Wafanyakazi
wa kampuni ya Tan Communication Media inayo miliki kituo cha Radio 5
chenye makao yake makuu jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja jana
katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kitaaluma ili waweze kuandika
habari za kuboresha maisha ya jamii kwa kupata maendeleo kuelekea
uchaguzi mkuu,mafunzo hayo yanaendeshwa na shirika lisilo la kiserikali
la BBC Media Action, aliyevalia shati la blue ni mkufunzi mwandamizi
Pendael Omari wa shirika hilo(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mkufunzi
mwandamizi Pendael Omari wa shirika lisilo la kiserikali la BBC Media
Action akiwa anatoa ufafanuzi katika mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika
katika ofisi za Radio 5,mafunzo hayo yalidumu kwa takribani wiki mbili
Mtangazaji
maarufu wa kituo hicho Ernest Matundiro a.k.a Prince de la ville
kushoto akiwa anaandika vipengele muhimu katika uandishi wa habari,kulia
ni Mhariri wa kituo hicho Monica Nangu
Msimamizi
mkuu wa vipindi vya Radio 5 kulia Mathew Philip akiwa anafatilia
mafunzo kwa ukaribu zaidia,kushoto ni mtangazaji wa kituo hicho Wilberd
Kiwale
Mkufunzi mwandamizi Pendael Omari akiwa anatoa ufafanuzi kwa Mhariri Mkuu Philip Magesse katika mafunzo hayo jana
Mtangazaji wa kituo hicho Yakubu Simba
Mtangazaji machachari wa kituo hicho Godfrey Thomas a.k.a GT
Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa http://jamiiblog.co.tz/ Pamela Mollel akiwa anafanya mahojiano na mkuu wa vipindi vya Radio 5 Mathew Philip kuhusu mafunzo hayo
Mtangazaji wa kituo hicho Clara Moita wakiwa katika majadiliano na mkuu wa vipindi vya Radio 5 Mathew Philip
Wafanyakazi wa Radio 5 katika pozi
Wafanyakazi
wa Radio 5 jijini A rusha wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa
kitaaluma ili waweze kuandika habari za kuboresha maisha ya jamii kwa
kupata maendeleo kuelekea uchaguzi mkuu,mafunzo hayo yanaendeshwa na
shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action,
Akizungumza mapema jana katika mafunzo hayo Mkufunzi
mwandamizi Pendael Omari wa shirika lisilo la kiserikali la BBC Media
Action alisema kuwa lengo la kufanya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa
kitaaluma pindi wanapokuwa katika kazi zao
Alisema
kuwa mafunzo hayo yatawezesha pia upatikanaji wa utawala bora kwa kuwa
vyombo vya habari vitaelimisha wananchi umuhimu wa kuchagua viongozi
watakaoleta maendeleo
Kwa
upande wake Msimamizi mkuu wa vipindi vya radio hiyo Mathew Philip
alisema kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kuwa
walikuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo zaidi
Pia
alisema kuwa kupitia mafunzo hayo wamepata ufahamu wa namna ya kutafuta
habari za kupigia kura maoni pamoja na uchaguzi mkuu bila upendeleo kwa
kumpa msikilizaji nafasi ya kusikika na kumpa elimu
Mafunzo hayo yalifanyika katika ofisi za radio 5 kwa muda wa wiki mbili
(Habari na Picha Pamela Mollel wa jamiiblog)
No comments:
Post a Comment