*AUNDA KAMATI YA KUSHUSHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARDHI KINONDONI
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema kuwa wilaya ya Kinondoni
inakabiliwa na changamoto migogoro ya ardhi ambayo inatakiwa kila mtu
ambaye amenyimwa haki ya ardhi watapata kutokana na utaratibu uliopo.
Makonda
aliyasema hayo hivi karibuni wakati ziara ya kutembelea wilaya hiyo,
Makonda alisema asili ya migogoro hii inatokana hasa na mgongano wa
uhalali wa umiliki pamoja na uvamizi wa maeneo ya wazi yaliyotengwa
maalumu kwa shughuli za jamii ni changamoto ya muda mrefu na natambua
juhudi nyingi zilizofanyika katika kutatua.
Makonda
alisema moja ya mkakati wangu ni kufanya utatuzi unaohusisha taasisi
zote muhimu ili kufupisha mlolongo unaowapotezea muda walioko kwenye
migogoro na kuhakikisha mwenye haki anapewa haki yake bila kuyumbishwa.
Alisema
anatenga siku moja ambayo ni ya Ijumaa kuwa siku maalumu ya kukutana na
wananchi na kusikiliza matatizo yanayohusiana na Ardhi na utaratibu huu
utaanza machi 6 mwaka huu na zoezi la uandikishaji kwa wale wanaohitaji
kusikilizwa matatizo yao utaanza majira ya saa 3.
Makonda
alisema Ili kupata ufumbuzi usio na shaka kamati ndogo itakayohusika
katika kushughulikia matatizo hayo itaundwa na Katibu tawala wilaya
(DAS) akiwa ni katibu, Mwanasheria wa Manispaa, Afisa Mipango miji,
Afisa Ardhi.
Aidha
alisema ili kufanya zoezi hili liwe na ufanisi na mafanikio ningeomba
wananchi wafuate utaratibu kuanzia ngazi za watendaji wa chini kabla ya
kufikisha kila muhusika ahakikishe amekuja na vielelezo vyote halali
vinavyoweza kutumika katika kufikia uamuzi.
No comments:
Post a Comment