Na Happy Shirima – Habari Maelezo.
Dar es salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo [WAMA]
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake
Duniani yatakayofanyika Machi 8 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es salaam .
Akizungumzia maadhimisho hayo
leo jijini Dar es salaam , Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar se salaam Mhe.
Raymond Mushi amesema kuwa maadhimisho hayo mwaka huu yataongozwa na
kauli mbiu isemayo “Uwezeshaji Wanawake Tekeleza, Wakati ni Sasa “.
Amesema ujumbe huo unaikumbusha
jamii kujenga mazingira wezeshi kwa kutambua mchango wa wanawake katika
kuleta maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla .
Ameeleza kuwa wadau kote nchini
wanatakiwa kuelimishwa ili kuangali upya wajibu wao kwa kuwashirikisha,
kuwaamini na kuwapa wanawake haki sawa katika nafasi za elimu , uchumi
na uongozi ili waweze kuwa chachu ya maendeleo yao binafsi, familia na
taifa zima.
“Lengo la maadhimisho haya ni
kukumbuka wajibu wa kila mmoja kushiriki katika mikakati ya
kukabiliana na changamoto mbalimbali za wanawake kuanzia ngazi ya kaya
hadi Taifa” Amesema.
Akitoa ufafanuzi kuhusu
maadhimisho hayo amesema kuwa yanaambatana na maonyesho ya kazi na
bidhaa mbalimbali za vikundi vya ujasiriamali na kuzishirikisha Asasi za
Kiraia zinazojishughulisha na masuala ya utoaji wa Elimu ya Uraia na
sheria ya utunzaji fedha.
Ameongeza kuwa siku ya kilele
kutakuwa na maandamano yatakayoanzia Barabara ya Lumumba na
kuishiaviwanja vya mnazi mmoja ambayo yatapokewa na mgeni rasmi na
wananchi wa mkoa wa Dare s salaam.
No comments:
Post a Comment