Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, ambaye pia alikuwa
mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya Tehama, Al Amin Yusuph
akiwasilisha mrejesho wa kazi ya kikundi chake wakati wa kuhitimisha
warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa mradi
wa kijiji cha kidigitali Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani
Arusha.(Picha na zote Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi Wetu
WAKAZI
wa kijiji cha Ololosokwan wamesema kwamba ujio wa kijiji cha digitali
katika kijiji chao ni neema kwao kwani kitawasaidia kukabiliana na
changamoto kubwa za maisha zinazowakabili.
Kauli
hiyo wameitoa mwishoni mwa wiki wakati wa kuhitimisha warsha ya siku
saba ya kuangalia fursa na changamoto zitakazoambatana na mradi huo wa
miaka mitatu unaodhaminiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la
Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwa kushirikiana na kampuni ya Ki-elektroniki
ya Samsung.
Akizungumza
kwa niaba ya wananchi wenzake waliohudhuria warsha hiyo ambapo
wataalamu mbalimbali wanaohusika na mradi huo walikutana kujadili
changamoto na namna ya kukabiliana nazo, Salangat Mako, alisema kwamba
tatizo la miundombinu, Afya na Elimu wanaamini litakabiliwa na mradi
huo.
Alisema
kuna shida kubwa ya elimu kutokana na mazingira yaliyopo ambapo
wanafunzi wanalazimika kutembea kilomita 14 kwenda na kurudi shule hali
inayodhoofisha ari ya kujifunza.
Mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta akitoa mrejesho wa kilichojadiliwa na kikundi chake.
Aidha
alisema kwamba kuna changamoto katika zahanati yao yenye wauguzi wawili
huku hospitali ya wilaya ikiwa kiasi cha kilomita 50 hali inayowafanya
watu wengi kutegemea mitishamba katika matibabu mbalimbali pamoja na
wanawake kusaidiwa uzazi na wakunga wa jadi.
Alisema
kuwepo kwa mradi huo kutasaidia wanafunzi kuweza kujisomea kwa kutumia
mfumo wa mtandao wa intaneti na hivyo kuwa katika nafasi ya kuelimika
vyema kutambua wajibu wao na fursa zilizopo zinazowazunguka kwa kuwa
hifadhini.
Aidha
kuwepo kwa kiliniki ya mtandao kutaongeza ufanisi wa zahanati iliyopo
pamoja na kuipa mkono katika tiba na kuondoa watu kutegemea tiba za
asili.
Akizungumzia
fursa za kiuchumi alisema ni matarajio yao kwamba kuwepo kwa kijiji
hicho na utamaduni wake, kutawezesha kutumia vyema fursa za kitalii ili
kukua kiuchumi kwa kujua mipango inayostahili katika kuendeleza
utamaduni kwa jicho la kibiashara zaidi.
Mratibu
wa shirika la IrikRAMAT Foundation, Salangat Mako akitoa mrejesho wa
suluhu za changamoto mbalimbali za kikundi cha uchumi na utamaduni
wakati wa kuhitimisha warsha hiyo ya wiki moja.
Naye
Mganga mfawidhi wa zahanati ya Ololosokwan Obeid Laizer ambaye yupo
katika kijiji hicho kwa miaka 15 amesema ana matumaini makubwa na mradi
huo kwa kuwa mchanyato wake unaonekana kujali zaidi sosholojia za watu
na afya zao hasa kwa kuwa na kliniki inayotembea na tiba kwa intaneti
itakayomuwezesha kuwasiliana na madaktari wenzake ili kupata ufumbuzi wa
matatizo ya afya.
Alisema
kwamba kijiji hicho kina magonjwa mengi japokuwa makubwa ni nyumonia,
ukosefu wa damu, magonjwa ya zinaa, majereha ya wanyama kutokana na
kuchunga mbugani na ugonjwa wa kuhara damu.
Alisema uwapo wa maabara utawasaidia kupata uhakika wa tiba kuliko sasa ambako wanafanya kwa kukisia zaidi.
Mwenyekiti
wa kikundi kazi cha sekta ya afya kutoka UNESCO, Bw. Mathias Herman
akiwasilisha mrejesho wa kikundi kazi chake wakati wa kuhitimisha warsha
ya wiki moja ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha
kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) cha Ololosokwan wilayani
Ngorongoro mkoani Arusha.
Naye
Ofisa Ustawi wa jamii Ngorongoro Beneth Bwikizo amesema kwamba mradi huo
utaleta mabadiliko makubwa kwa wanakijiji hapo kutokana na shughuli
nyingi za hapo kuhusanishwa na mradi huo.
Alisema
mradi huo ambao unaangalia zaidi kukabili utamaduni unaokwamisha
maendeleo kwa kutoa elimu na kuiunganisha na dunia nyingine kwa
mawasiliano unaonekana utafanya maisha ya wakazi wa hapo kuboreka.
Alisema
mradi huo wa kwanza nchini Tanzania na watatu bara la Afrika umempa
hamasa kubwa baada ya kuona unaangalia changamoto zilizopo Ololosokwan
ambazo ni za miundombinu katika elimu, afya na uchumi na kuzifanyia
kazi.
Ofisa
Ustawi wa jamii Ngorongoro, Beneth Bwikizo akitoa neno la shukrani kwa
niaba ya ujumbe wa kijijini cha Ololosokwan uliohudhuria warsha hiyo ya
wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa juma wilayani Bagamoyo mkoani
Pwani.
Afisa
Miradi msaidizi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko (kushoto) na Afisa
Maendeleo wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Teresia Irafay
wakinakili yanayojiri wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ikiwa ni
sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji cha kidigital (Unesco – Samsung
digital village) katika kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro
mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la IrikRAMAT linalomiliki
Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maoni yake wakati wa
kuhitimisha warsha ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa wiki wilayani
Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa
mradi kijiji cha Kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) cha
Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Warsha hiyo ya
wiki iliandaliwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) nchini.
Pichani
jii na chini ni wadau mbalimbali wa elimu, afya, Tehama na masuala ya
utamaduni na uchumi waliohudhuria warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na
UNESCO wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Kutoka
kushoto ni Mathias Herman wa UNESCO, Mkurugenzi wa elimu ya msingi
kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Sarah Mlaki pamoja na Afisa
Mtendaji wa kijiji cha Ololosokwan, Emmanuel Madeje.
Mkurugenzi
mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, akionesha kwa mifano
baadhi ya bidhaa za nje zikivyokuwa na ubora kwenye vifungashio wakati
wa warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha
digitali (Unesco-Samsung digital village) kwa wakazi wa kijiji cha
Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkurugenzi
mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisikiliza baadhi ya
maboresho ya changamoto zilizojadiliwa na kikundi kazi cha sekta ya
elimu na wadau mbalimbali wa elimu.
Mkurugenzi
Mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues akitoa maboresho ya kazi za vikundi
vilivyokuwa vikijadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali
zilizopo katika kijiji cha Ololosokwan kwa ajili ya utekelezaji wa mradi
wa kijiji cha kidigitali.
Picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo ya wiki moja iliyomaziki mwishoni mwa juma wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment