Na Mwandishi Wetu
ZAIDI
ya watu 10,000 wanaozunguka bwawa la Kalemawe wilayani Same mkoani
Kilimanjaro watanufaika na ukarabati wa bwawa hilo na kuwekewa muundo
mpya wa kiutawala na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Ukuzaji wa Mitaji
(UNCDF).
Bwawa
hilo ambalo lipo katika kata za Kalemawe na Ndungu lilijengwa na
watawala wa Kiingereza mwaka 1952-1959 kwa ajili ya kusaidia shughuli za
kilimo na ufugaji baada ya kuanzishwa kwa hifadhi ya Mkomazi na hivyo
wakazi kuzuiwa kwenda katika hifadhi hiyo kwa shughuli mbalimbali.
Taarifa
ya kuwepo kwa mradi huo mkubwa, imetolewa na Mkuu wa ushauri wa ufundi
wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) nchini, Bw. Peter
Malika wakati akiwakaribisha madiwani wa kata hizo ambao wameitwa
katika kongamano la siku moja Dar es salaam kuzungumzia ukarabati na
uendeshaji wa bwawa hilo.
Malika
amesema Mfuko huo wa ukuzaji wa mitaji unasaidia ukarabati wa bwawa
hilo kupitia mpango wake wa uendelezaji rasilimali kwa kutumia fedha za
ndani (LFI) .
Amesema baada ya ukarabati huo, mradi utaendeshwa kwa pamoja kati ya serikali na watu binafsi.
Malika alisema ukarabati huo unakidhi lengo la mfuko ambalo ni kuwezesha miundombini inayoleta maendeleo.
“Ukarabati na hatimaye uendeshaji wa bwawa hilo kutasaidia kuleta
mabadiliko makubwa ya maendeleo ya mitaji kwa watu binafsi na umma.”
alisema
Kapufi
alisema kwamba pamoja na kushukuru Mfuko wa Mitaji kukubali kuwasaidia,
amesema bwawa hilo ni muhimu sana katika kuondoa migogoro na migongano
ndani ya jamii pia na mamlaka ya hifadhi ya Mkomazi.
Alisema
kurejeshwa kwa hali yake ya zamani kutasaidia wafugaji, wakulima na
watumiaji wengine wa bawawa hilo kama wavuvi wa samaki kila mmoja kuwa
na nafasi katika matumizi ya bwawa.
Aidha
alisema ukarabati utakaofanywa na muundo wa uendeshaji wa bwawa hilo
utasaidia wilaya pia kufikiria namna ya kutengeneza bwawa jingine katika
Mto Ruvu kwa sababu kama hizo za kuwapa uwezo zaidi wananchi katika
maendeleo yao kwa kutumia rasilimali maji.
Toka
kujengwa kwake katika miaka ya 1950, bwawa hilo lenye urefu wa
takaribani kilomita tatu na upana wa mita 200 limepungua ukubwa wake kwa
karibu nusu ya uwezo wa awali kwa sababu za kujaa tope, matumizi
mabaya, kukosa ukarabati na usimamizi.
Aidha limeota magugu maji ambayo inaua kizazi cha samaki na kuvuruga uvuvi.
No comments:
Post a Comment