Angelina
Mziray Katibu Mkuu wa Women and Poverty Alleviation in Tanzania ,
Akiwakaribisha wageni Mbalimbali waliofika katika Sherehe za Kuazimisha
Siku ya Wanawake Duniani ambapo wao wameadhimisha mapema,Katika Ufunguzi
Alisema kuwa Shirika lisilo ka Kiserikali la Waupata wakishirikiana na
OXFAM wamesaidia Kijiji hicho katika kuleta maendeleo mbalimbali Tangu
mwaka 2006 ikiwa ni pamoja na Kilimo cha mpunga, Matumizi Bora ya Ardhi,
Ambapo Pia aliwashukuru OXFAM kwa kuleta ufugaji bora wa kuku wa
kienyeji, na ujenzi wa masoko mawili ya kisasa, Pia kusaidia wanawake
kupata hati milili za Ardhi ambapo wanawake 186 watapata Hati hizo.
Mwisho alishukuru taasisi zengine zisizo za Kiserikali ikiwemo
Mviwata,Ungo,Tupawaki pamoja na Mwayodeo kwa jitihada zao za kusaidia
wanawake na wanakijiji cha Gongoni katika maendeleo ya kijiji hicho.
Mkurugenzi
Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiongea na wanakijiji cha Gongoni
pamoja na wageni waalikwa katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani
ikiwa ni wiki ya maadhimisho hayo, alipongeza harakati za kuwawezesha
wanawake katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na umiliki wa Ardhi,
ambapo alisema kuwa OXFAM itahakikisha kila aliyeomba hati ya Kumiliki
Ardhi ataipata, pia ameshukuru Taasisi zengine zisizo za kiserikali
kuendelea kusaidiana ili kuleta maendeleo.
Meza Kuu wakifurahia Burudani
Burudani ikiwa inaendelea
Baadhi ya wanakijiji wakipokea Hati Miliki za Ardhi
Wanakijiji wakipata vijarida
Wanakijiji cha Gongoni pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika Sherehe hizo
Hata watoto walikuwa bize wakisoma Vipeperushi na Vijarida
No comments:
Post a Comment