Nyaraka
hizo zina orodha kubwa ya wadaiwa zikiwemo taasisi za serikali ,
makampuni zikiweno benki kama vile NMB inayodaiwa fedha ndogo ambayo
jumla yake ni shilingi elfu 79.179.50 fedha ambayo ni ndogo sana ikiwa
ni bili ya mwezi wa pili 2015.
Sauala
hilo limekuja baada ya malalamiko ya wananchi katika mkutano huo ambapo
walimweleza Katibu Mkuu wa CCM kuwa maji hayatoki, lakini kila mwezi
wanadaiwa bili ya maji jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwao, Akielezea
sakata hilo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji
Mpwapwa Bw. Shadrack Matemba amesema mradi huo ni mkubwa na unatosheleza
mahitaji ya maji kwa wananchi wa mji wa Mpwapwa. tatizo ni kwamba
Taasisi na makampuni mengi hayalipi bili zao kwa wakati jambo ambalo
linafanya uendeshaji kuwa mgumu huku akikabidhi nyaraka za wadaiwa hao
mbele ya Kinana
Kinana
amemkabidhi suala hilo mkuu wa mkoa wa Dodoma Kapteni Chiku Galawa na
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Dr. Jasmine Tisekwa ili kulishughulikia huku
akiahidi pia kulifuatilia yeye mwenyewe kwa makini ili kuhakikisha
wananchi wa mji wa Mpwapwa wanapata huduma nzuri ya maji safi na salama.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameanza ziara ya kikazi ya siku 9
mkoani Dodoma akizna na wilaya ya Mpwapwa kabla ya kuendelea na wilaya
zingine na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Katika ziara hiyo Kinana
anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kulia katika
picha ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji katika mji wa Mpwapwa Bw. Shadrack Matemba.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MPWAPWA).
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maji katika mji wa Mpwapwa Bw. Shadrack Matemba
akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Dodoma Mh. Adam Kimbisa mara baada ya kukabidhi orodha hiyo ya wadaiwa
sugu wa bili za maji kwa Mkuu wa mkoa wa Galawa ambaye anaonekana
akiipitia orodha hiyo.
No comments:
Post a Comment