…………………………………………………………………..
Na: Geofrey Tengeneza – Berlin Ujerumani
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu amekutana
na waziri mwenzake wa Biashara na Utaliiwa Kenya Bibi Phylis Kandie
katika banda la Kenya na kuwa na mazungumzo yanayohusu ushirikiano wa
nchi mbili katika sekta ya Utalii. Mazungumzo hayo hayakuwa rasmi hivyo
hayakuhudhuriwa na wandishi wa habari
Aidha Wiziri Nyalandu alitembelea banda la Tanzania na
kuzungumza na washiriki wa maonesho ya ITB kutoka makampuni mbalimbali
washiriki hao kwa ambapo amewapongeza kwa kuitangaza vema Tanzania
katika maonesho hayo.
No comments:
Post a Comment