Kumekuwa
na taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao ya kijamii kuhusu hali ya
Afya ya Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai. Ofisi ya Bunge inapenda
kuutangazia umma na Wananchi wote kuwa, taarifa hizo zinazosambazwa
katika baadhi ya Mitandao si za kweli, bali ni uzushi mtupu.
Ukweli ni kwamba Naibu Spika wa
Bunge, Mhe. Job Ndugai ni Mzima wa afya na hivi sasa yuko jimboni kwake
Kongwa, Mkoani Dodoma akifanya maandalizi ya Mwisho ya Ziara ya Katibu
Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana itakayofanyika mwishoni mwa wiki hii
na hasa Jimboni Kongwa, Dodoma.
Ofisi ya Bunge inapenda kuwatoa
hofu Wananchi wote na kuwataka kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa si za
kweli bali ni uvumi unaonezwa na watu wachache wenye nia ovu ya kujenga
hofu miongozni mwa Wananchi kupitia mitandao ya kijamii.
Aidha tunapenda kutoa rai kwa watu
wote kuacha kusambaza taarifa hizo potofu na badala yake kama kuna
taarifa zozote kuhusu Ofisi ya Bunge au Viongozi wake wafanye jitihada
za kuthibitisha taarifa hizo kwenye Mamlaka husika kabla za kuzisambaza.
Ofisi ya Bunge inao utaratibu
rasmi wa kutoa taarifa muhimu kwa wananchi na umma kwa ujumla, hivyo si
vyema kwa watu kusambaza taarifa potofu kuhusu Bunge na viongozi wake
ambazo zinaweza kuleta usumbufu miongoni mwa Viongozi na baadhi ya
wananchi.
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
4 MACHI 2015
No comments:
Post a Comment