Tume
ya Taifa ya Uchaguzi imeanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura baada ya kukamilika kwa maandalizi muhimu ya
Uboreshaji wa Daftari, ikiwemo manunuzi ya vifaa na upatikanaji wa fedha
kutoka Serikalini.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, tofauti
na Uboreshaji wa Daftari hilo kwa Awamu zote za Chaguzi zilizopita,
linafanyika kwa kutumia teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration
(BVR). Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilianza
kufanyika katika Kata tisa (9) za Halmashauri ya Mji wa Makambako katika
Vituo 54 vilivyowekwa katika Mitaa na Vitongoji, kuanzia tarehe
23/2/2015 katika Kata za Kitisi, Kivavi, Lyamkena, Maguvani, Majengo,
Makambako, Mji Mwema, Mlowa na Mwembetogwa.
Tume ililenga kuandikisha Wapiga Kura 32,370 kwa mujibu wa
taarifa za Ofisi ya Takwimu za Sensa ya Idadi ya watu ya mwaka 2012.
Tume ililenga kuandikisha kwa siku jumla ya watu 1,850. Hata hivyo mara
baada ya uandikishaji kuanza idadi ya Wapiga Kura waliokuwa wanajitokeza
iliendelea kuwa kubwa na kuongezeka kila siku ambapo kulikuwa na
misururu mirefu ya watu waliojitokeza kujiandisha katika Vituo vyote vya
Uandikishaji. Tume ilivuka malengo yaliyowekwa ya Uandikishaji kutokana
na kujitokeza kwa wingi kwa Wapiga Kura waliofika katika Vituo vya
Uandikishaji kila siku kwa Kata zote tisa (9) za Mji wa Makambako ambazo
zilikuwa zinaandikisha Wapiga Kura.
Idadi ya Wapiga Kura waliojitokeza na kuandikishwa kwa kila siku
katika Kata tisa (9) za Mji wa Makambako ilikuwa kama ifuatavyo:-
i. Tarehe 23/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 3,014;
ii. Tarehe 24/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 4,727;
iii. Tarehe 25/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 5,301;
iv. Tarehe 26/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 6,354;
v. Tarehe 27/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 6,731;
vi. Tarehe 28/2/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 6,545;
vii. Tarehe 1/3/2015 Tume iliandikisha Wapiga Kura 6,906;
viii. Tarehe 2/3/2015 kutokana na Watu waliokuwa wanajitokeza
kujiandikisha kuendelea kupungua, Tume iliandikisha Wapiga Kura 4,662;
na
No comments:
Post a Comment