Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa maradhi Zanzibar Dkt. Salma
Masauni akitoa neno la shukrani mara baada ya kumaliza mafunzo ya siku
tatu juu ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, mafunzo hayo yamezaminiwa
na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) huko Hoteli ya Zanzibar
Beach Resort.
Mwakilishi kutoka shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO)Tanzania
Dkt. Grase Saguti akiwataka wafanyakazi wa sekta ya Afya Zanzibar
kuyatumia vyema mafunzo waliyoyapata. Naibu
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiyafunga mafunzo ya
siku tutu ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, mafunzo hayo yanafanyika
Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mjini Unguja. Picha na Makame Mshenga-
Maelezo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment