan, Emmanuel Madeje.
DSC_0064Mkurugenzi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, akionesha kwa mifano baadhi ya bidhaa za nje zikivyokuwa na ubora kwenye vifungashio wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha digitali (Unesco-Samsung digital village) kwa wakazi wa kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
DSC_0118Mkurugenzi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisikiliza baadhi ya maboresho ya changamoto zilizojadiliwa na kikundi kazi cha sekta ya elimu na wadau mbalimbali wa elimu.
DSC_0070Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues akitoa maboresho ya kazi za vikundi vilivyokuwa vikijadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zilizopo katika kijiji cha Ololosokwan kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali.
DSC_0070Picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo ya wiki moja iliyomaziki mwishoni mwa juma wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

MAANDALIZI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO-MAAFISA NA ASKARI WA JESHI LA MAGEREZA

MAG1Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi ya kukimbia katika viunga vya manispaa ya Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro March 6, 2015. Maafisa hao wameweka kambi katika eneo la Gereza Karanga-Moshi.
MAG3Sehemu ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi makali katika mitaa ya mji wa Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi 6,2015. Katikati (mwenye vazi jeupe) ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Alexander Mmasy kutoka Makao Makuu ya Magereza, wa kwanza kulia ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza Mbezi Ramadhani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga na wa kwanza kushoto ni Mkaguzi wa Magereza Jamhuri Yassin kutoka Makao Makuu ya Magereza, Dar es salaam.
MAG4Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi ya kutembea katika viunga vya Manispaa ya Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro mnamo Machi 6, 2015. Kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Magereza Vicent Magessa kutoka Gereza Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Mkaguzi wa Magereza Tumaini Kihampa na Mkaguzi wa Magereza Jamhuri Yassin wote kutoka Makao Makuu ya Magereza.
MAG5Maafisa na Askari na baadhi wa watumishi raia wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi makali ya kupita katika njia ngumu ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi 6, 2015. Wa sita kutoka mbele ni Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Magereza Estomiah Hamis na wa mwisho ni Mkaguzi wa Magereza Abas Mikidadi.
MAG6Maafisa na Askari na baadhi wa watumishi raia wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi makali ya kupita katika njia ngumu ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi 6, 2015.
MAG7Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi ya viungo baada ya kutembea na kukimbia katika viunga vya Manispaa MAG8Wakipata chakula MAG9Wakipiga picha ya pamoja na baadhi ya watalii.

BONDIA OMARI KIMWERI AMPIGA TAFU YA VIFAA KOCHA SUPER D

Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania. kushoto akimkabidhi glove kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ katikati ni bondia Mtanzania anayefanya kazi zake nchiniAustralia, Omari Kimweri ambaye aliongozana nchini na mwanasoka huyo muda mfupi kabla awajapanda ndege kurudi kwao Picha na SUPER D.
………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Mtanzania Omari Kimweri anaefanya shughuli zake za mchezo wa masumbwi nchini Australia amempiga tafu ya vifaa vya kufundishia kocha wa kimataifa wa mchechezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ wakati wa zihara yake ya wiki mbili ya kutembelea nyumbani kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu zitumiwazo na mabondia wa nje kabla ya hapo bondia huyo aliongea na wadau mbalimbali wa masumbwi wakati wa mchezo wa ngumi za kulipwa kati ya Iddi Bonge na Alphonce Mchumiatumbo mpambano uliofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba na kumvalisha mkata wa ubingwa bondia wa uzito wa juu Mchumiatumbo baada ya kuibuka na ushindi wa K,O ya raundi ya kwanza siku hiyo pia alimpiga tafu kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kwa kumkabidhi vifaa vipya vya kufundishia mchezo wa masumbwi Akizungumza baada ya kumkabidhi vifaa kocha Super D alisema amekumbuka nyumbani kwa kuwa ndio alipo zaliwa na kitovu chake kimezikiwa hapa nchini hivyo ataendelea kuwakumbuka zaidi kwa kuwawezesha mabondia kucheza mara kwa mara pindi atakapoanzisha Kimweri Promotioon itakayoshilikiana na Super D Boxing Coach And Promotion kwa kushilikiana kuwapatia mabondia kupigana ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kujiongezea kipato pamoja na kupandishe rekodi zao kwa mabondia chipkizi nae kocha Super D alishukulu kwa kukabidhiwa vifaa hivyo ambavyo vitamsaidia kuendelea kuinua mabondia mbalimbali chipkizi

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWASILI DODOMA NA KUANZA ZIARA WILAYA YA MPWAPWA


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea mkoani Ruvuma ambako alihudhuria mazishi ya Kada wa CCM na Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi Marehemu John Damiano Komba aliyefariki hivi karibuni, Chama cha Mapinduzi kilikuwa na maombolezo ya kitaifa ya siku tatu mpaka mazishi ya kiongozi huyo yalipofanyika jana yakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete.
Ndugu Abdulrahman Kinana ameanza ziara ya siku 9 mkoani Dodoma  akianzia wilaya ya Mpwapwa kabla ya kuendelea na ziara hiyo katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DODOMA-MPWAPWA) 2Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Ndugu Adam Kimbisa kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara Ndugu Mwigulu Nchema. 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanaCCM na wananchi waliofika kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma. 5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto akiongozana na viongozi wenzake mara baada ya kuwasili mjini Dodoma kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Kapteni Chiku Galawa, Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, na Adam Kimbisa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma. 7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu na vijana wa chipukizi mara baada ya kuwasili mjini Mpwapwa ambako ndiko ameanzia ziara yake. 8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Dr. Jasmine  Tisekwa. 10Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Mpwapwa katika ofisi ya CCM wilaya ya Mpwapwa kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma. 11Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati alipokuwa akisalimia wananchi mjini Mpwapwa, kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma.

Bayport yazindua tawi la Kwimba mkoani Mwanza


Na Mwandishi Wetu, Kwimba
TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo imepongezwa na serikali kwa hatua yake ya kufungua tawi wilayani
Kwimba mkoani Mwanza.
 Meneja Mauzo
wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano
Kasambala, akimuelekeza jambo Katibu Tawala wa Wilaya Kwimba, Vicent Emmanuel,
katika uzinduzi wa tawi jipya wilayani humo, uliofanyika Machi 2 mwaka huu.
Wengine ni maofisa wa taasisi hiyo, Ramadhan Hanafi na Monica Mwangoka. Picha
na Mpigapicha Wetu.
 
Shughuli za
uzinduzi huo zilifanyika Machi 2 mwaka huu, huku mgeni rasmi akiwa ni Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kwimba, Vicent Emmanuel, akiongozana na viongozi mbalimbali
wa serikali wilayani humo.
Katibu
Tawala wa wilaya ya Kwimba, Vicent Emmanuel, kushoto akikata utepe kuashiria
kuzindua rasmi tawi jipya la taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services,
wilayani Kwimba, mkoani Mwanza. Kulia ni Meneja Mauzo wa taasisi hiyo Kanda ya
Ziwa, Lugano Kasambala. Picha na Mpigapicha Wetu.

Mradi wa Kinyerezi 1 kukamilika mwezi Juni; Wafikia asilimia 80 ya ukamilishwaji wake; Watumia Dola Milioni 167. 2 hadi sasa

KA1 
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wanja Mtawazo ( kulia) akisalimiana na Mbunge wa Lulindi- Masasi, Jerome Bwanausi ( kushoto) ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini mara baada ya kamati hiyo kuwasili katika eneo la mtambo wa kufua umeme wa Kinyerezi I. Kamati hiyo inafanya ziara katika miradi ya umeme katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Singida, Arusha na Kilimanjaro pamoja na kuzungumza na wadau wa madini ya tanzanite katika mkoa wa Manyara ili kujionea maendeleo ya sekta hizo.
KA2Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga (kulia) akimsikiliza kwa makini Meneja Mradi Mkazi wa Kampuni ya Yakobsen Elektro ya Norway inayojenga mtambo wa Kinyerezi I Markkli Repo ( wa pili kutoka kushoto) mara baada ya kuwasili katika eneo la mtambo huo ili aweze kuwaongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwenye ziara katika mitambo hiyo.
KA3Meneja Miradi ya Kinyerezi Mhandisi Simon Jilima (kulia) akielezea maendeleo ya ujezi wa mtambo wa Kinyerezi I mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga (wa tano kutoka kulia), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
KA4Mbunge wa Lulindi- Masasi, Jerome Bwanausi (katikati) akisisitiza jambo katika ziara hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga na kulia ni Meneja Miradi ya Kinyerezi Mhandisi Simon Jilima
KA5Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Felchesmi Mramba akielezea mikakati ya shirika la Tanesco kuboresha huduma za umeme nchini kote.
……………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam Meneja Miradi ya Kinyerezi Mhandisi Simon Jilima amesema kuwa mtambo wa Kinyerezi 1 unaojengwa na kampuni ya Yakobsen Elektro ya Norway unatarajia kukamilika mapema Juni mwaka huu. Mhandisi Jilima aliyasema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanya ziara katika mtambo huo ili kujionea maendeleo ya ujenzi wake. Kamati hiyo imeanza ziara ya kutembelea miradi ya umeme iliyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Singida, Arusha na Kilimanjaro pamoja na kuzungumza na wadau wa madini aina ya tanzanite katika mkoa wa Manyara. Mhandisi Jilima alisema kwa sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 80 na kufafanua kazi inayofanyika kwa sasa ni kumalizia utandazaji wa nyaya, ufungaji wa mabomba ya maji na gesi pamoja na ujenzi wa barabara za ndani. Alisema kuwa ofisi kwa ajili ya watumishi pamoja na karakana kwa ajili ya kuhifadhia mitambo imekamilika. Akielezea gharama za mradi huo Mhandisi Jilima alisema mpaka sasa serikali imelipa kiasi cha Dola za Marekani milioni 167.2 na kuongeza kuwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 15 kinatarajiwa kumaliziwa kabla ya kukamilika kwa mradi. Akielezea changamoto katika utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi Jilima alieleza kuwa awali changamoto kubwa ilikuwa ni ukamilishwaji wa mradi wa bomba la gesi ili waweze kutumia gesi hiyo katika kuzalisha umeme lakini kutokana na kasi ya mradi huo kuwa ya kuridhisha wana imani kuwa gesi itaanza kuzalishwa mapema kabla ya kukamilika kwa mtambo wa Kinyerezi 1 “ Ndugu wajumbe, awali tulikuwa na wasiwasi wa kupatikana kwa gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme kupitia mradi wa Kinyerezi 1 kutokana na mradi wa bomba la gesi kuwa na changamoto nyingi, lakini baada ya kuona mradi wa bomba la gesi uko katika hatua nzuri yaani zaidi ya asilimia 90, tunaamini kuwa mara mtambo utapokamilika, gesi itakuwa imekwishaanza kuzalishwa na hapo ndipo tutaanza kuzalisha umeme mara moja,” alieleza Mhandisi Jilima Akielezea fidia kwa wakazi waliopisha ujenzi wa mradi huo, Mhandisi Jilima alieleza kuwa mradi wa Kinyerezi I ulikwishafanya tahmini pamoja na kulipa fidia kwa wakazi waliopisha ujenzi wa mtambo huo tangu mwaka juzi. Wakati huohuo wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini walipongeza hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mtambo huo na kuitaka serikali kukamilisha malipo ya kiasi kilichobaki cha Dola za Marekani milioni 15 ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.

WAFANYAKAZI WA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR WAPEWA MAFUNZO JINSI YA KUKABILIANA NA UGONJWA WA EBOLA.

za1 Mshauri wa mambo ya Afya kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) Dk. Andemichael Ghirmay akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta ya Afya Zanzibar kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, mafunzo hayo ya siku tatu yanafanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort na yamezaminiwa na WHO. za2Mgeni rasmin Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mohammed Jidawi akifungua mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta ya Afya Zanzibar kukabiliana na ugonjwa wa Ebola. za3  Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mgeni rasmin Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mohammed Jidawi (hayupo pichani) wakati alipokua akifungua mafunzo hayo huko Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mjini Ungujaza5Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mgeni rasmin Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mohammed Jidawi (hayupo pichani) wakati alipokua akifungua mafunzo hayo huko Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mjini Unguja
za6    Mmoja wawakufunzi kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) anaefanyia kazi Tanzania Dk. Grace Saguti akifafanua jambo alipokuwa akiwasilisha mada yake.
za7Mgeni rasmin Dkt. Jidawi katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola yanayofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

RAIS KIKWETE AUNGANA NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUMZIKA KEPTENI JOHN DAMIANO KOMBA KIJIJINI LITUHI LEO

ko1Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa ,Mkoani Ruvuma. ko2Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa ,Mkoani Ruvuma. ko3Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Mbinga Mhashamu John Ndimbo akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma leo(picha na Freddy Maro)
………………………………………………………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Machi 3, 2015, ameungana na mamia ya waombolezaji kumzika Mbunge wa Jimbo la Nyasa na msanii mahiri wa muziki nchini, Mheshimiwa Kepteni John Damiano Komba, kwenye makaburi ya Kanisa Katoliki katika Kijiji cha Lituhi, Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma. Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea, akitokea Dar es Salaam, kiasi cha saa tano na robo asubuhi, Rais Kikwete amekwenda moja kwa moja Lituhi, karibu kiasi cha kilomita 140 kutoka mjini Songea, kwa ajili ya mazishi ya Mheshimiwa Komba ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Rais Kikwete amejiunga na waombolezaji akiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda kiasi cha saa tisa mchana kwa ajili ya mazishi ya mmoja wa wasanii ambao walijijengea heshima kubwa kwa nyimbo zake za uhamasishaji. Wakati wa shughuli za mazishi ambazo kidini zimeongozwa na Askofu John Ndimbo wa Jimbo Katoliki Mbinga, waombolezaji walisomewa salamu za rambirambi ambazo zimetumwa na Rais wa Pili wa Malawi, Mheshimiwa Bakili Muluzi ambaye sasa amestaafu. Katika salamu hizo, Mheshimiwa Muluzi amesema: “Nilimjua Komba kama rafiki na taarifa za kifo chake cha ghafla zimenistua sana.” Mwili wa Marehemu Komba uliteremshwa kaburini saa 9:30 mchana huku ukishuhudiwa na mjane wa marehemu Salome Komba na watoto wake 11. Rais Kikwete ameondoka Lituhi mara baada ya mazishi kurejea mjini Songea kumalizia ziara yake ya siku mbili ya kikazi mkoani Ruvuma.
Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM.
3 Machi, 2015

Live Band – Every Wednesday At City Lounge

New Picture (106)UNATAKA KUEPUKA NA BUGUDHA YA KUKAA KWENYE FOLENI KWA MASAA MAWILI? KARIBU “CITY LOUNGE” UPUMZISHE AKILI NA
” THE BACKYARD BAND “. KILA JUMATANO KUANZIA SAA 11.00 JIONI

MAKONDA KUKUTANA NA WANANCHI WA KINONDONI WENYE MIGOGORO YA ARDHI KILA IJUMAA

*AUNDA KAMATI YA KUSHUSHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARDHI KINONDONI

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema kuwa wilaya ya Kinondoni inakabiliwa na changamoto migogoro ya ardhi ambayo inatakiwa kila mtu ambaye amenyimwa haki ya ardhi watapata kutokana na utaratibu uliopo.

Makonda aliyasema hayo hivi karibuni wakati ziara ya kutembelea wilaya hiyo, Makonda alisema asili ya migogoro hii inatokana hasa na mgongano wa uhalali wa umiliki pamoja na uvamizi wa maeneo ya wazi yaliyotengwa maalumu kwa shughuli za jamii ni changamoto ya muda mrefu na natambua juhudi nyingi zilizofanyika katika kutatua.

Makonda alisema moja ya mkakati wangu ni kufanya utatuzi unaohusisha taasisi zote muhimu ili kufupisha mlolongo unaowapotezea muda walioko kwenye migogoro na kuhakikisha mwenye haki anapewa haki yake bila kuyumbishwa.

Alisema anatenga siku moja ambayo ni ya Ijumaa kuwa siku maalumu ya kukutana na wananchi na kusikiliza matatizo yanayohusiana na Ardhi na utaratibu huu utaanza machi 6 mwaka huu na zoezi la uandikishaji kwa wale wanaohitaji kusikilizwa matatizo yao utaanza majira ya saa 3.

Makonda alisema Ili kupata ufumbuzi usio na shaka kamati ndogo itakayohusika katika kushughulikia matatizo hayo itaundwa na Katibu tawala wilaya (DAS) akiwa ni katibu, Mwanasheria wa Manispaa, Afisa Mipango miji, Afisa Ardhi.

Aidha alisema ili kufanya zoezi hili liwe na ufanisi na mafanikio ningeomba wananchi wafuate utaratibu kuanzia ngazi za watendaji wa chini kabla ya kufikisha kila muhusika ahakikishe amekuja na vielelezo vyote halali vinavyoweza kutumika katika kufikia uamuzi.

http://shaabanmpalule.blogspot.com/

Ni wakati wa furaha na kuonyesha Upendo kwa Taifa Lako, Piga vita Rushwa ni Adui wa Haki na Mpiga Maendeleo kwa Taifa, tumia Uhuru wako katika kusema na kufichua Maovu, Mwaka 2015 Chagua Kiongozi asiyetumia Rushwa na Mwadilifu katika Mawazo, Maamuzi, Vitendo na Uwajibikaji kwa Wananchi.