Mkurugenzi
wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wanja Mtawazo (
kulia) akisalimiana na Mbunge wa Lulindi- Masasi, Jerome Bwanausi (
kushoto) ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini mara baada ya kamati hiyo kuwasili katika eneo la
mtambo wa kufua umeme wa Kinyerezi I. Kamati hiyo inafanya ziara katika
miradi ya umeme katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Singida, Arusha
na Kilimanjaro pamoja na kuzungumza na wadau wa madini ya tanzanite
katika mkoa wa Manyara ili kujionea maendeleo ya sekta hizo.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga (kulia)
akimsikiliza kwa makini Meneja Mradi Mkazi wa Kampuni ya Yakobsen
Elektro ya Norway inayojenga mtambo wa Kinyerezi I Markkli Repo ( wa
pili kutoka kushoto) mara baada ya kuwasili katika eneo la mtambo huo
ili aweze kuwaongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na
Madini kwenye ziara katika mitambo hiyo.
Meneja
Miradi ya Kinyerezi Mhandisi Simon Jilima (kulia) akielezea maendeleo
ya ujezi wa mtambo wa Kinyerezi I mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na
Madini (Madini), Charles Kitwanga (wa tano kutoka kulia), Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na wataalamu kutoka Wizara ya
Nishati na Madini.
Mbunge
wa Lulindi- Masasi, Jerome Bwanausi (katikati) akisisitiza jambo katika
ziara hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini),
Charles Kitwanga na kulia ni Meneja Miradi ya Kinyerezi Mhandisi Simon
Jilima
Mkurugenzi
wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Felchesmi Mramba
akielezea mikakati ya shirika la Tanesco kuboresha huduma za umeme
nchini kote.
……………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Meneja Miradi ya Kinyerezi Mhandisi Simon Jilima amesema kuwa
mtambo wa Kinyerezi 1 unaojengwa na kampuni ya Yakobsen Elektro ya
Norway unatarajia kukamilika mapema Juni mwaka huu.
Mhandisi Jilima aliyasema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Nishati na Madini iliyofanya ziara katika mtambo huo ili
kujionea maendeleo ya ujenzi wake. Kamati hiyo imeanza ziara ya
kutembelea miradi ya umeme iliyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,
Dodoma, Singida, Arusha na Kilimanjaro pamoja na kuzungumza na wadau wa
madini aina ya tanzanite katika mkoa wa Manyara.
Mhandisi Jilima alisema kwa sasa mradi huo umekamilika kwa
asilimia 80 na kufafanua kazi inayofanyika kwa sasa ni kumalizia
utandazaji wa nyaya, ufungaji wa mabomba ya maji na gesi pamoja na
ujenzi wa barabara za ndani.
Alisema kuwa ofisi kwa ajili ya watumishi pamoja na karakana kwa ajili ya kuhifadhia mitambo imekamilika.
Akielezea gharama za mradi huo Mhandisi Jilima alisema mpaka
sasa serikali imelipa kiasi cha Dola za Marekani milioni 167.2 na
kuongeza kuwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 15 kinatarajiwa
kumaliziwa kabla ya kukamilika kwa mradi.
Akielezea changamoto katika utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi
Jilima alieleza kuwa awali changamoto kubwa ilikuwa ni ukamilishwaji wa
mradi wa bomba la gesi ili waweze kutumia gesi hiyo katika kuzalisha
umeme lakini kutokana na kasi ya mradi huo kuwa ya kuridhisha wana imani
kuwa gesi itaanza kuzalishwa mapema kabla ya kukamilika kwa mtambo wa
Kinyerezi 1
“ Ndugu wajumbe, awali tulikuwa na wasiwasi wa kupatikana kwa
gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme kupitia mradi wa Kinyerezi 1 kutokana
na mradi wa bomba la gesi kuwa na changamoto nyingi, lakini baada ya
kuona mradi wa bomba la gesi uko katika hatua nzuri yaani zaidi ya
asilimia 90, tunaamini kuwa mara mtambo utapokamilika, gesi itakuwa
imekwishaanza kuzalishwa na hapo ndipo tutaanza kuzalisha umeme mara
moja,” alieleza Mhandisi Jilima
Akielezea fidia kwa wakazi waliopisha ujenzi wa mradi huo,
Mhandisi Jilima alieleza kuwa mradi wa Kinyerezi I ulikwishafanya
tahmini pamoja na kulipa fidia kwa wakazi waliopisha ujenzi wa mtambo
huo tangu mwaka juzi.
Wakati huohuo wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini
walipongeza hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mtambo huo na kuitaka
serikali kukamilisha malipo ya kiasi kilichobaki cha Dola za Marekani
milioni 15 ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.
No comments:
Post a Comment