NA GLADNESS MUSHI - ARUSHA
WANANCHI wa
kjiji cha Olkunjwado kilichopo kata ya Ngarenanyuki wilayani Arumeru wamemlalamikia mwenyekiti wa kijiji
hicho Bw Joseph Loibai kwa kosa la kuuza
ardhi kinyume cha sheria sambamba na kutowasomea mapato na matumizi wananchi hao.
Wakiongea na WAANDISHI WA HABARI baadhi ya
wananchi ambao hawakupenda kutajwa majina yao walisema kuwa mwenyekiti huyo amakuwa na
tabia ya kuuza maeneo ya watu wasiokuwa
na uwezo kwa mzungu anaeishi katika kijiji hicho kwa manufaa yake binafsi Aidha walisema kuwa sheria ya ardhi inasema ardhi
haiuzwi kiholela na hata kama basi
itauzwa kuna asilimia ambayo itaenda serikalini lakini kwa mwenyekiti huyo ni tofauti na sheria hiyo.
Mbali na hilo waliongeza kuwa kwa kipindi cha
mwaka jana walimtaka mwenyekiti huyo
kuwasomea wananchi hao mapato na matumizi kwa ajili ya michango mbali mbali wanaochanga kijijini hapo lakini
hakufanya kama walivyokuwa wanataka
wao. Waliongeza kuwa mapato hayo na
matumizi waliyoomba kusomewa yanatokana na michango waliyochanga kwa ajili ya shule ya kutwa
ya sekondari ya Momela na hadi sasa
fedha hizo hazijulikani zilipo hali ambayo inawatia mashakani na mwenyekiti huyo ambapo hadi
sasa wamekataa kuchanga michango mingine
hadi wasomewe mapato hayo Hata hivyo
walimtaka diwani wa kata hiyo kuitisha mkutano ili waweze kutoa kero zao kwa kuwa mwenyekiti huyo amekataa
kusikiliza kero zao Aidha gazeti hili
liliweza kuongea na mwenyekiti huyo kwa njia ya simu na kueleza kuwa hajauza ardhi kinyume cha sheria
bali ni makubaliano yao wote
waliopitisha kumpatia mzungu huyo eneo. Kwa upande wa kuwasomea mapato na matumizi alisema
kuwa alishawaomea mapato na matumizi kwa
kipindi cha nyuma ila mara ya mwisho koramu haikutimia hivyo kushindikana kusomewa kwa mapato
hayo... .
No comments:
Post a Comment