kuu wa UDP Zanzibar Juma Khamis Fakih amemvaa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim
Seif
Sharif Hamad na kuigwaya kauli yake ya kuwataka wananchi kutoshiriki
zoezi la upigaji wa kura ya maoni juu ya katiba inayopendekzwa .
Amesema
kuwa kauli ya Katibu Mkuu wa CUF haina nia njema na wananchi wa
Zanzibar na haifai kutolewa na Kiongozi wa juu wa Serikali kama huyo
ambaye amepewa dhamana ya kuwaongoza na kuwatumikia wazanzibar .
Katika mahojiano maalumu na gazeti hili Naibu
Katibu huyo amewataka wananchi kuipuuza kauli hiyo na kuwahimiza
kuisoma katiba inayopendekezwa ili wakati ukifika afanye maamuzi sahihi
na kutumia haki yao kidemokrasia .
Amesema
kuwa katiba inayopendekezwa ni suluhisho la changamoto na kero za
muungano ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu na kwamba
kutoipigia kura katiba hii ni kuhalalisha kuendelea kutumika kwa katiba
iliyopo ambayo ina mapungufu mengi .
“Ni
vyema wananchi kuipuuza kauli ya Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar
ya kuwataka kutoshiriki kura ya maoni , hii ni kauli ambayo haina nia
njema na wananchi wa Zanzibar na haifai kutolewa na kiongozi wa juu wa
Serikali kama yeye ”alieleza .
“Kama
hatukuipigia kura katiba hii unafikiri mafuta ambayo tumekuwa tukiyadai
tutayapata wapi , mikopo ya nje tutaipatawapi ? , hapa ni lazima
wananchi wapime kuhusu kauli hii ” alihoji na kuongeza .
Aidha ameongeza
kwa kuwataka wananchi viongozi wa vyama vya upinzani ambao wanaoipinga
katiba inayopendekezwa kuwapa uhuru wananchi wa kuamua wenyewe kulingana
na maoni yao baada ya kuisoma katiba hiyo .
“Hii
ni katiba ya watanzania wote na hizi kauli za viongozi akiwemo Makamo
wa Kwanza wa Rais ni kama kuwalazimisha wananchi kufuata maoni yake
jambo ambalo linapingana na misingi ya utawala bora ”alifahamisha .
Katika
hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu huyo amewataka wananchi wa Zanzibar
hususani Kisiwani Pemba kuacha kuwa watumwa wa Kisiasa kwa kuwaepuka
viongozi wanaojali maslahi yao binafsi bali waangalie viongozi wenye nia ya kuwaletea maendeleo .
Amesema
kuwa amajimbo ya Pemba ambayo vingozi wake Wabunge na Wawakilishi ambao
wanatoka chama cha CUF wameshindwa kuwaletea mabadiliko ya maendeleo na
badala yake wangalie viongozi walio na uwezo wa kuleta maendeleo katika
majimbo yao bila ya ubaguzi .
Na Masanja Mabula –PembaNaibu Katibu M
No comments:
Post a Comment