Rais
Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi studio za
kisasa za Azam Media jijini Dar es Salaam leo. Rais Kikwete alizindua
studio hizo ambazo ni za kisasa zaidi zilizowahi kufunguliwa katika
nchi za Afrika Mashariki na Jangwa la Sahara zilizogharimu sh Bilioni
53. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media,
Tido Mhando, Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella
Mukangara na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Bakhresa, Said Salim
Bakhresa.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akilakiwa na Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Azam Media, Tido Mhando alipokwenda kuzindua rasmi studio za Azam Media
jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam
Media, Rhys Torrington. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa studio za Azam Media jijini Dar es Salaam leo. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Azam Media jijini Dar es Salaam leo. Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo,
Dk. Fenella Mukangara, uongozi wa Azam Media pamoja na baadhi ya wageni
waalikwa wakiangalia moja ya magari ya kurushia matangazo ya moja kwa
moja baada ya uzinduzi rasmi wa studio za kampuni hiyo jijini Dar es
Salaam leo. Wasanii
wa muziki wa kizazi kipya, Barnaba (kushoto)na Mwansiti Alimasi wakimba
wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Azam Media jijini Dar es
Salaam leo.
No comments:
Post a Comment