Meneja
Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea
maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika
hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania,
Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo
tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na
Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.

Spika
wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akitoa shukrani kwa uongozi wa NSSF
mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea miradi anuai ya NSSF
jijini Dar es Salaam, ambapo aliambatana na wajumbe wa kamati ya uongozi
ya Bunge.
Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau (mwenye kanzu) akitoa ufafanuzi kwa Spika
wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya
uongozi ya Bunge walipo tembelea miradi mbalimbali ya NSSF ya jijini Dar
es Salaam ukiwemo mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa
ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.
Moja ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa unaotekelezwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) eneo la Kigamboni.
Baadhi
ya viongozi wa NSSF wakimuongoza Spika wa Bunge la Tanzania, Anne
Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge katika ziara yao
ya kutembelea miradi anuai ya NSSF jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu, Joseph Nyamuanga (wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi kwa
Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya
pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa
daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha
Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.
Spika
wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya
uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na
NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa
Kigamboni.
Meneja
Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa
Fedha, Saada Mkuya Salum (MB) juu ya mradi. Wengine ni Spika wa Bunge la
Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge
walipo tembelea miradi mbalimbali ya NSSF ya jijini Dar es Salaam
ukiwemo mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na
Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.
Spika
wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya
uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na
NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa
Kigamboni. Mwenye kanzu ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhani Dau.
Meneja
Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (aliyenyoosha mkono) akielezea
maendeleo ya mradi huo kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda
pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa
daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha
Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.
Spika
wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya
uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na
NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa
Kigamboni.
Meneja
Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (wa pili kushoto mbele) akitoa
ufafanuzi juu ya mradi huo kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda
pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa
daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha
Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SPIKA wa Bunge la Tanzania, Anne
Makinda amelipongeza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa
miradi mikubwa mbalimbali linayoendelea kuwekeza nchini ambayo imekuwa
chachu ya maendeleo na kukuza hadhi ya nchini.
Spika Makinda ametoa kauli hiyo
jana alipokuwa akitembelea baadhi ya miradi mikubwa ya NSSF iliyopo
jijini Dar es Salaam, ukiwemo mradi wa ujenzi wa daraja la kubwa la
kisasa linalojengwa kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na Mji wa
Kigamboni pamoja na mradi mkubwa wa ujenzi wa Mji wa Kisasa unaojulikana
kwa jina la Dege ECO Village unaojengwa kwa ubia pamoja na ujenzi wa
nyumba za kisasa zenye hadhi mbalimbali kulingana na mahitaji ya watu.
Akizungumza wakati akitembelea
miradi hiyo, Makinda alisema miradi hiyo mbali na kuleta maendeleo
nchini inakuza hadhi ya nchi pamoja na kuirahisishia serikali katika
utoaji huduma kwa wananchi wake.
Aliiomba Serikali kupitia Wizara
mbalimbali na jamii nzima kuendelea kutoa ushirikiano dhidi ya miradi
hiyo kwani inachangia maendeleo kuanzia ngazi ya jamii pamoja na taifa
kwa ujumla. Aliwataka wananchi kutumia fursa iliyopo ya kununua na
kukopa nyumba zinazojengwa na shirika hilo kwani mbali na kujengwa kwa
hadhi anuai na kisasa zimepangiliwa jambo ambalo linarahisisha utoaji wa
huduma za jamii dhidi yao.
Alisema kwa maendeleo ya sasa ni
nchi ya Tanzania pekee ambapo raia wake hujenga nyumba wenyewe, kwani
mataifa mengi yaliyoendelea nyumba hujengwa na mashirika na kuuzwa kwa
raia jambo ambalo huchangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa miji
iliyopangiliwa tofauti na ilivyo Tanzania.
“…Duniani kote watu wanaojenga
nyumba wenyewe hadi sasa ni Tanzania tu, na hii ndio chanzo kikubwa cha
nchi yetu kuendelea na kuwa na miji ambayo haijapangiliwa (ujenzi
holela). Lazima tubadilike unajua ukiwa na mji uliopangiliwa ni rahisi
hata kuwahudumia wananchi wako…,” alisema Makinda.
Aidha alishauri uwepo wa utaratibu
mzuri wa kukopesha nyumba za kisasa zinazojengwa na NSSF ili wahitaji
wapewe na kulipa kwa awamu huku wakimilikishwa nyumba hizo jambo ambalo
litaondoa adha ya upatikanaji wa makazi bora kwa wananchi.
Katika ziara hiyo Spika Makinda
aliambatana na Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenista Mhagama , Waziri wa Kazi
na Ajira, Gaudensia Kabaka pamoja na Kamati ya Uongozi ya Bunge la
Tanzania ambao kwa pamoja walilipongeza Shirika la NSSF na kushauri
kuendelea kuwekeza pia katika mikoa mingine inayochipukia kimaendeleo
kwa sasa ili kusambaza huduma maendeleo mengine.
Awali akitoa taarifa za maendeleo
ya ujenzi wa daraja la kisasa la Kigamboni, Meneja Mradi wa NSSF,
Mhandisi John Msemwa alisema licha ya changamoto zilizojitokeza mradi
huo hadi sasa umekamilika kwa asilimia 75 ya ujenzi wake.
Kwa upande wake, Mhandisi Juhus
Nyamuhokya wa kampuni ya Ujenzi ya Hifadhi wabia wa NSSF katika ujenzi
wa Kijiji cha kisasa cha ‘Dege ECO Village’ kinachojumuisha ujenzi wa
nyumba 7,460 za kisasa zenye hadhi tofauti kulingana na mahitaji alisema
ujenzi wake utajumuisha miaka minne ukijengwa kwa awamu tatu.
Mhandisi Nyamuhokya alisema awamu
ya kwanza ya mradi huo inakamilika Desemba 2015, awamu ya pili
itakamilika Desemba 2016 huku awamu nyingine ikitarajiwa kukamilika
Desemba 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhani
Dau alimshukuru Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda pamoja na
wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge kwa kutembelea miradi hiyo ambayo
ina lengo lakuchochea maendeleo ya taifa na wananchi kiujumla.
No comments:
Post a Comment