Mwanaharakati wa siku nyingi wa
wanyama pori na mazingira nchini Tanzania Kidon Mkuu, akiwa Philipine
Manila December 2014 kwenye harakati zake za matatembezi ya kupinga
kuuwawa kwa Tembo na Faru akiwa na wanaharakati wenzake wa huko
Philipine
Mwanaharakati wa siku nyingi wa
wanyama pori na mazingira nchini Kidon Mkuu, akiwa Philipine Manila
December 2014 kwenye matatembezi ya kupinga kuuwawa kwa Tembo na Faru
akiwa na Susan Jaylo
Mwanaharakati Kidon Mkuu akiwa kweye hoteli alikoshukia ya Sofitel mjini Manila Philipine
…………………………………………………………………….
Na Pamela Mollel,Arusha
Mwanaharakati wa siku nyingi wa wanyama pori na mazingira nchini Tanzania Bw.Kidon Mkuu amempongeza Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa kitendo cha kuchoma moto meno ya tembo tani 15 katika kuhadhimisha siku ya wanyamapori Dunia
Mwanaharakati wa siku nyingi wa wanyama pori na mazingira nchini Tanzania Bw.Kidon Mkuu amempongeza Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa kitendo cha kuchoma moto meno ya tembo tani 15 katika kuhadhimisha siku ya wanyamapori Dunia
Bw.Mkuu aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati akiongea na
vyomba vya habari kuhusu siku ya wanyamapori dunia, ambapo alisema kuwa
anamuunga mkono Rais huyo kwa kufanya tukio hilo la kihistoria la
kuchoma meno ya tembo
Alisema faida ya kufanya hivyo ni kudhibiti masoko na mianya ya
kusafirisha meno hayo hali itakayosaidia ujangili wa tembo kupungua
Aidha alitoa wito kwa serikali na wizara kuhamasisha jamii
kuhusu siku ya wanyamapori dunia kama wanavyofanya nchi zingine hali
itakayosaidia jamii kufahamu wajibu wao wa kulinda wanyamapori
Siku ya Wanyamapori Duniani
ilitangazwa na Baraza la Umoja wa Mataifa Desemba 20, 2013 ili
kuhamasisha kulinda wanyamapori na mapori na uhadhimishwa tarehe3 April
kila mwaka
No comments:
Post a Comment