Ofisa
wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Pauline Mdendemi akizungumza
na wanawake wafanyabiashara masokoni katika soko la Mchikichini Dar es
Salaam jana kutoka Wilaya ya Lushoto ambao wamekuja Manispaa ya Ilala
kwa mafunzo ya siku tatu kuhusu mambo mbalimbali pamoja na masuala ya
vicoba.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Soko la Mchikichini, Betty Mtewele (katika), akizungumza na wanawake wajasiriamali.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Soko la Mchikichini, Juliana Richard akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mjasiriamali kutoka Lushoto Tanga, Magreth Mkomwa (katikati), akiuliza swali katika mafunzo hayo.
Wanawake wajasiriamali wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Wanawake wajasiriamali wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Soko la Lukozi lililopo wilayani Lushoto, Zakati Tendwa akichangia jambo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
Wajasiriamali hao wakitembelea soko la Mchikichini kuona kazi za wenzao zinauzwa katika soko hilo.
Hapa wakiangalia nguo aina ya batiki zinazotengenezwa na wenzao wa soko hilo.
Hapa wakifurahia gauni la batiki katika soko hilo.
Dotto Mwaibale
WANAWAKE
wafanyabiashara katika masoko wametakiwa kujenga tabia ya kutunza
kumbukumbu zao na kufanya vikao vya mara kwa mara jambo litakalosaidia
kuwapunguzia changamoto za kazi zao.
Mwito
huo ulitolewa na Ofisa wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Pauline
Mdendemi wakati akizungumza na wanawake wafanyabiashara masokoni Dar es
Salaam jana kutoka Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga na Manispaa ya Temeke
ambao wapo Manispaa ya Ilala kwa ziara ya siku tatu ya mafunzo mbalimbali pamoja na masuala ya vicoba yaliyofikia tamati jana.
“Jengeni
tabia ya kutunza kumbukumbu zetu pamoja na kufanya vikao vya mara kwa
mara itawasaidia kujua changamoto mlizonazo na kuzitatua ” alisema
Mdendemi.
Mdendemi
alisema shirika hilo la EfG limefanikiwa kwa kiasi kikubwa utekelezaji
wa programu ya “Sauti ya Mwanamke Sokoni” kwa Manispaa ya Ilala ambapo
wanawake wajasiriamali wameweza kupaza sauti ya kupinga vitendo vya
kinyanyasaji dhidi yao.
Alisema
shirika hilo lilifanya mradi wa miaka mitatu katika manispaa hiyo
ambayo sasa imekuwa ya mfano na ndio maana wafanyabiashara wanawake
kutoka Lushoto mkoani Tanga wamefika kujifunza ili nao elimu hiyo
waipeleke kwa wenzao.
Alisema
lengo la mafunzo ni kuwapa fursa washiriki hao kuweza kujifunza kutoka
kwa wanawake wajasiriamali sokoni katika manispaa ya Ilala masuala
mbalimbali ikiwemo mbinu za kufanya ushawishi na utetezi ili kuboresha
mazingira ya ufanyaji kazi katika masoko.
Alitaja
malengo mengine kuwa ni namna ya kuongeza wanachama wa umoja na vicoba,
uendeshaji vikao vya umoja sokoni na namna mfumo wa kuweka na kukopa
(Vicoba) unavyoweza kuwasaidia wanawake wajasiriamali kukuza vipato vyao
na kuboresha biashara na maisha yao kwa ujumla.
Mdendemi
alitaja wajasiriamali walionufaika na mafunzo hayo kuwa ni wanawake
wanne kutoka wilaya ya Lushoto, Lukozi Lushoto watatu, Chamazi watatu na
Temeke Sterio watatu.
Mwenyekiti
wa soko la Lukozi kutoka Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Zakati Tendwa
alisema mafunzo hayo yamewafumbua macho kwani walikkuwa hawajui chochote
kuhusu masuala ya vicoba na kwa niaba ya wenzake amelishukuru shirika
la EfG kwa kuwapigania wanawake wajasiriamali masokoni. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment