TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 8, 2012

KATIBU MKUU WIZARA YA AFRIKA MASHARIKI AZINDUA RIPOTI YA KIJIOGRAFIA

Naibu katibu mkuu wa wizara ya uhusiano wa Afrika mashariki. Bwana Uledi Mussa akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Ripoti kuhusu hali ya kijiogrofia katika nchi za jumuiya ya Afrika mashaki iliyoandaliwa na Benki ya dunia uzinduzi huo ulifanyika katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya wadau waliohudhuria kati uzinduzi ya ripoti hiyo.

MIUNDOMBINU YA MIFUGO SOKO LA NYAMATALA MISUNGWI HAIJAKAMILIKA KUWA SOKO LA KIMATAIFA

Mwenyekiti wa wafanyabishara wa mifugo Nyaga wa Nyaga akitoa mapendekezo ya wafanyabiashara kupinga kuhamia katika soko hilo kutokana na kutokamikilia kwa miundombinu huku Dkt Mugarula na Dkt Qwali wakitupia kisogo kamera wakiwa wameweka mikono nyuma kuashiria kushindwa kwa hoja zao. Wafanya biashara hao wamesema kama Wizara ya Mifugo na Uvuvi haitarekebisha kasoro ambazo ziko katika soko la Nyamatala, hawako tayari kuhama katika soko la Igoma ambako wanafanyia biashara yao kwa sasa, na kama watalazimishwa kuhama watasitisha kutoa huduma ya kuuza na kuchinja mifugo ili kuipa serikali ujumbe kuhusu kutatua tatizo hilo.
Choo kinachotarajiwa kutumiwa na wafanyabiashara wa mifugo pamoja na wateja mbalimbali watakaofika katika soko la Kimataifa la mnada wa Nyamatala, Misungwi Mwanza.Choo hicho kina matundu manne mawili kwa ajili ya wanawake na mengine kwa matumizi ya wanaume.
Trekta na bolzer la maji likiwa limeegeshwa katika soko la Kimataifa Nyamatala, Misungwi bolzer hilo linauwezo wa kubeba maji lita 4000, maji ambayo yatatumika kwa ajili ya kunywesha mifugo pamoja na matumizi ya choo
Jengo la kujikinga na mvua ama jua liliojengwa katika soko la mnada wa Kimataifa wa Nyamatala ,Misungwi Mkoani Mwanza, ambalo linalalamikiwa na wafanyabiashara wa mifugo kuwa ni dogo na halikidhi mahitaji ya soko hilo kulingana na hadhi yake.
Sehemu ya kunyweshea mifugo maji katika soko la mnada wa Kimataifa, Nyamatala wilayani Misungwi kama linavyoonekana.
Dkt Mugarula wa kwanza kushoto akisikiliza maswali kutoka kwa Joseph Sikila, Makamu Mwenyekiti wa MWASIBA aliysimama kulia.
Dkt Mugarula akijitetea mbele ya umati wa wafanyabiashara wa mifuko kwenye mkutano uliofanyika katika eneo la soko la kimataifa Nyamatala Misungwi, kushoto kwake ni misimamizi wa minada kanda ya ziwa dkt. Bura Qwali.
Ikengele Simon akimbana kwa maswali Dkt Mugarula. (PICHA NA MASHAKA BARTAZAR -MWANZA)

WAZIRI MKUU PINDA KUKUTANA NA MADKTARI UKUMBI WA CPL HOSPITALI YA MUHIMBILI KESHO SAA 3 ASUBUHI

Waziri Mkuu Mizengo Pinda
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA YUPO DAR ES SALAAM KUTOKA DODOMA KUSHUGHULIKIA MGOMO WA MADAKTARI AMBAO UMEKUWA UKIENDELEA KWA LENGO LA KUUPATIA UFUMBUZI. LEO AMEKUTANA NA UONGOZI WA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI PAMOJA NA MADAKTARI BINGWA KUTOKA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI NA WASTAAFU. KESHO SAA 3 ASUBUHI ATAKUTANA NA MADAKTARI BINGWA, MADAKTARI WALIOSAJILIWA (REGISTRALS) NA MADAKTARI WALIOKO KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNS) NA BAADA YA HAPO SAA 4 ATAKUTANA NA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA MUHIMBILI, MOI, OCEAN ROAD NA WAWAKILISHI KUTOKA HOSPITALI ZA MKOA WA DAR ES SALAAM, KWENYE UKUMBI WA CPL, MUHIMBILI. MATARAJIO YA SERIKALI NI KWAMBA MAZUNGUMZO HAYO YATAWEZA KUMALIZA MGOGORO HUU NA MADAKTARI WOTE KUREJEA KAZINI NA HIVYO KUREJESHA HUDUMA ZA MATIBABU KATIKA HALI YA KAWAIDA KWA WANANCHI WA TANZANIA. HIVYO SERIKALI INAWAOMBA WOTE WANAOHUSIKA WAFIKE KATIKA MIKUTANO HIYO BILA YA KUKOSA. (IMETOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

WANANCHI ARUSHA WALALAMIKA KUPORWA ARDHI

NA GLADNESS MUSHI - ARUSHA
WANANCHI wa kjiji cha Olkunjwado kilichopo kata ya Ngarenanyuki wilayani Arumeru wamemlalamikia mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Joseph Loibai kwa kosa la kuuza ardhi kinyume cha sheria sambamba na kutowasomea mapato na matumizi wananchi hao. Wakiongea na WAANDISHI WA HABARI baadhi ya wananchi ambao hawakupenda kutajwa majina yao walisema kuwa mwenyekiti huyo amakuwa na tabia ya kuuza maeneo ya watu wasiokuwa na uwezo kwa mzungu anaeishi katika kijiji hicho kwa manufaa yake binafsi Aidha walisema kuwa sheria ya ardhi inasema ardhi haiuzwi kiholela na hata kama basi itauzwa kuna asilimia ambayo itaenda serikalini lakini kwa mwenyekiti huyo ni tofauti na sheria hiyo. Mbali na hilo waliongeza kuwa kwa kipindi cha mwaka jana walimtaka mwenyekiti huyo kuwasomea wananchi hao mapato na matumizi kwa ajili ya michango mbali mbali wanaochanga kijijini hapo lakini hakufanya kama walivyokuwa wanataka wao. Waliongeza kuwa mapato hayo na matumizi waliyoomba kusomewa yanatokana na michango waliyochanga kwa ajili ya shule ya kutwa ya sekondari ya Momela na hadi sasa fedha hizo hazijulikani zilipo hali ambayo inawatia mashakani na mwenyekiti huyo ambapo hadi sasa wamekataa kuchanga michango mingine hadi wasomewe mapato hayo Hata hivyo walimtaka diwani wa kata hiyo kuitisha mkutano ili waweze kutoa kero zao kwa kuwa mwenyekiti huyo amekataa kusikiliza kero zao Aidha gazeti hili liliweza kuongea na mwenyekiti huyo kwa njia ya simu na kueleza kuwa hajauza ardhi kinyume cha sheria bali ni makubaliano yao wote waliopitisha kumpatia mzungu huyo eneo. Kwa upande wa kuwasomea mapato na matumizi alisema kuwa alishawaomea mapato na matumizi kwa kipindi cha nyuma ila mara ya mwisho koramu haikutimia hivyo kushindikana kusomewa kwa mapato hayo... .
UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI KUFANYIKA APRIL MOSI
Na Lydia Churi, MAELEZO
Uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki unatarajiwa kufanyika April Mosi mwaka huu.
Uchaguzi huo utafanyika baada ya jimbo hilo kuwa wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wake Marehemu Jeremia Solomon Sumari aliyefariki dunia Januari 19 mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi leo jijini Dar es salaam imesema pamoja na uchaguzi huo mdogo pia kutakuwepo na chaguzi ndogo za madiwani katika kata za Halmashauri mbalimbali nchini.
Taarifa hiyo ya Tume ya Taifa ya uchaguzi inaonesha kuwa katika uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye jimbo la Arumeru Mashariki uteuzi wa wagombea utafanyika Machi 8, na kampeni zitaanza Machi 9 hadi 31 mwaka huu.
Aidha, Tume hiyo pia itafanya chaguzi ndogo za madiwani katika kata nane zilizoko katika halmashauri mbalimbali nchini kufuatia kuwepo wazi kwa nafasi za viti vya madiwani ambazo zimetokana na vifo vya madiwani husika.
Katika chaguzi ndogo za madiwani uteuzi wa wagombea utafanyika Machi 5 na kampeni zitaanza Machi 6 hadi 31 mwaka huu. Kata zitakazohusika kwenye uchaguzi huo ni zile vijibweni-Temeke, Kiwanga-bagamoyo, Kirumba-Mwanza, Logangabilili-Bariadi, Chan’gombe-Dodoma, Kiwira-Rungwe, Lizaboni-Songea na Msambweni-Tanga.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva imesema kuwa hakutakuwa na kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya chaguzi hizo ila daftari la kudumu la wapiga kura lililotumika wakati wa uchaguzi mkuu uliopita litatumika.
Tume inawasisitiza wananchi na vyama vyote vya siasa kuzingatia na kufuata ratiba ya uchaguzi na kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi kuanzia siku ya uteuzi wa wagombea, kampeni za uchaguzi na siku ya kupiga kura. Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1.00 asubuhi na kufungwa saa 10.00 alasiri

BUNGE LAAHIRISHWA LEO HUKU HOJA YA MGOMO WA MADAKTARI IKIIBUKA KWA MARA YA SITA BUNGENI,SPIKA KUTOA UFAFANUZI KESHO.

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa wamesimama mara baada ya Naibu Spika wa Bunge Job Ndugay Kuahirisha kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.Pamoja na mambo mengine yaliyojitokeza wakati wa kuahirisha kikao hicho ni hoja ya Mgomo wa madaktari ambayo iliibuliwa na mbunge wa Kigoma mjini Peter Selukamba ambaye aliitaka serikali kutoa tamko la hatma ya mgomo huo ambapo Naibu spika Job Ndugay aliwataka wabunge kuwa na subira ili Ofisi ya spika ikutane na kamati ya uongozi ya bunge ili kutoa maamuzi hapo kesho kabla ya kuahirisha mkutano huo wa sita.
Aliyekuwa waziri mkuu na mbunge wa Monduli Edward Lowasa (kushoto) akijadili jambo na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira (katikati) na mbunge wa viti maalum CHADEMA Leticia Nyerere leo mjini Dodoma.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (Kulia) akizungumza na Zainabu Kawawa mbunge wa viti maalum CCM mara baada ya kumalizika kwa kikao cha saba cha bunge leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (katikati)akifurahia jambo na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (kulia) maarufu kwa jina la Sugu (CHADEMA) na mbunge wa Kigoma mjini Peter Selukamba (kushoto) nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugay akitekeleza majukumu yake wakati wa Kipindi cha maswali na majibu leo mjini Dodoma .

MAANDAMANO YA WANAHARAKATI KUSHINIKIZA SERIKALI KUCHUKUA HATUA JUU YA MGOMO WA MADAKTARI WA MUHIMBILI

 
Mkurugenzi wa TAMWA, Analilea Nkya akiwa ameshikilia bango lake wakati wa maandamano hayo jijini Dar es salaam leo.
Polisi wakiwaamuru waandamanaji watawanyike mara baada ya kufika katika eneo la Salender Brige jijini Dar es salaam leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba akizungumza na waandishi wa habari katika maeneo ya Salender Brige, kuelezea maadamano ya wanaharakati hao ya kuishinikiza serikali kuchukua hatua na kutatua mgogoro wa mgomo wa Madaktari wa Hospitali ya Muhimbili, ulioanza hivi karibuni na ambao bado unaendelea. Ameongeza kwamba hali ya wagonjwa inaendelea kuwa mbaya zaidi kwa sababu ya mgomo huo, Dk Hellen Kijo-Bisimba mara baada ya kumalizika kwa maandamano hayo yaliyofanyika leo. 

YANGA YAIGALAGAZA MTIBWA SUKARI 3 -1 UWANJA WA TAIFA LEO

 
Refarii wa mchezo huo akinyoosha mkono wake juu kuashiria timu ya Yanga ipige mpira wa adhabu kuelekea lango la timu ya Mtibwa Sugar.
Mmoja wa Mashabiki wa timu ya Yanga akiwa amejipaka masizi usoni mwake ikiwa ni moja ya staili ya ushangiliaji kwa timu yake.
Mchezaji wa timu ya Yanga Haruna Niyonzima akichuana na beki wa timu ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii jijini Dar es salaam, Mpira umekwisha na Yanga imefanikiwa kuitandika Mtibwa Sugar Magoli 3-0 bila huruma katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Tuesday, February 7, 2012

YANGA , MTIBWA KESHO NDO KESHO LIGI KUU VODACOM TANZANIA

Ligi Kuu ya Vodacom ambayo iko katika raundi ya 16 inaendelea kesho kwa mechi moja kati ya Yanga na Mtibwa Sugar. Mechi hiyo namba 112 itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.
Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Ibrahim Kidiwa kutoka Tanga wakati wasaidizi wake ni Michael Mkongwa kutoka Iringa na Kudura Omary wa Tanga. Kamishna wa mechi hiyo ni Mohamed Nyange kutoka Dodoma.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP B na C, na sh. 15,000 kwa VIP A.

Timu 14 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zitakuwa kwenye viwanja saba tofauti kesho (Februari 8 mwaka huu) katika mfululizo wa ligi hiyo ambayo iko katika hatua ya makundi.
Transit Camp na Mgambo Shooting zitachuana kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga katika mechi pekee ya kundi A itakayochezeshwa na mwamuzi Said Ndege wa Dar es Salaam.
Kundi B litashuhudia mechi tatu. Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji wa Small Kids kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, JKT Mlale itaoneshana kazi na Mbeya City kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea na Polisi Iringa itacheza na Majimaji kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa.
Mechi za kundi C zitakuwa kati ya Polisi Morogoro na Morani FC itakayochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, AFC na Rhino zitacheza kwenye Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha na Polisi Tabora itakuwa mwenyeji wa 94 KJ kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Kiongozi wa Olimpiki London 2012 Bw. Lord Sebastian Ceo atembelea shule ya sekondari kibasila

Kiongozi wa Olimpiki London 2012 Bw. Lord Sebastian Ceo akiwa katika picha ya pamoja na watoto baada ya kuwakabidhi vyeti katika ziara maalum aliyoifanya nchini Tanzania na kutembelea shule ya Sekondari ya Kibasila, ambako kuliandaliwa kliniki ya watoto kwa kuvumbua vipaji na kuwaandaa kwa ajili ya michezo ya Olimpiki katika siku za usoni, iliyojulikana kama Interanational Inspiration Tanzania na kushirikisha watoto kutoka shule mbalimbali jijini Dar es salaam, hapa wakionyesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa vyeti vyao na kiongozi huyo.
Kiongozi wa Olimpiki London 2012 Bw. Lord Sebastian Ceo akiruka viunzi pamoja na mtoto Aica Nicolaus wakati wa kiliniki hiyo kwenye viwanja vya shule ya Sekondari ya Kibasila.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kibasila wakicheza ngoma kumkaribisha kiongozi wa Olimpiki London 2012 Bw. Lord Sebastian Ceo.
Mmoja wa watoto akirusha Tufe mbele ya Kiongozi wa Olimpiki London 2012 Bw. Lord Sebastian Ceo wa tano kutoka kulia, hyuku viongozi wengine kutoka kamati ya Olimpiki nchini na Baraza la Michezo na ubalozi wa Uingereza nchini wakishuhudia tukio hilo.
Kiongozi wa Olimpiki London 2012 Bw. Lord Sebastian Ceo kulia akiangalia watoto wakati walipokuwa wakifanya mazoezi ya kuruka viunzi anayefuata katika picha ni Dk. Ndee na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC, Filbert Bay.
Watoto wakifanya mazoezi
Kutoka kulia ni Julie, Nelly Musembi na Vickie Maundu nao walihudhurika katika kiliniki hiyo ya International Inspiration Tanzania
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Mrs Aikande Urasa akimuongoza mgeni ambaye ni Kiongozi wa Olimpiki London 2012 Bw. Lord Sebastian Ceo kulia alipowasili katika shule hiyo katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC, Filbert Bay.

WAZIRI MKUU NA MATUKIO YANAYOENDELEA BUNGENI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mbunge wa Sumbawanga Mjini Khalfan Aeshi wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Februari 7,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Maswa Magalle Shibuda kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Februari 7, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais Dk Shein,Mgeni Rasmi Siku ya Sheria Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za siku ya Sheria,Zanzibar,(kulia) ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu,Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Abubakar Khamis,na Jaji Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Fakih Jundu,(kushoto) ambapo "kauli mbiu kuga vita Rushwa katika utowaji wa haki" ,sherehe hizo zilifanyika katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(kulia) akifuatana na Jaji mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu,(katikati) na Jaji Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Mhe.Fakih Jundu,alipowasili katika viwanja vya Victoria Garden katika sherehe za siku ya Sheria,Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu,Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Ali Abdalla Ali,(kulia) Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis,(kushoto)Jaji Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Fakih Jundu,na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Abubakar Khamis, wakiwa wamesimama wimbo wa taifa ukipigwa na kikundi cha polisi Brass Band katika sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar,zilizofanyika Victoria Gaden Mjini Unguja.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu,akiongoza maandamano ya majaji na wanasheria wa serikali na wakujitegemea wakati wa Sherehe za Siku ya Sheria,ambapo kauli Mbiu ya mwaka huu "Kupiga vita rushwa katika utowaji wa haki",sherehe hizo zilifanyika katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja leo.
Baadhi ya wananchi na viongozi mbali mbali walioalikwa katika sherehe za siku ya Sheria Zanzibar,ambvapo kila ifikapo Tr 7 Feb ya kila mwaka huadhimishwa kwa kusherehekea siku hiyo,hafla ya sherehe zilizofanyika katika, katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja leo.

Rais Jakaya Kikwete ashuhudia uwekaji saini makubaliano ya ushirikiano kupambana na maharamia

Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali washuhudia awaziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (shoto)na wa Tanzania Dr Hussein Mwinyi wakibadilishana nyaraka huku wa Afrika Kusini DKT L.N. Sisulu akitazama baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao. (PICHA NA IKULU)
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakishuhudia Mawaziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (kushoto), wa Tanzania Dr Hussein Mwinyi (wa pili kushoto), na wa Afrika Kusini DKT L.N. Sisulu wakitiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.
Rais Jakaya Kikwete akiongea huku Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Mawaziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (shoto), wa Tanzania Dr Hussein Mwinyi (wa pili kushoto), na wa Afrika Kusini DKT L.N. Sisulu baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiwa katika picha ya pamoja na na Mawaziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (shoto), wa Afrika Kusini DKT L.N. Sisulu na wa Tanzania Dkt Hussein Mwinyi baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiongea na Mawaziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (shoto), wa Tanzania Dr Hussein Mwinyi (wa pili kushoto), na wa Afrika Kusini DKT L.N. Sisulu baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.

Rais Jakaya Kikwete amuapisha Dr. James Msekela kuwa balozi Italy leo

Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi nyenzo za kazi Dkt James Msekela baada ya kuapishwa leo kuwa balozi wa Tanzania Italy ikulu jijini Dar es salaam . (PICHA NA IKULU)
Rais Jakaya Kikwete akimuapisha Dkt James Msekela kuwa balozi wa Tanzania Italy leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Gharib Mohamed Bilal na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa Mh John Haule (kulia) na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Penaeli Lyimo (kushoto) na Dkt James Msekela baada ya kuapishwa kuwa balozi wa Tanzania Italy leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Dr James Msekela na Familia yake baada ya kuapishwa kuwa balozi wa Tanzania Italy leo Ikulu jijini Dar
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakiongea na Dr James Nsekela na Mkewe baada ya Dr Msekela kula kiapo cha kuwa balozi wa Tanzania nchini Italy leo Ikulu jijini Dar es salaam
Dr James Msekela na Familia yake baada ya kuapishwa kuwa balozi wa Tanzania Italy leo Ikulu jijini Dar