Waziri
wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif Suleiman akikata utepe kuzindua mpango
wa upimaji usikivu wa watoto wachanga katika hafla iliyofanyika
Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar, wa kwanza (kushoto)
mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay Andemichael na (wakatikati)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
Daktari
Asma Ame Hassan akimpima usikivu mtoto Nour Sabri Al hilal katika
uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga hafla iliyofanyika
Hospitali kuu ya Mnazimmoja.
Wafanyakazi
wa Afya waliopatiwa mafunzo maalum ya kuwapima usikivu watoto wachanga
wakimsikiliza Waziri wa Afya (hayupo pichani) katika uzinduzi huo.
Waziri
wa Afya Rashid Seif Suleiman akisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa
kuwapima usikivu watoto wachanga. (kulia) Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya
Mnazimmoja Dkt. Jamala Adam Taib na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
Baadhi
ya wageni walioalikwa katika uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto
wachanga wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika Hospitali ya Mnazimmoja.
…………………………………………………………………….
Na Ali Issa Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Afya wa Zanzibar Rashid
Seif Suleiman amesema sikio, mdomo na macho ni sehemu muhimu sana
katika maisha ya binaadamu hivyo unapokuwa na wataalamu wa
kushughulikia viungo hivyo ni neema kubwa inayopaswa kuenziwa.
Haya ameyasema jana katika
Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar wakati wa uzinduzi wa
kuwapima usikivu watoto wachanga mara baadaya kuzaliwa ili kujua
matatizo yao.
Amesema uchunguzi wa watoto
wachanga kujua usikivu wao mapema ni mpango mzuri ambao utalisaidia
Taifa kuwa na watoto wenye usikivu mzuri na njia rahisi ya kuwapatia
matibabu kwa watakaogundulika na matatizo hayo.
“Kujua tatizo la kiafya mapema na
kuanza kulishughulikia kunapunguza gharama za matibabu hivyo nawanasihi
wazazi kuwapeleka watoto wenu mara baada ya kujifungua, ”alisisitiza
Waziri wa Afya.
Amesema maradhi ya usikivu
yamekuwa yakiwasumbua watoto wengi Zanzibar na iwapo kila mzazi
atatimiza wajibu wake wa kumpeleka mtoto wake kupata vipimo yataweza
kupungua.
Waziri wa Afya aliwataka wazazi
kuwa na utamaduni wa kuzalia Hospitali ili kupata huduma hiyo kwa
urahisi na watakaozalia majumbani kuwapeleka watoto wao kuchunguzwa
usikivu mara baada ya kuzaa.
Aidha Waziri huyo aliwataka
madaktari waliopatiwa mafunzo ya kutoa huduma hiyo kuwa waadilifu
katika kutekeleza kazi zao kwani huduma za watoto wachanga na wazazi
zinahitaji uvumilivu.
Waziri alisema tatizo la uskivu
huazia mtoto anapochelewa kulia mara baada ya kuzaliwa ama wanapopata
homa ya manjano, kutopatiwa chanjo, mzazi kuchelewa kuzaa baada ya
uchungu wa muda mrefu na kuzaliwa mtoto bila ya ya kufika muda wa
kuzaliwa.
Nao madaktari walio patiwa mafuzo
hayo walisema kuwa wana uwezo mzuri wa kuwapima usikivu watoto na
kubaini matatizo yao na kuishauri Serikali kuandaa utaratibu mzuri wa
kuwafikia watoto watakaozaliwa vijijini.
Mradi huo wa kupima watoto usikivu
ulipokea msada wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi kutoka Jumuiya ya
Madaktari wanotoa huduma za matibabu vijijini ( ZOP) ambavyo vina
thamani vya Dola elfu 50 za kimarekani.
No comments:
Post a Comment