………………………………………………………………………….
Na: Geofrey Tengeneza – Berlin
Maonesho ya Utalii ya kimataifa ya ITB ya siku tano yameanza leo
jijini Berlin . Maonesho haya yanayofanyika kila mwaka na ambayo ni
makubwa kuliko yote duniani yanahudhuriwa na waoneshajio zaidi ya 10000
kutoka nchi 190 duniani.
Tanzania katika maonesho haya inawakilishwa na waoneshaji 160
kutoka katika makampuni 60 kutoka sekta ya umma na binafsi . Taasisi za
serikali zinazoshiriki maonesho haya ni Idara ya Utalii ya Wizara ya
Maliaslili na Utalii, Bodi ya utalii Tanzania (TTB) ambao ndio waratibu
wa ushiriki wa Tanzania katika maonesho haya. Nyingine ni Kamisheni ya
Utalii Zanzibar, Shirika la hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka
ya hifadhi ya ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Jumuia ya Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa Geofrey Meena Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii
Tanzania idadi ya makampuni na taaisi yanayoshiriki kutoka Tanzania
katika onesho la ITB imekuwa ikiongezeka kila mwaka ambapo mwaka huu
washiriki ni sitini (60) wakati mwaka jana jumla ya makampuni yalikuwa
hamsini na tatu (53).
Miongoni mwa matukio muhimu yanayotarajiwa ni pamoja na tukio la
siku ya Jumuia ya Afrika Mashariki katika maonesho haya litakayofanyika
tarehe 6/2/2015 ambapo Tanzania kama mwenyekiti wa jumuia hiyo itakuwa
mwenyeji wa tukio hilo litafanyika katika banda la Tanzania. Mawaziri wa
Utalii kutoka nchi wanachama, mabalozi wa nchi hizo hapa Ujerumani na
wageni wengine mbalimbali waalikwa wanatarajiwa kujumuika na mwenyeji
wao Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katika hafla hiyo
katika banda la Tanzania.
No comments:
Post a Comment