Waziri
wa Maliasili na Utalii wa Tanzania Mh.Lazoro Nyalandu akizungumza
wakati wa hafla ya siku ya Jumuia ya Afrika Mashariki iliyofanyika
katika banda la Tanzania katika maonesho ya ITB berlin Ujerumani
Waziri
Nyalandu katika picha ya pamoja na Mawaziri wenzake Mh. Phylis Kandie
(Wa pili kushoto), Waziri wa Maliasili na Mambo ya Kale wa Ugand Mh.
Maria Mutagamba (wa pili kulia) na wageni wengine mashuhuri katika banda
la Tanzania.
Kikundi
cha ngoma kutoka Kenya kikitumbuiza mawaziri, Mabalozi na wageni
mbalimbali waalikwa katika siku ya Jumuia ya Afrika Mashariki katika
banda la Tanzania.
……………………………………………………………….
Na: Geofrey Tengeneza – Berlin
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mheshimiwa Lazaro Nyalandu amesma kuwa serikali ya Tanzania inaamini
kuwa zuio lililowekwa na Serikali ya Kenya kwa magari ya utalii kutoka
Tanzania kuingia katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata litatatuliwa na
kuondolewa muda si mrefu kutokana na utayari wa kila nchi kukaa pamoaja
na kuzungumzia suala hilo kwa lengo la kuona kuwa ushirikiano katika
biashara ya utalii unaendelea kustawi kwa manufaa ya nchi hizi mbili na
jumuia ya Afrka Mashariki kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Waziri Nyalandu katika hafla ya siku ya Afrika
Mashariki katika maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya ITB Berlin
Ujerumani iliyofanyika katika banda la Tanzania na kuhudhuriwa na Waziri
wa Biashara na Utalii wa Kenya Mheshimiwa Phylis Kandie, Waziri wa
Utalii na Mambo ya Kale wa Uganda Mheshimiwa Maria Mutagamba,mabalozi
wanaowakilisha nchi za Afrika Mashariki nchini Ujerumani na wageni
wengine mashuhuri.
“Napenda kuchuka nafasi hii kuwahikishieni mliopo hapa na dunia
kwa ujumla kwamba hakuna tatizo lolote ambalo Tanzania na Kenya hatuwezi
kulitatua katika meza ya mazungumzo” alisema. Waziri Nyalandu amedokeza
kuwa tarehe 20 mwezi huu anatarajia kukutana Waziri Kandle wa Kenya
kuzungumzia suala hili ambapokabla ya hapo tarehe 18 Machi Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maliasili na utalii Dk. Adelhelm Meru atakutana na katibu
wa Wizara ya Biashara na Utalii ya Kenya.
No comments:
Post a Comment