Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye ndege mara baada
ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea mkoani Ruvuma
ambako alihudhuria mazishi ya Kada wa CCM na Mbunge wa jimbo la Mbinga
Magharibi Marehemu John Damiano Komba aliyefariki hivi karibuni, Chama
cha Mapinduzi kilikuwa na maombolezo ya kitaifa ya siku tatu mpaka
mazishi ya kiongozi huyo yalipofanyika jana yakiongozwa na Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete.
Ndugu
Abdulrahman Kinana ameanza ziara ya siku 9 mkoani Dodoma akianzia
wilaya ya Mpwapwa kabla ya kuendelea na ziara hiyo katika mikoa ya
Arusha na Kilimanjaro, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-DODOMA-MPWAPWA) Nape
Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM akisalimiana na Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Dodoma Ndugu Adam Kimbisa kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM
bara Ndugu Mwigulu Nchema. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanaCCM na wananchi waliofika kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma. Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto akiongozana na viongozi
wenzake mara baada ya kuwasili mjini Dodoma kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa
wa Dodoma Kapteni Chiku Galawa, Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi, na Adam Kimbisa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu na vijana wa chipukizi mara baada ya kuwasili mjini Mpwapwa ambako ndiko ameanzia ziara yake. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Dr. Jasmine Tisekwa. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza
na wananchi wa Mpwapwa katika ofisi ya CCM wilaya ya Mpwapwa kulia ni
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na katikati ni Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Dodoma. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati alipokuwa akisalimia
wananchi mjini Mpwapwa, kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment