PICHA NA IKULU
========================
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amefurahishwa na
uwepo wa vyama vya Ushirika vya Akiba na mikopo (SACCOS) katika taasisi
na idara za serikali, akisema kuwa hilo ni jambo la maana kwa kuwa
inatoa fursa kwa watumishi kuwa na kipato cha ziada kitachosaidia
kuwaletea ahueni kwani mishahara pekee haikidhi matakwa yao yote.
Amesema SACCOS ni
kama
benki ya mtu mnyonge, na kusisitiza kwamba mifuko ya aina
hiyo inaposimamiwa vizuri faida yake kwa wanachama ni kubwa sana kwani
humpa mtumishi ahueni na kumfanya afanye kazi kwa moyo na bila wasiwasi
ama usongo wa mawazo.
Balozi Sefue ameyasema hayo Jumanne Machi 3, 2015 jioni alipokuwa akiongea na uongozi wa Ikulu SACCOS,
uli
omtembelea ofisini kwake Ikulu Dar es salaam kumkabidhi rasmi
kitabu chake cha uanachama kufuatia kujiunga kwake na ushirika huo.
“Mishahara yetu ndani ya utumishi wa umma haitoshi kukidhi
mahitaji yetu yote, kwa hiyo mipango yote hii ya SACCOS, Mfuko wa
Rambirambi na Mfuko wa Ushirika
iliyopo hapa Ikulu
inafanya maisha ya mtumishi yawe na ahueni sana na kumfanya afanye kazi kwa moyo.
“Hayo ni mambo ambayo nayaamini sana na nayaunga mkono; na
naamini hata Mhe Rais mwenyewe anayaunga mkono na ndio maana amekuwa
mwepesi kujiunga na ushirika ”, amesema Balozi Sefue baada ya
kukabidhiwa kitabu namba 2 na Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw.
Deodatus Gaudio. Kitabu namba moja amekabidhiwa Rais Jakaya Mrisho
Kikwete.
Awali, mshauri Mkuu na Mlezi wa Ushirika huo wa Ikulu, Bw.
Joseph Sanga, alimfahamisha Katibu Mkuu Kiongozi kwamba mifuko ya
SACCOS, Ushirika wa Nyumba na Rambirambi ya watumishi wa Ikulu iko
imara na inaendelea kunufaisha wanachama wake kwa ufanisi.
Bw. Sanga amesema malengo makuu ya mifuko hiyo ni kuleta
ustawi kwa watumishi na kwamba wote wanaelewa kuwa mikopo ya SACCOS yao
sio kwa ajili ya kununulia chakula ama mavazi bali ni ya kuwekeza kwenye
miradi itayowaongezea kipato.
“TUnataka kwenda mbali zaidi kwa kushirikiana na mfuko wetu
ya Ushirika wa Nyumba ambo tayari umepeleka maombi ya ardhi kwa
wanachama wake ambapo viwanja vikipatikana tuna mategemeo ya kuwapa
mikopo kuvununua. Mpango huu una faida kwani ni wa amana kubwa na riba
ndogo”, alisema Bw. Sanga alipokuwa anafafanua kuhusu mipango ya Ikulu
SACCOS.
No comments:
Post a Comment