Mkurugenzi wa tigo nyanda za juu
kusini, Jackson Kiswaga akikabidhi moja ya bati alizotoa kwa shule
mbalimbali za jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa
…………………………………………………………………………..
NA DENIS MLOWE, IRINGA
WANANCHI wa jimbo la Kalenga
wametakiwa kujenga utamaduni wa kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu,
badala ya kujikita kuchangia sherehe za harusi na mambo mengine
yasiyokuwa na tija katika maendeleo ya jimbo hilo.
Hayo yamezungumzwa na mdau wa
maendeleo, Jackson Kiswaga wakati akikabidhi mabati 50 na mifuko ya
saruji 30 kwa shule ya sekondari ya Nyabula inayomilikiwa na kanisa
katoriki parokia ya Nyabula katika sherehe ya kuchangia ujenzi wa
maabara ya Shule hiyo iliyoko katika wilaya ya Iringa vijijini.
Kiswaga alisema kuwa urithi
pekee kwa watoto ni elimu hivyo ni jukumu la wazazi kuchangia sekta ya
elimu kuliko kusubiri serikali ambayo ina mzigo mkubwa kwa faida ya
vizazi vilivyopo na vijavyo katika kukuza uwezo wa wanafunzi katika
mambo ya masomo.
“Mzazi unaweza kumwachia kijana
wako mali, lakini itakwisha, ukimwachia elimu hakika huu ndiyo urithi
pekee watanzania wenzangu, tujitoe kuchangia sekta ya elimu kama ambavyo
tunafanya katika sherehe na kumbuka maisha ya sasa bila elimu
utasababisha mwanao awe katika maisha magumu hapo mbeleni hivyo
tusisubiri serikali tuwe na utamaduni wa kuchangia katika sekta hii ya
elimu ndugu zangu,” alisema Kiswaga.
Alisema kuwa juhudi za wananchi
na mashirika pamoja na serikali zinahitajika ili kuwajengea wanafunzi
mazingira bora ya kujifunzia na ili waweze kufaulu vizuri katika masomo
yao hivyo kuchangia maabara itasaidia sana kukuza uwezo wa mwanafunzi
katika masomo ya sayansi pindi yakikamilika.
Kiswaga aliongeza kuwa sekta ya
elimu ni sekta muhimu sana kwa maendeleo ya nchi ambapo inabidi juhudi
zaidi ziongezeke kuweza kuifanya elimu kuwa silaha bora itakayowasiadia
vijana kuondokana na umaskini.
Naye Padri wa Parokia ya Nyabula
Philipo Kindole alimshukuru Kiswaga kwa msaada wa mabati na saruji na
kuwataka wananchi wengine kuiga mfano huo kwa maendeleo ya elimu katika
mkoa wa
No comments:
Post a Comment